Kuanzisha ofa

Kwa kuanzisha ofa katika Dashibodi ya Google Play, unaweza kuwaruhusu wateja watumie programu inayolipishwa, bidhaa ya ndani ya programu au usajili bila kutozwa wanapotumia kuponi ya ofa. Kuna aina mbili za kuponi za ofa:

  • Kuponi za kutumiwa mara moja: Kuponi za kipekee zilizotengenezwa kiotomatiki ambazo zinaweza kutumiwa mara moja. Watumiaji wanaweza kutumia moja kwa moja kuponi zinazotumiwa mara moja kwenye Duka la Google Play au ndani ya programu.

  • Kuponi maalumu: Kuponi maalumu unazobainisha ambazo zinaweza kutumiwa mara nyingi au hadi kufikia kikomo ulichobainisha awali. Watumiaji wanaweza tu kutumia kuponi maalumu ndani ya programu. Kuponi maalumu zinaweza kutumiwa katika usajili pekee na watumiaji ambao hawajawahi kujisajili. Ni lazima ubainishe kwa watumiaji wako masharti ya kujiunga katika ofa kwa njia dhahiri.

Muhimu: Ni lazima uwe na uwazi kuhusu ofa zako. Hii inajumuisha kuwa dhahiri kuhusu sheria na masharti ya ofa yako. Watumiaji hawapaswi kutekeleza hatua nyingine yoyote ya ziada ili kusoma maelezo. Ili uhakikishe kuwa programu yako inatii sera zetu, pitia Sera yetu ya Usajili katika Kituo cha Sera za Wasanidi Programu.

Kuponi za ofa za usajili humpatia mtumiaji jaribio lisilolipishwa la kati ya siku 3 hadi 90. Unachagua aina ya usajili utakaoutengenezea kuponi za ofa na usajili wa mpango wa msingi ulio oanifu kwa matoleo ya awali unaotumika. Iwapo tayari ofa ina jaribio lisilolipishwa au ofa zingine, nafasi yake itabadilishwa na kuwa urefu wa jaribio lisilolipishwa la kuponi ya ofa.

Weka mipangilio ya ofa

Hatua ya kwanza: Tayarisha programu yako itumie kuponi za ofa

Usajili na ununuzi wa ndani ya programu: Kama unataka kuweka kuponi za ofa kwa ajili ya usajili au ununuzi wa ndani ya programu, unahitaji kuweka Ofa za Ndani ya Programu kwenye programu yako. Kumbuka kuwa huwezi kutumia kuponi za ofa katika bidhaa ambazo hazitumiki.

Programu zinazolipishwa: Ili kutoa kuponi za ofa kwa ajili ya programu zinazolipishwa, nenda kwenye Hatua ya 2.

Hatua ya 2: Kagua viwango na upatikanaji wa kuponi ya ofa

Ninaweza kuweka kuponi ngapi za ofa?

Viwango mbalimbali kwa kila robo ya mwaka vinatumika kwa kuponi za ofa zinazotumia na zisizotumia usajili. Kuponi za ofa zilizotengenezwa kwa ajili ya ofa za usajili hazihesabiwi katika kiwango chako cha ofa zisizo za usajili na vinginevyo.

Unaweza kuweka hadi kuponi 500 za ofa kwa kila robo ya mwaka kwenye ofa zote zisizo za usajili katika programu. Unaweza kutumia aina yoyote ya mseto wa kuponi za ofa za programu zinazolipishwa na za ofa za ndani ya programu, kama vile:

  • Kuponi 500 za ofa ya programu inayolipishwa
  • Kuponi 500 za ofa za bidhaa moja ya ndani ya programu
  • Kuponi 250 za ofa za programu zinazolipishwa + kuponi 250 za ofa za bidhaa moja ya ndani ya programu
  • Kuponi 100 za ofa za bidhaa tano za ndani ya programu

Unaweza kutumia ofa za usajili katika viwango vifuatavyo:

  • Kuponi zinazotumiwa mara moja: Kuponi 10,000 za ofa kwa kila robo kwa kila bidhaa inayolipiwa. 

  • Kuponi maalumu: Unaweza kuchagua kikomo cha kutumiwa wakati wa kuanzisha ofa, ambacho ni lazima kiwe kati ya kikomo kisichopungua 2,000 na kisichozidi 99,999.

Kumbuka: Baada ya kutengeneza ofa, huwezi kubadilisha idadi ya kuponi za ofa katika ofa hiyo wala kubadilisha kuponi za ofa ziwe za aina tofauti (kwa mfano, kubadilisha ofa ya programu inayolipishwa iwe ofa ya bidhaa inayodhibitiwa).

Ni nini kitafanyika kwenye kuponi zangu za kutumiwa mara moja mwishoni mwa robo ya mwaka?

  • Kuponi mpya: Iwapo ni siku ya kwanza ya robo mpya na umeshindwa kuweka kuponi mpya, subiri kwa saa 24 kisha ujaribu tena.
  • Kuponi ambazo hazijatumika: Iwapo hutumii kuponi zako zote za ofa katika robo moja, utapoteza uwezo wa kuzifikia. Kuponi za ofa zisizotumika haziwezi kuhamishiwa kwenye robo inayofuata.
  • Kuponi zilizochakatwa: Watumiaji wanaweza kutumia kuponi zao za ofa kwenye Google Play hadi tarehe ya mwisho ya ofa, uliyoweka katika Dashibodi ya Google Play. Ofa zinaweza kudumu kwa muda wa hadi mwaka mmoja.
Hatua ya 3: Kuweka ofa katika Dashibodi ya Google Play
  1. Fungua Dashibodi ya Google Play kisha uende kwenye ukurasa wa Kuponi za ofa (Chuma mapato > Kuponi za ofa).
  2. Bofya Tengeneza kuponi ya ofa.
  3. Kagua na ukubali Sheria na Masharti ya kuponi za ofa.
  4. Fuata maagizo kwenye skrini ili uipe jina ofa yako, uchague tarehe ya kuanza na kukamilika, uchague aina ya ofa na uweke idadi ya kuponi za ofa ambazo unataka kutengeneza.
  5. Iwapo unaweka ofa ya usajili, chagua aina ya usajili ambao utautengenezea kuponi ya ofa na muda wa jaribio lisilolipishwa. Kumbuka kwamba mpango wa msingi wa uoanifu kwa matoleo ya awali ya usajili unatumika.
  6. Iwapo unaweka kuponi maalumu, weka kuponi na kiwango cha kutumiwa. Yafuatayo ni baadhi ya mambo unayopaswa kuzingatia unapotengeneza kuponi maalumu:

    • Ni lazima kuponi maalumu ziwe za kipekee kwa kila programu, kumaanisha kuwa huwezi kuitumia tena katika programu ile ile kwenye kampeni tofauti. 

    • Ni lazima kuponi maalumu ziwe na herufi na nambari bila kujali kama ni herufi kubwa au ndogo.

    • Kuponi maalumu hazipaswi kuwa na vifungu au maneno yasiyofaa au yanayokera.

    • Tunapendekeza uweke mwaka au tarehe mwishoni mwa kuponi yako maalum ili kurahisisha kufuatilia wakati ambao kila kuponi ilianzishwa.

  7. Ili uruhusu ofa itumiwe kati ya tarehe ulizoweka za kuanza na kumalizika, weka hali iwe Inaendelea.
  8. Bofya Weka.
  9. Iwapo uliweka kuponi ya kutumiwa mara moja, subiri kwa sekunde kadhaa kisha uchague kiungo cha pakua. Kuponi zako zitapakuliwa kwenye faili ya thamani zilizotenganishwa kwa koma (.CSV). Ili ushiriki na watumiaji, unaweza kuchapisha kuponi au utume kiungo kinachoruhusu watumiaji kutumia kuponi kupitia barua pepe au arifa katika programu yako.

Kulinganisha kuponi za ofa na ofa kwa ajili ya usajili

Unaweza kutoa ofa na kuponi za ofa mbalimbali kulingana na mahitaji ya biashara yako:

  Ofa ya kupata mteja mpya Ofa ya Toleo jipya Ofa zilizobainishwa na msanidi programu Kuponi ya ofa ya kutumiwa mara moja Kuponi ya ofa maalumu
Madhumuni Pata watumiaji wapya Watumiaji wa usajili wa kiwango cha juu, kiwango cha chini na wa kiwango cha kati Unaamua Pata watumiaji na uwadumishe Pata watumiaji wapya
Manufaa Jaribio lisilolipishwa na au awamu za bei ya utangulizi Jaribio lisilolipishwa na au awamu za bei ya utangulizi Jaribio lisilolipishwa na au awamu za bei ya utangulizi Jaribio moja lisilolipishwa Jaribio moja lisilolipishwa
Masharti ya Kujiunga Watumiaji wapya Watumiaji waliopo Unaamua Watumiaji wapya, waliopo, au waliokuwepo awali Watumiaji wapya
Ugunduzi na ununuzi Ndani ya programu yako au Play Store Ndani ya programu yako au Play Store Ndani ya programu yako pekee Sambaza kupitia njia yoyote. Tumia ndani ya programu yako au Duka la Google Play. Ndani ya programu yako pekee

 

Kagua na usasishe ofa

Katika Dashibodi ya Google Play, unaweza kufikia ofa zinazoendelea na zilizositishwa.

  • Zinazoendelea: Watumiaji wanaweza kutumia kuponi za ofa kwa sababu iko katika kipindi cha tarehe ya mwanzo na mwisho wa ofa.
  • Zilizositishwa: Watumiaji hawawezi kutumia kuponi za ofa zako hadi utakaporejesha ofa. Katika ukurasa wako wa Ofa kwenye Dashibodi ya Google Play, hakikisha umeweka hali ya Inaendelea na uweke tarehe ya mwisho.

Kumbuka: Baada ya tarehe ya mwisho wa ofa, muda wa kutumia kuponi ya ofa utaisha. Baada ya muda wa kutumia kuponi ya ofa kuisha, watumiaji hawataweza kutumia kuponi na hutaweza kuona wala kusasisha kuponi kwenye Dashibodi ya Google Play.

Kusasisha ofa inayoendelea au iliyositishwa
  1. Fungua Dashibodi ya Google Play kisha nenda kwenye ukurasa wa Kuponi za ofa (Chuma mapato > Kuponi za ofa).
  2. Pembeni mwa ofa unayotaka kuibadilisha, bofya Tazama ofa.
  3. Unaweza kufanya usasishaji kwenye jina, tarehe ya kuanza na kumalizika na hali ya ofa (zilizositishwa au zinazoendelea).
    • Sasisha tarehe ya kuanza: Iwapo utabadilisha tarehe ya kuanza kwa ofa kuwa katika wakati ujao, utasimamisha ofa hadi tarehe hiyo.
    • Sasisha tarehe ya mwisho: Unaweza tu kusasisha tarehe ya mwisho wa ofa iwe katika wakati ujao.
    • Sitisha ofa: Unaweza kubofya Sitisha ofa kwenye sehemu ya juu kulia ya ukurasa. Watumiaji hawataweza kutumia kuponi za ofa kwa ofa hii hadi utakapoianzisha tena.

Je, maelezo haya yamekufaa?

Tunawezaje kuboresha?

Je, unahitaji usaidizi mwingine?

Jaribu hatua zifuatazo:

Tafuta
Futa utafutaji
Funga kisanduku cha kutafutia
Menyu kuu
7294452422369942946
true
Tafuta kwenye Kituo cha Usaidizi
true
true
true
true
true
92637
false
false