Jinsi ya kuanza kutumia Dashibodi ya Google Play

Makala haya yanafafanua jinsi ya kufungua na kuweka mipangilio ya akaunti yako ya msanidi programu ya Dashibodi ya Google Play, na yanatoa viungo vya nyenzo nyingine zinazoweza kukufaa unapoanza.

Kusajili akaunti ya Msanidi Programu wa Google Play

Fuata hatua zilizo hapa chini ili ufungue na uweke mipangilio ya akaunti yako ya msanidi programu ya Dashibodi ya Google Play, ili uweze kuanza kuchapisha programu za Android kwenye Google Play.

Hatua ya 1: Fungua akaunti ya msanidi programu ya Dashibodi ya Google Play

Ni lazima uwe na angalau umri wa miaka 18 ili ufungue akaunti ya Msanidi Programu wa Google Play.

  1. Kwa kutumia Akaunti yako ya Google, fungua akaunti ya msanidi programu ya Dashibodi ya Google Play.
  2. Baada ya kufungua akaunti, unaweza kutumia Dashibodi ya Google Play kuchapisha na kudhibiti programu zako.
Hatua ya 2: Kubali Mkataba wa Usambazaji kwa Wasanidi Programu

Wakati wa kujiandikisha, utahitaji kukagua na kukubali Mkataba wa Usambazaji kwa Wasanidi Programu wa Google Play.

Hatua ya 3: Lipa ada ya usajili

Kuna ada inayolipwa mara moja ya $25 za Marekani. Unaweza kulipa ada hii kwa kutumia kadi za malipo au mikopo zifuatazo:

  • MasterCard
  • Visa
  • American Express
  • Discover (Marekani pekee)
  • Visa Electron (Nje ya mipaka ya Marekani pekee)

Kumbuka: Kadi za kulipia mapema hazikubaliwi. Aina za kadi zinazokubaliwa zinaweza kutofautiana kulingana na mahali.

Hatua ya 4: Chagua aina ya akaunti ya msanidi programu

Chagua aina ya akaunti unayotaka kufungua. Google Play inatoa aina mbili za akaunti za wasanidi programu, Akaunti ya Binafsi na ya Shirika, ambazo unaweza kupata maelezo zaidi kuzihusu hapa.

Kumbuka: Wasanidi programu walio na akaunti za binafsi za msanidi programu lazima watimize masharti fulani ya majaribio ya programu kabla waweze kusambaza programu zao kwenye Google Play. Kwa maelezo zaidi, nenda kwenye (Akaunti za binafsi pekee) Hatua ya 6: Thibitisha maelezo ya utambulisho wako wa msanidi programu.

Hatua ya 5: Thibitisha maelezo ya utambulisho wako wa msanidi programu

Kama sehemu ya juhudi zetu endelevu za kufanya Google Play kuwa mfumo salama na unaoaminika, sharti ukamilishe uthibitishaji uliofafanuliwa kwenye ukurasa huu unapoweka mipangilio ya akaunti yako ya msanidi programu ya Dashibodi ya Google Play. Hii hutusaidia kuelewa vyema wasanidi programu na hutuwezesha kuwazuia wadukuzi wasisambaze programu hasidi. Masharti ya uthibitishaji yanatofautiana kulingana na aina ya akaunti unayochagua katika Hatua ya 4.

Unaweza kuweka taarifa zaidi ya akaunti baada ya kufungua akaunti yako.

Kumbuka: Ili kuchakata ombi lako la Akaunti ya Msanidi Programu wa Google Play huenda ukaombwa kutoa kitambulisho sahihi cha serikali na kadi ya mikopo, vyote vikiwa na jina lako. Ikiwa tutabaini kuwa maelezo haya si sahihi, hatutakurejeshea pesa za ada ya usajili.

(Akaunti za binafsi pekee) Hatua ya 6: Timiza masharti ya majaribio na uthibitishaji wa kifaa

Wasanidi programu walio na akaunti za binafsi zilizofunguliwa kabla ya tarehe 13 Novemba 2023, lazima watimize masharti mahususi ya kujaribu kabla ya kuchapisha programu zao kwenye Google Play. Soma makala haya ya Kituo cha Usaidizi ili upate maelezo zaidi.

Kuanzia mwanzoni mwa 2024, wasanidi programu walio na akaunti mpya za binafsi watahitajika kuthibitisha kwamba wanafikia kifaa cha Android kwa kutumia programu ya vifaa vya mkononi ya Dashibodi ya Google Play kabla ya kufanya programu zao zipatikane kwenye Google Play. Soma makala haya ya Kituo cha Usaidizi ili upate maelezo zaidi. 

Kusanidi programu za Android

Unaweza kupata maelezo kuhusu jinsi ya kubuni, kusanidi na kusambaza programu zako za Android kwenye Google kupitia viungo muhimu vilivyo hapa chini:

Vipengele maarufu

Kwa maelezo zaidi kuhusu baadhi ya vipengele maarufu zaidi, bofya viungo vilivyo hapo chini:

Mpya

Hizi ni baadhi ya nyenzo maarufu zilizo na habari na vidokezo vipya kuhusu usanidi wa programu na michezo ya Android kwenye Google Play.

Tatua

Je, unahitaji usaidizi wa kuchapisha programu kwenye Google Play? Zifuatazo ni baadhi ya kurasa ambazo unaweza kutembelea ili upate usaidizi wa ziada:

Kumbuka: Timu yetu ya usaidizi inaweza kukusaidia utumie Dashibodi ya Google Play lakini haiwezi kutoa usaidizi wa kiufundi au usanidi.

Je, maelezo haya yamekufaa?

Tunawezaje kuboresha?

Je, unahitaji usaidizi mwingine?

Jaribu hatua zifuatazo:

Tafuta
Futa utafutaji
Funga kisanduku cha kutafutia
Menyu kuu
15519605744604864748
true
Tafuta kwenye Kituo cha Usaidizi
true
true
true
true
true
92637
false
false