Unganisha akaunti yako ya msanidi programu kwenye huduma za Google

Unaweza kuunganisha Akaunti yako ya Msanidi Programu wa Google Play kwenye akaunti na huduma zilizochaguliwa. Ikiwa ni pamoja na Google Ads, Google Marketing Platform, Firebase na Kituo cha malipo ya Google.

Unganisha akaunti au miradi

Google Ads

Wamiliki wa akaunti za Dashibodi ya Google Play wanaweza kutuma maombi ya kuunganisha akaunti kutoka Dashibodi ya Google Play kwenda kwa akaunti za Google Ads ili kutoa ruhusa ya kufanya kampeni zinazolenga watumiaji.

Utaratibu wa kuunganisha

Unapounganisha akaunti ya Google Ads na ya Msanidi programu wa Google Play, wamiliki wa akaunti za Google Ads wataweza kufikia orodha za utangazaji tena zinazozalishwa kiotomatiki kwa programu zilizochapishwa kwenye akaunti yako ya msanidi programu.

Unaweza kuondoa akaunti iliyounganishwa wakati wowote. Iwapo akaunti iliyounganishwa imeondolewa, orodha za utangazaji tena kutoka Google Ads ambazo zinatokana na programu zilizopo katika akaunti ya msanidi programu iliyounganishwa zitazimwa na huenda matangazo yoyote yanayolenga orodha hizo yasionyeshwe. Kwa maelezo zaidi ya jinsi ya kuunganisha akaunti ya Google Ads na akaunti ya msanidi programu, tembelea Kituo cha Usaidizi cha Google Ads.

Kutuma maombi ya kuunganisha

  1. Fungua Dashibodi ya Google Play kisha uende kwenye ukurasa wa Huduma zilizounganishwa  (Mipangilio > Huduma zilizounganishwa).
  2. Chini ya "Google Ads," bofya Unganisha Akaunti ya Google Ads.
  3. Weka kitambulisho cha mteja wa Google Ads.

Ombi la barua pepe litatumwa kwenye akaunti ya Google Ads. Wasimamizi wa akaunti ya Google Ads wanaweza kukagua maombi ya kuunganisha akaunti kwa kuingia katika Akaunti zao za Google Ads na kubofya Mipangilio > Huduma zilizounganishwa.

Firebase

Utaratibu wa kuunganisha

Iwapo unatumia Firebase kuunda programu za Android, unaweza kuunganisha Programu yako ya Android ya Firebase kwenye akaunti ya msanidi programu wa Google Play ili uruhusu yafuatayo:

  • Usambazaji wa Programu: kuweza kutumia Android App Bundle
    • Unapopakia App Bundle kwenye mchakato wa Usambazaji wa Programu, hutumwa kwenye Google Play ili kutengeneza APK ambayo imeboreshwa kwa ajili ya usanidi wa kifaa cha mchunguzaji wa programu yako.
  • Crashlytics: shiriki data ya programu na matukio ya kuacha kufanya kazi
    • Fikia data ya uthabiti na programu yako kwenye Google Play katika huduma ya Crashlytics ili upate mwonekano bora zaidi wa uthabiti wa programu yako. Data ya huduma yako ya Crashlytics inaweza pia kuendesha vipengele kwenye Dashibodi ya Google Play. Pata maelezo zaidi
  • Google Analytics: shiriki data ya hadhira na mapato

Unganisha au tenganisha programu

Unaweza kuunda na kudhibiti viongo vya Programu za Firebase kwenye akaunti za msanidi programu wa Google Play kwa kutumia dashibodi ya Firebase (Mipangilio ya mradi > Ujumuishaji > Google Play). Tembelea Kituo cha Usaidizi cha Firebase ili upate maelezo zaidi.

Unaweza kutenganisha Programu ya Firebase na akaunti ya msanidi programu wa Google Play kwa kutumia Dashibodi ya Google Play au Dashibodi ya Firebase.

Yafuatayo yatafanyika kwa programu ambayo imetenganishwa:

  • Data yoyote iliyohamishwa hapo awali inaweza kuendelea kupatikana kwenye bidhaa za mpokeaji.
  • Shughuli zote za uhamishaji wa data kati ya programu ya Firebase na Google Play kupitia michakato husika ya ujumuishaji wa bidhaa zitakoma. 
  • Ikiwa programu iliunganishwa kupitia mchakato wa ujumuishaji wa Usambazaji wa Programu, hutaweza tena kupakia App Bundle mpya kwenye Usambazaji wa Programu na kuzituma kwenye Google Play kupitia mchakato wa ujumuishaji wa Usambazaji wa Programu.
  • Ikiwa programu iliunganishwa kupitia mchakato wa ujumuishaji wa Google Analytics, shughuli zote za utumaji wa data ya mapato na watumiaji kati ya Google Play na Google Analytics kupitia mchakato huu wa ujumuishaji zitakoma.

Kabla ya kuanza

Ili uunganishe Programu ya Firebase na akaunti ya msanidi programu wa Google Play, hakikisha:

Ili utenganishe Programu ya Firebase kwenye akaunti ya msanidi progamu wa Google Play, hakikisha:

Hatua

Fahamu jinsi ya kuunganisha Programu ya Firebase na akaunti ya msanidi programu wa Google Play kwenye Kituo cha Usaidizi cha Firebase. Pia ina maelezo kuhusu jinsi unavyoweza kutenganisha akaunti yako pamoja na maelezo mengine muhimu.

Ikiwa unachagua kutenganisha Programu yako ya Android kwenye Firebase kwa kutumia Dashibodi ya Google Play, fuata hatua hizi:

  1. Fungua Dashibodi ya Google Play, kisha uende kwenye ukurasa wa Huduma zilizounganishwa (Mipangilio > Huduma zilizounganishwa).
  2. Chini ya "Firebase", chagua Tenganisha.
Google Marketing Platform

Iwapo wewe (au shirika la kutangaza unalofanyia kazi) ungependa kutumia Campaign Manager 360 au Display & Video 360 kufuatilia wanaoshawishika kusakinisha programu, unaweza kutuma ombi la kuunganisha akaunti kutoka kwenye akaunti ya Google Marketing Platform kwenda kwenye akaunti yako ya msanidi programu wa Google Play.

Muhimu: Maombi ya kuunganisha yanahitaji kutumwa kutoka kwenye CM360 au Display & Video 360 na yaidhinishwe katika Dashibodi ya Google Play. Unaweza tu kukubali, kukataa au kuondoa maombi katika Dashibodi ya Google Play.

Unaweza kuondoa akaunti iliyounganishwa wakati wowote. Iwapo akaunti iliyounganishwa imeondolewa, kipengele cha Google Marketing Platform cha kufuatilia programu kutoka kwenye akaunti iliyounganishwa ya msanidi programu kitazimwa.

Kagua maombi ya kuunganisha

Baada ya msimamizi wa akaunti kutuma ombi ya kuunganisha akaunti ya Google Ads au ya Google Marketing Platform kwenye akaunti yako ya msanidi programu, utapokea arifa ya barua pepe. Unaweza pia kukagua maombi kwenye ukurasa wa Mipangilio ya Dashibodi ya Google Play.

  1. Fungua Dashibodi ya Google Play kisha uende kwenye ukurasa wa Huduma zilizounganishwa  (Mipangilio > Huduma zilizounganishwa).
  2. Chini ya "Vitendo," idhinisha au ukatae ombi la kuunganisha.

Batilisha viungo kwenye akaunti nyingine

Ili uondoe viungo kwenye akaunti za Google Ads au Google Marketing Platform:

  1. Fungua Dashibodi ya Google Play kisha uende kwenye ukurasa wa Huduma zilizounganishwa  (MipangilioHuduma zilizounganishwa).
  2. Chini ya "Vitendo," bofya Tenganisha akaunti.

Maudhui yanayohusiana

Unganisha Akaunti ya Msanidi Programu wa Google Play kwenye taarifa za malipo.

Je, maelezo haya yamekufaa?

Tunawezaje kuboresha?

Je, unahitaji usaidizi mwingine?

Jaribu hatua zifuatazo:

Tafuta
Futa utafutaji
Funga kisanduku cha kutafutia
Menyu kuu
134747188894518943
true
Tafuta kwenye Kituo cha Usaidizi
true
true
true
true
true
92637
false
false