Kuorodhesha Programu kwenye Huduma ya Tafuta na Google

Kwa kutumia kipengele cha Ujumuishaji wa Programu katika Faharasa, watumiaji waliosakinisha programu yako wanaweza kufungua viungo kutoka huduma ya tafuta na Google kwa vifaa vya mkononi moja kwa moja katika programu yako.

Omba uhusiano kati ya programu na tovuti yako

Ili uwashe Ujumuishaji wa Programu katika Faharasa, lazima kwanza uweke mipangilio ya viungo vya kina. Kisha, unaweza kuanzisha uhusiano kati ya programu na tovuti yako yenye maudhui ya programu. Zifuatazo ni hatua za kuanza kuomba uhusiano:

  1. Ingia katika akaunti ya Dashibodi ya Google Play.
  2. Bofya Programu zote.
  3. Chagua programu ambapo ungependa kuomba uhusiano.
  4. Kwenye menyu ya kushoto, bofya MipangilioMipangilio ya kina.
  5. Chini ya "Ujumuishaji wa Programu katika Faharasa," bofya Weka tovuti.
  6. Weka URL ya ukurasa wa kwanza. Tunapendekeza uondoe itifaki (HTTP au HTTPS) na uandike jina la kikoa pekee (kwa mfano, "abcxyz.com").
  7. Bofya Tuma ombi la uthibitishaji.
  8. Ombi litatumwa kwa mmiliki wa tovuti katika Dashibodi ya Utafutaji. Ikiwa akaunti ya Dashibodi ya Google Play na akaunti ya Dashibodi ya Utafutaji ni ile ile, uhusiano unaweza kuidhinishwa kiotomatiki mara moja. Vinginevyo:
    • Ikiwa wewe ni mmiliki wa tovuti kwenye Dashibodi ya Utafutaji, unaweza kubofya "Kubali" katika ujumbe kisha uidhinishe ombi. Unaweza pia kwenda kwenye ukarasa wa uhusishaji wa Dashibodi ya Tafuta na Google  na uidhinishe ombi.
    • Ikiwa wewe si mmiliki wa tovuti katika Dashibodi ya Utafutaji, utasubiri mmiliki aidhinishe ombi lako.
Kumbuka: Ikiwa kuna mali mbalimbali za Dashibodi ya Utafutaji zinazohusiana na tovuti hii (kwa mfano, kuna mali za Dashibodi ya Utafutaji za "http://abcxyz.com na https://abcxyz.com") na uliomba uhusiano bila itifaki "abcxyz.com"), basi Google Play itachagua kuhusisha mojawapo ya mali hizi za Dashibodi za Utafutaji.

Ondoa uhusiano wa tovuti

Kuna njia mbili za kufuta uhusiano na unahitaji tu kutumia mojawapo kuondoa au kutohusisha tovuti.

Kwenye Dashibodi ya Google

  1. Ingia katika akaunti ya Dashibodi ya Google Play.
  2. Bofya Programu zote.
  3. Chagua programu ambapo ungependa kughairi uhusiano.
  4. Kwenye menyu ya kushoto, bofya MipangilioMipangilio ya kina.
  5. Chagua kichupo cha "Ujumuishaji wa Programu katika Faharasa".
  6. Karibu na tovuti ambayo ungependa kuondoa, bofya Ondoa.

Kutoka kwenye Dashibodi ya Utafutaji

Kumbuka: Lazima uwe mmiliki wa mali (tovuti) hii ya Dashibodi ya Utafutaji ili udhibiti kipengele hiki.
  1. Fungua ukurasa wa Mipangilio ya uhusishaji kwenye Dashibodi ya Utafutaji.
  2. Pata uhusiano ambao ungependa kufuta kwenye jedwali.
  3. Chagua aikoni ya mipangilio zaidiZaidina ubofye Ondoa uhusiano.

Unaweza kupata maelezo zaidi kuhusu Uhusiano kwenye Usaidizi wa Dashibodi ya Utafutaji.

Je, maelezo haya yamekufaa?

Tunawezaje kuboresha?

Je, unahitaji usaidizi mwingine?

Jaribu hatua zifuatazo:

Tafuta
Futa utafutaji
Funga kisanduku cha kutafutia
Menyu kuu
1777917035400123960
true
Tafuta kwenye Kituo cha Usaidizi
true
true
true
true
true
92637
false
false