Programu yako inaweza kugunduliwa kwenye huduma ya utafutaji kwenye Google Play

Huduma ya utafutaji kwenye Google Play ni zana kuu inayowasaidia watumiaji kupata programu zinazowafaa na maarufu kwa ajili ya vifaa vya Android. Kuhakikisha kuwa programu na ukurasa wa programu yako katika Google Play ni kamilifu na umeboreshwa ni kigezo muhimu cha kugunduliwa na watumiaji kwenye Google Play.

Unda ukurasa wa programu katika Google Play ambao una maelezo ya kina

Maandishi kwenye ukurasa wa programu yako katika Google Play husaidia watumiaji kugundua programu yako. Pia ni sehemu muhimu ya kuunda ukurasa wa programu katika Google Play ambao unaridhisha. Zingatia vidokezo vifuatavyo unapoboresha ukurasa wa programu yako katika Google Play:

Jina

  • Jina la programu yako linapaswa kuwa la kipekee na la kufikika, usitumie maneno ya kawaida na utilie mkazo kile ambacho programu yako itatekeleza.
  • Hakikisha unatumia jina dhahiri. Majina marefu yanaweza kufupishwa kwenye baadhi ya vifaa vinavyotumiwa na watumiaji wako kuvinjari.
  • Usitumie maendelezo yasiyo sahihi ya maneno ya kawaida kwani watumiaji wanaweza kuishia kusahihisha tahajia katika utafutaji.
  • Usitumie herufi za ascii au emoji nyingi mno kwenye jina la programu yako. Watumiaji wa programu kama vile visoma skrini au programu za kudhibiti kwa sauti watakumbana na matatizo iwapo utatumia maandishi ya ascii au emoji nyingi mno.

Maelezo

  • Zingatia watumiaji wako na watakachokipata kwa kutumia programu yako.
  • Kagua maelezo ya programu yako kwenye programu ya Google Play na duka la wavuti ili uhakikishe kuwa maandishi muhimu zaidi yanaonekana kwenye nusu ya juu ya ukurasa wa wavuti ambapo watumiaji hawahitaji kusogeza chini.
  • Tumia Mbinu bora za kuimarisha upatikanaji kwenye injini za utafutaji katika "Maelezo" yako, lakini zingatia Sera za Maudhui ya Google Play kuhusu taka na Ukiukaji wa Haki za Uvumbuzi (kwa mfano, kufanya taka za maneno muhimu, uigaji, n.k.).
  • Usitumie herufi za ascii au emoji nyingi mno kwenye maelezo ya programu yako. Watumiaji wa programu kama vile visoma skrini au programu za kudhibiti kwa sauti watakumbana na matatizo iwapo utatumia maandishi ya ascii au emoji nyingi mno.

Maandishi ya Tangazo

  • Weka maelezo mafupi ya mstari mmoja ili kufafanua programu yako. 

Vipengee vya Picha na Vipicha

Aikoni za programu, picha na picha za skrini husaidia kufanya programu yako ionekane kwa urahisi katika matokeo ya utafutaji, aina na orodha za programu husika katika Google Play.

Ingawa si vipengee vyote vya picha vinavyotakiwa kwenye ukurasa wa programu katika Google Play, tunapendekeza uweke picha bora za skrini zinazoonyesha aina za vifaa vinavyoweza kutumia programu yako (kwa mfano, simu, kishikwambi cha inchi 7, kishikwambi cha inchi 10).

Hakikisha kuwa kila picha ya skrini ina matini mbadala ya kipekee. Matini mbadala hufanya iwe rahisi kwa watumiaji wa visoma skrini kufuatilia lengo la kila picha uliyojumuisha kwenye chapisho lako. Tumia fursa hii kuwasiliana na mtu ambaye hawezi kuona picha zako za skrini na umsaidie kuelewa matumizi ya programu yako kwa sentensi moja au mbili.

Kuunda vipengele anuwai kwa ajili ya watumiaji wako

Kujanibisha ukurasa wa programu yako katika Google Play

Google huweka tafsiri zilizofanywa na mashine kiotomatiki kwenye kurasa za programu katika Google Play. Tafsiri hizi hazitimizi mahitaji ya programu yako. Hata hivyo, kutumia huduma za tafsiri kutoka kwa wataalamu ili watafsiri "Maelezo ya programu yako" kunaweza kuleta matokeo bora ya utafutaji na uwezo wa kutambulika kwa watumiaji ulimwenguni kote. Katika Dashibodi ya Google Play, unaweza kulipia huduma za watafsiri wataalamu kutoka kwa wauzaji wengine.

Vigezo vya ziada vya utafutaji

Kuweka hali bora ya utumiaji

Utafutaji kwenye Google Play huzingatia hali ya jumla ya matumizi ya programu yako kulingana na shughuli na maoni ya watumiaji. Programu zinakadiriwa kulingana na muunganiko wa alama za makadirio, maoni, vipakuliwa na vigezo vingine. Ingawa maelezo ya vipimo na thamani hizi unamilikiwa kama sehemu ya algoriti ya Tafuta na Google, unaweza kufanya juhudi ili uboreshe uonekanaji wa programu yako kwa:

  • Kuunda hali ya utumiaji inayodumu na yenye maana kwa watumiaji wako
  • Kudumisha na kuboresha programu yako kupitia masasisho ya mara kwa mara
  • Kuhamasisha watumiaji kutoa maoni kwa njia ya ukadiriaji na maoni
  • Kutoa huduma nzuri kwa wateja kwa kuwajibu watumiaji wako na kushughulikia matatizo

Je, maelezo haya yamekufaa?

Tunawezaje kuboresha?

Je, unahitaji usaidizi mwingine?

Jaribu hatua zifuatazo:

Tafuta
Futa utafutaji
Funga kisanduku cha kutafutia
Menyu kuu
12255073424064034004
true
Tafuta kwenye Kituo cha Usaidizi
true
true
true
true
true
92637
false
false