Ukaguzi wa Mapema: Kuhatarisha Maisha ya Watoto

Toleo Tangulizi la sera (kuanza kutumika tarehe 31 Januari, 2025)

Makala haya yanatanguliza mabadiliko katika masasisho ya Aprili 2024 ya sera yetu.

Tunaanzisha Sera ya Viwango vya Usalama wa Watoto inayohitaji programu za Kijamii na za Kuchumbiana kufuata viwango mahususi na kuthibitisha zenyewe kuwa zinatii sera hii kwenye Dashibodi ya Google Play kabla ya kuchapishwa.

Ili uangalie makala ya sasa ya "Kuhatarisha Maisha ya Watoto", tembelea ukurasa huu.

Programu ambazo hazizuii watumiaji kutengeneza, kupakia au kusambaza maudhui yanayowezesha unyanyasaji wa watoto zitaondolewa mara moja kwenye Google Play. Hii ni pamoja na maudhui yote yanayoonyesha unyanyasaji wa watoto kingono. Ili uripoti maudhui yaliyo kwenye bidhaa ya Google yanayoweza kumnyanyasa mtoto, bofya Ripoti matumizi mabaya. Iwapo utapata maudhui mahali pengine kwenye intaneti, tafadhali wasiliana moja kwa moja na shirika husika katika nchi yako

Tunazuia matumizi ya programu ili kuwahatarisha watoto. Ikiwa ni pamoja na lakini si tu, matumizi ya programu kuendeleza tabia za kuwanyemelea watoto, kama vile:

  • Matendo yasiyofaa yanayowalenga watoto (kwa mfano, kuwapapasa au kuwagusa).
  • Kumpevua mtoto (kwa mfano, kuanzisha urafiki na mtoto mtandaoni ili kuwezesha mtagusano wa kingono mtandaoni na/au kubadilishana picha za ngono na mtoto huyo mtandaoni au nje ya mtandao).
  • Kuwafanya watoto wachukuliwe kwa mtazamo wa kingono (kwa mfano, picha zinazoonyesha, kuhimiza au kuendeleza unyanyasaji wa kingono dhidi ya watoto au kuwaonyesha watoto kwa namna inayoweza kusababisha unyanyasaji wa watoto kingono).
  • Dhuluma inayohusiana na masuala ya ngono (kwa mfano, kumtishia au kumhadaa mtoto kwa kutumia uwezo halisi au unaokisiwa wa kufikia picha nyeti za mtoto).
  • Ulanguzi wa mtoto (kwa mfano, utangazaji au kumshawishi mtoto kwa ajili ya biashara ya unyanyasaji wa kingono).

Tutachukua hatua stahiki, ikiwemo kutoa ripoti katika shirika la National Center for Missing & Exploited Children, iwapo tutatambua maudhui yanayoonyesha unyanyasaji wa watoto kingono. Ikiwa unaamini kuwa mtoto yupo hatarini, amenyanyaswa au ni mhasiriwa wa ulanguzi, wasiliana na wakala wako wa sheria katika eneo mahususi na shirika la usalama wa watoto lililoorodheshwa hapa.

Mbali na hayo, programu zinazowavutia watoto lakini zina maudhui ya watu wazima haziruhusiwi, ikiwa ni pamoja na, lakini si tu:

  • Programu zenye vurugu zilizokithiri, maudhui ya kutisha na ya umwagaji damu katika kiwango kikubwa.
  • Programu zinazoonyesha au kuhimiza shughuli hatarishi na za kudhuru.

Pia, haturuhusu programu zinazotangaza maudhui ya kujidunisha mwonekano au kujidharau ikiwa ni pamoja na programu zinazoonyesha utengenezaji wa viungo bandia, kupunguza uzito na marekebisho mengine ya urembo katika mwonekano wa mtu, kwa lengo la burudani.

Sera ya Viwango vya Usalama wa Watoto

Google Play inahitaji programu za Kijamii na za Kuchumbiana zitii sera yetu ya Viwango vya Usalama wa Watoto.

Ni lazima programu hizi:

  • Ziwe na Viwango Vilivyochapishwa: Lazima programu yako izuie kwa uwazi Kuwanyanyasa na Kuwadhulumu Watoto Kingono (CSAE) katika viwango vinavyoweza kufikiwa na umma, kama vile sheria na masharti, mwongozo wa jumuiya au hati yoyote ya sera ya watumiaji ya programu yako inayoweza kufikiwa na umma.
  • Ziweke Mbinu ya Ndani ya Programu ya Maoni ya Watumiaji: Ni lazima uthibitishe mwenyewe kuwa unatoa mbinu ndani ya programu yako ili watumiaji watume maoni, matatizo au ripoti katika programu yako.
  • Zishughulikie Maudhui Yanayoonyesha Unyanyasaji wa Watoto Kingono (CSAM): Lazima uthibitishe mwenyewe kuwa programu yako inachukua hatua inayofaa, ikiwa ni pamoja na, lakini si tu kuondoa maudhui yanayoonyesha unyanyasaji wa watoto kingono (CSAM), baada ya kupata ufahamu halisi wa kuwepo kwake, kwa mujibu wa viwango vyako ulivyochapisha na sheria zinazotumika.
  • Zitii Sheria za Usalama wa Watoto: Lazima uthibitishe mwenyewe kuwa programu yako inatii sheria na kanuni zinazotumika za usalama wa watoto, ikiwa ni pamoja na, lakini si tu, kuwa na mchakato ulioweka wa kuripoti maudhui yaliyothibitishwa kuwa yanaonyesha unyanyasaji wa watoto kingono (CSAM) kwenye Kituo cha Kitaifa cha Watoto Waliopotea na Wanaonyanyaswa au mamlaka husika ya eneo uliko.
  • Zitoe maelezo ya Mtu wa Kuwasiliana Naye kuhusu Usalama wa Watoto:Lazima programu yako itoe maelezo ya mtu aliyebainishwa wa kuwasiliana naye wa kupokea arifa zinazoweza kutoka Google Play kuhusu maudhui ya Kuwanyanyasa na Kuwadhulumu Watoto Kingono (CSAE) yanayopatikana kwenye programu au mfumo wako. Mwakilishi huyu lazima awe amejiandaa kuzungumzia taratibu za utekelezaji na ukaguzi pamoja na kuchukua hatua ikihitajika.

Pata maelezo zaidi hapa kuhusu masharti haya na jinsi ya kuyatii katika makala yetu ya Kituo cha Usaidizi.

Je, maelezo haya yamekufaa?

Tunawezaje kuboresha?

Je, unahitaji usaidizi mwingine?

Jaribu hatua zifuatazo:

Tafuta
Futa utafutaji
Funga kisanduku cha kutafutia
Menyu kuu
16327377526158783226
true
Tafuta kwenye Kituo cha Usaidizi
true
true
true
true
true
92637
false
false