Kujisajili kwenye mpango wa ofa za nje

 

Kuanzia tarehe 6 Machi, 2024, wasanidi programu kwa kutegemea iwapo wanatimiza masharti ya mpango yaliyo hapa chini pamoja na kifungu cha 9 cha Sera yetu ya malipo, wanaweza kujisajili kwenye mpango mpya wa ofa za nje iwapo wangependa kuwaelekeza watumiaji walio kwenye nchi washirika katika Makubaliano ya Kiuchumi ya Ulaya (EEA), nje ya programu, ikijumuisha kutangaza ofa za vipengele na huduma za kidijitali za ndani ya programu. Angalia maelezo hapa chini kisha utembelee mwongozo wetu wa ujumuishaji wa wasanidi programu ili uanze.

Mpango wa ofa za nje huwezesha wasanidi programu wa programu zinazosambazwa na Google Play kuwaelekeza watumiaji walio kwenye nchi washirika katika Makubaliano ya Kiuchumi ya Ulaya (EEA) nje ya programu, ikiwa ni pamoja na kutangaza ofa za huduma na vipengele vya ndani ya programu, kwa kutegemea Sera ya malipo ya Google Play. Ni lazima wasanidi programu watimize masharti yaliyo hapa chini na wakamilishe kujiandikisha kwenye mpango huu kabla ya kutangaza ofa za nje. Wasanidi programu wanaoshiriki wanasimamiwa na Sera yetu ya malipo na ada za huduma zinazotumika zinazoelezwa hapa chini, zinazowezesha uwekezaji wetu kwenye Google Play na Android, zitaendelea kutumika.

Masharti ya kujiunga

Ili utimize masharti ya kujiunga kwenye mpango huu:

  • Ni lazima msanidi programu ajisajili kama biashara.

Masharti

Wasanidi programu wanaoshiriki katika mpango huu ni lazima watii masharti yafuatayo: 

  • Waweke kikomo cha ofa za nje kwa watumiaji walio katika EEA.
  • Ofa za nje lazima ziwaelekeze tu watumiaji kwenye huduma au vipengele dijitali vinavyomilikiwa na msanidi programu.
  • Watoe URL zote za kusudio kupitia Dashibodi ya Google Play.
  • Wajiandikishe na programu zao ziidhinishwe kwenye mpango wa ofa za nje kama inavyoelezwa hapa chini.
  • Wajumuishe kwenye API za ofa za nje ili waelekeze watumiaji nje ya programu, ikiwa ni pamoja na kutekeleza API hizi ili Google iweze kuonyesha skrini inayofaa yenye maelezo na wasanidi programu waweze kuripoti miamala husika.
  • Watoe huduma kwa wateja na njia ya kurejeshewa pesa kwa watumiaji wanaofanya miamala ya nje kupitia ofa ya nje na kutoa mchakato wa kupinga miamala isiyoidhinishwa.
  • Ukurasa wa programu katika Google Play haupaswi kujumuisha maelezo yanayohusiana na ununuzi wa nje ya programu ili kupunguza uwezekano wowote wa kumchanganya mtumiaji.
  • Wanapowaelekeza watumiaji nje ya programu, ni sharti wasanidi programu:
    • Wamfahamishe mtumiaji kuhusu ukurasa lengwa na madhumuni yake na waweke aikoni hii papo hapo baada ya kiungo ili kuashiria kuwa mtumiaji ataelekezwa nje ya programu. Kwa mfano:

      Angalia ofa zaidi zilizo bora katika gems.exampleapp.com
       
    • Wawe na URL inayoonekana wazi kwenye ukurasa wao lengwa, hali inayomwezesha mtumiaji kuelewa mahali ameelekezwa.
    • Wasiruhusu vigezo vya ziada kwenye URL au kujaza data kiotomatiki kutoka kwenye programu, ili kumlinda mtumiaji.
    • Wasiwapotoshe wala kuwaelekeza kwingine watumiaji kwenye ukurasa lengwa ambao ni tofauti na ule uliopo kwenye ofa yao ya nje au kutoa maelezo mengine ya uongo au ya udanganyifu.
  • Walipe Google ada husika za miamala inayohusiana na programu ya Google Play inayofanywa nje ya programu kufuatia ofa ya nje. Sawa na ada zetu za kawaida za huduma, ada zinazohusishwa na mpango wa ofa za nje zinaonyesha thamani ambayo Android na Google Play hutoa na huwezesha uwekezaji wetu unaoendelea kwenye Android na Google Play. Ada hizi zinajumuisha sehemu mbili tofauti zinazohusiana na thamani ambayo Google Play hutoa: (a) ada yenye kikomo cha miaka miwili ya ununuzi wa kwanza wa mtumiaji na (b) ada ya huduma zinazoendelea (ikiwa ni pamoja na huduma za usalama na masasisho ya Google Play) ambayo Google Play huendelea kutoa kwa wasanidi programu. 
    • Ada zifuatazo zinatumika, kuanzia hatua ambapo mtumiaji anakamilisha muamala wa kwanza ndani ya saa 120 baada ya kufikia ofa ya nje (muamala wa kwanza wa nje):
      • Ada ya ununuzi wa kwanza: asilimia 5 kwa kusasisha usajili kiotomatiki na asilimia 10 kwa ofa nyingine za vipengele na huduma za kidijitali za ndani ya programu.
      • Ada ya huduma zinazoendelea: asilimia 7 kwa kusasisha usajili kiotomatiki na asimilia 17 kwa ofa nyingine za vipengele na huduma za kidijitali za ndani ya programu.
    • Ada zilizotajwa hapa juu zinatumika kwa muamala wa kwanza pamoja na maudhui yote ya kidijitali yatakayonunuliwa baadaye kwenye tovuti ya nje ili kutumiwa kwenye programu, bila kujali kipindi chochote cha wakati.
    • Baada ya kipindi cha ununuzi wa kwanza cha miaka miwili, msanidi programu anaweza kuchagua kufunga kabisa huduma zinazoendelea za Google Play za programu husika. Kwa kuwa watumiaji walipata programu kupitia Google Play wakiwa na matarajio ya kupata huduma kama vile vidhibiti vya wazazi, uchanganuzi wa usalama, uzuiaji wa ulaghai na masasisho yanayoendelea ya programu, mtumiaji pia atatakiwa kutoa idhini ili huduma zifungwe kabisa. Baada ya hatua hiyo, huduma zinazoendelea na ada zinazohusiana hazitatumika tena kwa watumiaji hawa. Wasanidi programu bado wana wajibu wa kuripoti miamala inayohusisha watumiaji watakaochagua kuendelea kupokea huduma zinazoendelea kutoka Google Play.

Kuandikisha programu yako kwenye mpango wa ofa za nje

Ili ujiandikishe kwenye mpango wa ofa za nje, ni lazima ukamilishe hatua zifuatazo:

  1. Kagua masharti yaliyo kwenye ukurasa huu ili ubaini iwapo programu zako zinatimiza masharti ya kujiunga.
  2. Jaza fomu ya taarifa ya ofa za nje, kubali Sheria na Masharti na ukamilishe hatua zozote za kufahamu mazingira ya matumizi zinazohitajika ili ujiandikishe kwenye mpango kupitia timu ya usaidizi ya Google.
  3. Jumuisha API za ofa za nje.
  4. Andikisha programu zako moja kwa moja kupitia Dashibodi ya Google Play. Ukishabainisha programu na nchi au maeneo ambapo utatoa ofa za nje, bofya sehemu iliyo hapa chini ili uipanue na ufuate hatua ili uandikishe programu yako na udhibiti mipangilio yako ya ofa za nje:
a. Kuandikisha programu yako
  1. Fungua Dashibodi ya Google Play kisha uende kwenye ukurasa wa Ofa za nje (Mipangilio > Kuunganisha kwenye ofa za nje).
  2. Tafuta programu ambayo ungependa kuandikisha kisha ubofye Dhibiti kwenye jedwali. Hatua hii itafungua ukurasa wa mipangilio ya Uchumaji wa Mapato wa programu husika.
  3. Bofya + Weka/Badilisha nchi au maeneo ili uchague nchi au maeneo ya EEA ambayo ungependa kutumia mpango wa ofa za nje katika programu hii.
    • Orodha ya nchi au maeneo yanayoweza kuchaguliwa hubainishwa na upatikanaji wa mpango katika nchi au maeneo hayo.
  4. Ukishamaliza kuchagua nchi au maeneo, bofya Hifadhi mabadiliko.
  5. Hatua hizi zinapaswa kukamilishwa katika kila programu ambayo ungependa kuandikisha kwenye mpango.
b. Kuangalia maelezo na kudhibiti mipangilio ya mpango

Unaweza kudhibiti mipangilio yako ya mpango wa ofa za nje, ikiwa ni pamoja na uandikishaji katika kiwango cha programu na maelezo ya wasifu, kwenye ukurasa wa Ofa za nje (Mipangilio > Kuunganisha kwenye ofa za nje).

c. Kuangalia maelezo ya kimaeneo ya ankara ya ofa za nje
  1. Fungua Dashibodi ya Google Play kisha uende kwenye ukurasa wa Ankara (Mipangilio > Ankara za malipo nje ya mfumo wa Malipo kupitia Google Play).
  2. Unaweza kuchagua kichupo cha eneo linalofaa la mtumiaji ili uangalie maelezo yanayolingana ya miamala na ada ya huduma inayohusishwa na miamala iliyofanywa na watumiaji katika eneo hilo kama vile kiasi unachodai, miamala, ankara na hati pamoja na mipangilio.
d. Kudhibiti mipangilio ya ofa za nje
  1. Fungua Dashibodi ya Google Play kisha uende kwenye ukurasa wa Ofa za nje (Mipangilio > Kuunganisha kwenye ofa za nje).
  2. Tafuta programu ambayo ungependa kuandikisha kisha ubofye Dhibiti kwenye jedwali. Hatua hii itafungua ukurasa wa mipangilio ya Uchumaji wa Mapato wa programu husika.
  3. Bofya + Badilisha nchi au maeneo ili uchague nchi au maeneo ambapo ungependa kusasisha ofa za nje.
    • Orodha ya nchi au maeneo yanayoweza kuchaguliwa hubainishwa na upatikanaji wa mpango katika nchi au maeneo hayo.
  4. Ukishamaliza kuchagua nchi au maeneo, bofya Hifadhi Mabadiliko.

5. Ripoti kwenye Google miamala yote husika iliyoidhinishwa ndani ya saa 24 ya muamala wa nje.

Ikiwa una maswali yoyote ya ziada, unaweza kuwasiliana na timu yetu ya usaidizi hapa.

 Fungua fomu ya taarifa

Maswali yanayoulizwa sana

Je, wasanidi programu wanaweza kutumia ofa za nje kwa watumiaji walio katika maeneo mengine ya kijiografia kando na EEA?

Hapana, mpango huu unapatikana tu kwa watumiaji walio katika EEA. Wasanidi programu kutoka maeneo mengine wanaweza kujiandikisha kwenye mpango huu ili kuwalenga watumiaji walio katika EEA nje ya Programu ya Google Play.

Je, ni nchi zipi ambazo ni washirika katika Makubaliano ya Kiuchumi ya Ulaya (EEA)?

Hivi sasa EEA inajumuisha: Austria, Ubelgiji, Bulgaria, Korasia, Jamhuri ya Kuprosi, Jamhuri ya Zechia, Denmaki, Estonia, Ufini, Ufaransa, Ujerumani, Ugiriki, Hungaria, Isilandi, Ayalandi, Italia, Latvia, Lishenteni, Litwania, Lasembagi, Malta, Uholanzi, Norwe, Polandi, Ureno, Romania, Slovakia, Slovenia, Uhispania na Uswidi.

Je, wasanidi programu za michezo wanatimiza masharti ya kujiunga kwenye mpango huu?

Ndiyo, wasanidi programu za michezo na programu za kawaida wanatimiza masharti ya kutuma maombi na kushiriki katika mpango wa ofa za nje.

Je, ninaweza kutoa mpango wa ofa za nje kwa aina zipi za bidhaa?

Mpango unapatikana kwenye programu na michezo katika maumbo yote ikiwa ni pamoja na vifaa vya mkononi, kishikwambi, Mfumo wa Uendeshaji wa Chrome, Android TV na Wear OS.

Je, wasanidi programu wote wanapaswa kujiandikisha kwenye mpango wa ofa za nje?

Hapana, huu ni mpango wa kujijumuisha tu. Iwapo hungependa kuwaelekeza watumiaji nje ya programu, huhitaji kuchukua hatua yoyote.

Je, ninaweza kufanya ofa za nje zipatikane kwa baadhi tu ya programu zangu?

Ndiyo, baada ya kujisajili kwenye mpango wa ofa za nje, unaweza kuchagua programu ambazo ungependa kuandikisha kwenye ofa za nje wakati wowote ukitumia Dashibodi ya Google Play.

Ninawezaje kuarifu Google kuhusu mabadiliko yoyote kwenye chaguo za kujiandikisha katika mpango wa malipo ya nje ya nchi husika?

Unaweza kubadilisha uandikishaji kwenye mpango wa malipo ya nje katika soko kwa kifurushi mahususi cha programu kupitia mipangilio yako ya Dashibodi ya Google Play. Masasisho yoyote yataanza kutumika papo hapo ikiwa ni pamoja na ada husika za huduma.

Je, hatua za kuunganisha kwenye API za ofa za nje ni zipi?

Ni rahisi kupanua ujumuishaji wako uliopo wa mfumo wa utozaji wa Google Play ili utumie API za ofa za nje. API hizi zimeundwa kwa kutumia kanuni na miundo ile ile ya usanifu, sawa na Maktaba yetu ya Malipo kupitia Google Play na API za Msanidi Programu wa Google Play. Hii inamaanisha kuwa API hizi zinaoana na usanifu uliopo na timu zako zitakuwa na ufahamu nazo. Kwenye mwongozo wetu wa ujumuishaji kwa wasanidi programu, tunatoa nyenzo na mwongozo wa kina kuhusu jinsi ya kuanza. Tungependa kupokea maoni ya wasanidi programu kuhusu API hizi na nyenzo zozote za ziada zinazoweza kusaidia.

Ikiwa una maswali au maoni yoyote kuhusu API za ofa za nje, tafadhali wasiliana nasi hapa.

Ikiwa tayari ninashiriki katika mpango wa mfumo mbadala wa utozaji, je, ninaweza pia kushiriki katika mpango wa ofa za nje?

Ndiyo, wasanidi programu wanaweza kushiriki katika mipango yote miwili ikiwa watachagua kufanya hivyo na ikiwa wanatimiza masharti ya kujiunga na mipango yote miwili. Ikiwa mipango yote miwili inapatikana kwenye programu, ada husika za huduma za muamala zitategemea ni wapi mtumiaji amechagua kufanyia muamala (ndani ya programu au nje ya programu). Ili ushiriki katika mpango wa ofa za nje na uanze kutangaza ofa za nje, unatakiwa ukamilishe mchakato wa kujisajili na utii masharti yote ya programu.

Je, ninaweza kutumia mfumo wa utozaji wa Google Play pamoja na ofa za nje?

Ndiyo, wasanidi programu wanaweza kutumia mfumo wa utozaji wa Google Play huku pia wakishiriki katika mpango wa ofa za nje. Ikiwa una mfumo wa Malipo kupitia Google Play na unatangaza ofa za nje, ada husika za huduma za muamala zinategemea ni wapi mtumiaji amechagua kufanyia muamala (ndani ya programu au nje ya programu). Ili ushiriki katika mpango wa ofa za nje na uanze kutangaza ofa za nje, unatakiwa ukamilishe mchakato wa kujisajili na utii masharti yote ya programu.

Kwa nini mpango wa ofa za nje unahitaji ada ya huduma?

Ada za Google Play huwezesha uwekezaji wetu kwenye Android na Google Play na huonyesha thamani inayotolewa na Android na Google Play, ikiwa ni pamoja na kutuwezesha kusambaza Android bila malipo na kutoa kifurushi kinachoendelea kukua cha zana na huduma zinazowasaidia wasanidi programu kukuza biashara zinazofanikiwa, huku tukidumisha usalama kwenye mifumo yetu kwa mabilioni ya watumiaji kote duniani. 

Ili kutiii kanuni za Sheria ya Masoko Dijitali (DMA), wasanidi programu wanaweza kujiandikisha kwenye mpango wa ofa za nje. Ili tuendeleze uwekezaji wetu katika mfumo huu, wasanidi programu wanaoshiriki katika mpango wa ofa za nje watakatwa ada mpya za huduma za ununuzi wa watumiaji unaohusishwa na programu ya Google Play unaofanywa nje ya programu, ikiwa ni pamoja na ada za ununuzi wa kwanza na ada za huduma zinazoendelea.

Je, Google Play iliamua vipi mfumo mpya wa ada za mpango wa ofa za nje?

Mfumo mpya wa ada za huduma za mpango wa ofa za nje una sehemu mbili : 

Ada ya ununuzi wa kwanza itawekewa kikomo ili kuonyesha kuwa Google Play inatoza tu kwa thamani iliyotoa katika kuwezesha ununuzi wa kwanza wa mtumiaji kupitia Google Play. Kipindi cha ‘ununuzi wa kwanza’ upande mwingine, kitazingatia jinsi ambavyo wasanidi programu kwa kawaida huchuma mapato kutokana na programu. Wasanidi programu wengi hufanya hivyo kupitia miamala midogo inayoongezeka inayofanywa kwa vipindi virefu. Kwa miamala yoyote iliyo nje ya muda wa miaka miwili ya ununuzi wa kwanza wa mtumiaji mahususi, wasanidi programu hawatatozwa ada ya ununuzi wa kwanza. 

Ada ya huduma zinazoendelea itatozwa ilimradi msanidi programu anaendelea kutumia huduma zinazoendelea za Google Play (ikiwa ni pamoja na huduma za usalama na masasisho ya Google Play). Msanidi programu anaweza kuchagua kujiondoa kwenye huduma zinazoendelea za Google Play katika programu fulani, baada ya kipindi cha ununuzi wa kwanza cha miaka miwili kuisha. Kwa kuwa watumiaji walipata programu kupitia Google Play wakitarajia kupata huduma kama vile vidhibiti vya wazazi, uchanganuzi wa usalama, kuzuia ulaghai na masasisho yanayoendelea ya programu, kufunga kabisa huduma kunahitaji idhini ya mtumiaji. Kwa hivyo, msanidi programu anapoamua kujiondoa, watumiaji wanaotimiza masharti ya kutumia programu hii lazima wachukue hatua ili kukubali kujiondoa kwa msanidi programu huyo. Ada za huduma zinazoendelea na zinazohusiana hazitatumika kwa watumiaji hao. Bado utahitaji kuripoti miamala ya watumiaji wanaochagua kuendelea kupokea huduma zinazoendelea kutoka Google Play.

Je, ada tofauti za huduma hutozwa vipi ikiwa ninatoa mfumo wa utozaji wa Google Play na kushiriki pia katika mpango wa ofa za nje?
Ufuatao ni mfano unaonyesha jinsi ada tofauti za huduma zinatumika katika hali hii. Mtumiaji A anatumia Programu ya Fantastiq inayochuma mapato kwa kutumia mfumo wa utozaji wa Google Play ndani ya programu na anashiriki katika mpango wa ofa za nje. Ifuatayo ni sampuli ya ununuzi kutoka kwa mtumiaji huyo na ada zinazotumika za huduma kwa msanidi programu:
 
Mtumiaji anapokamilisha muamala akitumia Programu ya Fantastiq Aina ya ada ya muundo Muda wa ununuzi Aina ya bidhaa aliyonunua Ada
Ndani ya programu Mfumo wa utozaji wa Google Play Haitumiki Usajili wa Kila Mwezi wa Michezo Bomba Asilimia 15
Nje ya programu Ofa za nje Ndani ya miaka miwili baada ya muamala wa kwanza wa nje Usajili wa Kila Mwaka wa Kutiririsha Zaidi

Ada ya ununuzi wa kwanza: asilimia 5
+
Ada ya huduma zinazoendelea: asilimia 7 (unaweza kujiondoa kwayo baada ya mwaka wa pili)

 

Nje ya programu Ofa za nje Miaka miwili baada ya muamala wa kwanza wa nje 100 Extra Hearts

Ada ya huduma zinazoendelea: Asilimia 17 (ikiwa mtumiaji ataendelea kutumia huduma za Google Play)

Nje ya programu Ofa za nje Miaka miwili baada ya muamala wa kwanza wa nje Usajili wa Kila Mwezi wa Premium

Ada ya huduma zinazoendelea: Asilimia 7 (ikiwa mtumiaji ataendelea kutumia huduma za Google Play)

 

Je, maelezo haya yamekufaa?

Tunawezaje kuboresha?

Je, unahitaji usaidizi mwingine?

Jaribu hatua zifuatazo:

true
Tafuta
Futa utafutaji
Funga kisanduku cha kutafutia
Menyu kuu
2698596606195851443
true
Tafuta kwenye Kituo cha Usaidizi
true
true
true
true
true
92637
false
false