Toleo Tangulizi la sera
Ili kuwapa watumiaji hali bora ya utumiaji, tunaanzisha vikomo vipya kwa utumiaji wa ruhusa ya USE_FULL_SCREEN_INTENT. Kwa programu zinazolenga toleo la Android U (kiwango cha API cha 34) na zaidi, tunabadilisha ruhusa hii kuwa ruhusa maalum ya ufikiaji wa programu. Ni programu ambazo utendaji wao wa msingi unahitaji arifa ya skrini nzima tu ndizo zitapewa ruhusa hii kwa chaguomsingi. Programu zingine zote zitahitaji kuomba ruhusa kutoka kwa mtumiaji. (kuanza kutumika tarehe 31 Mei, 2024)
Kwa hali ya utumiaji inayodumisha faragha ya watumiaji, tunawaletea sera ya Ruhusa za Picha na Video ili kupunguza idadi ya programu zinazoruhusiwa kuomba ruhusa pana za picha/video (READ_MEDIA_IMAGES na READ_MEDIA_VIDEO). Programu zinaweza tu kufikia picha na video kwa madhumuni yanayohusiana moja kwa moja na utendaji wa programu. Programu ambazo zinahitaji kufikia faili hizi mara moja tu au mara chache zinaombwa kutumia kiteuzi cha mfumo, kama vile kiteua picha cha Android. (kuanzia Tarehe 31 Agosti, 2024)
Tunasasisha Sera ya Health Connect ili kurahisisha mchakato wa kutuma maombi wa Health Connect pamoja na kutii sera ya Programu za Afya. Baadye mwaka huu, taarifa mpya ya Dashibodi ya Google Play itatumika badala ya mchakato uliopo wa kutumia fomu. (kuanzia Tarehe 31 Agosti, 2024)
Ili uone makala ya sasa ya “Ruhusa na API Zinazofikia Taarifa Nyeti”, tembelea ukurasa huu.
Maombi ya ruhusa na API zinazofikia maelezo nyeti lazima ziwe bayana kwa mtumiaji. Unapaswa tu kuomba ruhusa na API zinazofikia maelezo nyeti zinazohitajika kutekeleza vipengele au huduma za sasa katika programu yako ambazo umezitangaza kwenye ukurasa wa programu yako katika Google Play. Hupaswi kutumia ruhusa au API zinazofikia maelezo nyeti ambazo zinakupa ufikiaji wa data ya vifaa au ya watumiaji kwa madhumuni yasiyofichuliwa, yasiyotekelezwa au yasiyoruhusiwa au kwenye vipengee ambavyo haviruhusiwi. Huruhusiwi kuuza wala kushiriki data binafsi au nyeti inayofikiwa kupitia ruhusa au API zinazoweza kufikia maelezo nyeti.
Omba ruhusa au API zinazofikia maelezo nyeti ili ufikie data husika (kupitia maombi endelevu), ili watumiaji waweze kuelewa kwa nini programu yako inaomba ruhusa. Tumia data kwa madhumuni ambayo mtumiaji ameidhinisha pekee. Kama ungependa kutumia data kwa madhumuni mengine baadaye, lazima uwaombe watumiaji idhini na uhakikishe wanakubali kabisa matumizi ya ziada.
Ruhusa Zinazodhibitiwa
Mbali na maelezo yaliyo hapo juu, ruhusa zinazodhibitiwa ni ruhusa ambazo zimebainishwa kuwa Hatari, Maalum, Saini au jinsi inavyobainishwa hapa chini. Ruhusa hizi zinategemea vidhibiti na masharti ya ziada yafuatayo:
- Data ya kifaa au ya mtumiaji inayofikiwa kupitia Ruhusa Zilizodhibitiwa inachukuliwa kuwa data nyeti na binafsi. Masharti ya Sera ya Data ya Mtumiaji yatatumika.
- Heshimu uamuzi wa watumiaji iwapo watakataa ombi la kutoa Ruhusa Inayodhibitiwa na watumiaji hawapaswi kulazimishwa au kulaghaiwa ili watoe idhini ya ruhusa zozote zisizo muhimu. Ni lazima ujitahidi kuwakubali watumiaji ambao hawatoi uwezo wa kufikia ruhusa nyeti (kwa mfano, kumruhusu mtumiaji aweke mwenyewe nambari ya simu iwapo hajaruhusu ufikiaji wa Rekodi ya Nambari za Simu).
- Haturuhusu kabisa matumizi ya ruhusa kwa njia inayokiuka sera za programu hasidi za Google Play (ikiwa ni pamoja na Matumizi Mabaya ya Ufikiaji Maalum).
Ruhusa fulani Zinazodhibitiwa zinaweza kutegemea masharti ya ziada jinsi inavyoelezewa kwa kina hapa chini. Lengo la masharti haya ni kulinda faragha ya mtumiaji. Tunaweza kuruhusu hali kadhaa zisizofuata masharti yaliyo hapa chini katika matukio ambayo hutokea kwa nadra, ambapo programu zinatoa kipengele cha lazima au muhimu zaidi na katika hali ambapo hakuna njia mbadala ya kutoa kipengele hicho. Tunatathmini hali pendekezwa zisizofuata kanuni kwa kuzingatia uwezekano wa kuathiri faragha au usalama wa watumiaji.
Ruhusa za SMS na Rekodi ya Nambari za SimuRuhusa za SMS na Rekodi ya Nambari za Simu huchukuliwa kuwa data ya mtumiaji ambayo ni nyeti na ya binafsi kwa mujibu wa sera ya Taarifa Binafsi na Nyeti na masharti yafuatayo:
Programu zisizo na uwezo wa kidhibiti chaguomsingi cha SMS, Simu au Programu ya Mratibu hazipaswi kutangaza matumizi ya ruhusa zilizo hapo juu kwenye faili ya maelezo. Uwezo huu unajumuisha maandishi ya kishikilia nafasi kwenye faili ya maelezo. Vile vile, ni lazima programu ziwe zimesajiliwa kuwa kidhibiti chaguomsingi cha programu ya Mratibu, SMS au Simu kabla ya kudokezea watumiaji wakubali mojawapo ya ruhusa zozote zilizo hapo juu na sharti ziache mara moja kutumia ruhusa zikiacha kuwa kidhibiti chaguomsingi. Matumizi na hali zisizofuata kanuni zinazoruhusiwa zinapatikana kwenye ukurasa huu wa Kituo cha Usaidizi. Programu zinaweza kutumia tu ruhusa (na data yoyote inayotokana na ruhusa) ili kutoa utendaji wa msingi wa programu ulioidhinishwa. Utendaji wa msingi unafafanuliwa kuwa lengo kuu la programu. Hili linaweza kujumuisha vipengele vya msingi, ambavyo vinapaswa kurekodiwa kwa njia dhahiri katika maelezo ya programu. Bila vipengele vya msingi, programu “haijakamilika” au inachukuliwa kuwa haiwezi kutumika. Uhamishaji, kushiriki au matumizi yaliyoidhinishwa ya data hii ni sharti yatoe tu huduma au vipengele vya msingi katika programu na matumizi yake hayapaswi kuenezwa kwa madhumuni mengine yoyote (k.m. madhumuni ya utangazaji au uuzaji, kuboresha programu au huduma nyingine). Hupaswi kutumia njia mbadala (ikiwa ni pamoja na ruhusa, API au vyanzo vya wengine) ili kupata data inayohusishwa na ruhusa za SMS au Rekodi ya Nambari za Simu. |
Ruhusa za MahaliData ya mahali kifaa kilipo huchukuliwa kuwa data ya mtumiaji ambayo ni nyeti na ya binafsi kwa mujibu wa sera ya Taarifa Binafsi na Nyeti na Sera ya Ruhusa ya Kubainisha Mahali Chinichini na masharti yafuatayo:
Programu zinaruhusiwa kufikia data ya mahali kwa kutumia ruhusa ya huduma ya ufikiaji wakati programu inatumika (programu ina uwezo wa ufikiaji wakati inatumika tu, k.m., "inapotumika") ikiwa matumizi haya:
Ni lazima programu zilizobuniwa kwa ajili ya watoto zitii sera ya Programu za Familia Yote. Ili upate maelezo zaidi kuhusu masharti ya sera, tafadhali angalia makala haya ya usaidizi. |
Ruhusa ya Kufikia Faili ZoteSifa za faili na saraka kwenye kifaa cha mtumiaji huchukuliwa kuwa data ya mtumiaji ambayo ni nyeti na ya binafsi kwa mujibu wa sera ya Taarifa Binafsi na Nyeti na masharti yafuatayo:
|
Ruhusa za Picha na VideoPicha na video zilizo kwenye kifaa cha mtumiaji huchukuliwa kuwa data ya mtumiaji ambayo ni nyeti na ya binafsi kwa mujibu wa Sera ya Data ya Mtumiaji kwenye Google Play. Programu zinaweza tu kufikia picha na video kwa madhumuni yanayohusiana moja kwa moja na utendaji wa programu na hazipaswi kuomba ufikiaji kwa niaba ya programu yoyote ya wengine kwa madhumuni yoyote yasiyohusiana na utendaji wa programu unaowalenga watumiaji. Ili ufurahie hali ya utumiaji inayodumisha faragha, tunakuhimiza utumie kiteuzi cha mfumo kama vile kiteua picha. Lazima programu zinazotaka uwezo mpana wa kufikia faili za picha na video zinazopatikana katika hifadhi inayoshirikiwa kwenye vifaa zipite ukaguzi wa ufikiaji unaofaa na zionyeshe hali ya utumiaji wa msingi inayohitaji ufikiaji endelevu au wa mara kwa mara wa faili za picha au video zilizo katika hifadhi inayoshirikiwa. Programu ambazo zinahitaji kufikia faili hizi mara moja tu au mara chache zinaombwa kutumia kiteuzi cha mfumo, kama vile kiteua picha cha Android. Uwezo mpana wa kufikia picha na video unategemea pia masharti yafuatayo:
Iwapo programu yako haihitaji au haitimizi masharti ya uwezo mpana wa kufikia ruhusa za READ_MEDIA_VIDEO au READ_MEDIA_IMAGES, ni lazima uiondoe kwenye faili ya maelezo ya programu yako ili utimize masharti ya upitiaji wa sera. Kwa mujibu wa sera ya Ruhusa Zinazodhibitiwa, ni lazima ujitahidi uwezavyo kuwashughulikia watumiaji ambao hawatoi uwezo mpana wa kufikia faili za maudhui zilizo kwenye vifaa vyao. Hii inajumuisha kuweka hali ya utumiaji wa programu inayowaruhusu watumiaji wafurahie kipengele au utendaji wa msingi wa programu yako. Programu zilizo na uwezo halali wa kufikia picha au video, lakini hazijatimiza masharti ya kutumia ruhusa za READ_MEDIA_IMAGES au READ_MEDIA_VIDEO zinaweza kutumia kiteuzi cha mfumo kama vile kiteua picha. Kwa maelezo zaidi, tafadhali angalia makala haya ya Kituo cha Usaidizi. |
Ruhusa ya Uonekanaji wa Kifurushi (Programu)Orodha ya programu zilizosakinishwa iliyotumwa kutoka kwenye kifaa huchukuliwa kuwa data ya mtumiaji ambayo ni nyeti na ya binafsi kwa mujibu wa sera ya Maelezo Nyeti na ya Kibinafsi na masharti yafuatayo: Programu ambazo zina lengo kuu la kufungua, kutafuta au kufanya kazi na programu zingine kwenye kifaa, zinaweza kupata ruhusa inayofaa upeo wa uonekanaji kwenye programu zingine zilizosakinishwa kwenye kifaa jinsi inavyobainishwa hapa chini:
Hupaswi kuuza au kushiriki data ya orodha ya programu iliyotumwa kutoka kwenye programu zinazosambazwa na Google Play kwa ajili ya takwimu au madhumuni ya uchumaji wa mapato ya matangazo. |
API ya UfikivuAPI ya Ufikivu haitumiki:
API ya Ufikivu haijabuniwa na haiwezi kuombwa kwa ajili ya kurekodi simu ya sauti kutoka mbali. Ni lazima utumiaji wa API ya Ufikivu urekodiwe kwenye ukurasa wa programu katika Google Play. Mwongozo wa IsAccessibilityToolProgramu ambazo utendaji wa msingi unanuia kuwasaidia walemavu kwa njia ya moja kwa moja zinatimiza masharti ya kutumia IsAccessibilityTool ili ziweze kujibainisha hadharani inavyofaa kuwa programu za ufikivu. Programu zisizotimiza masharti ya IsAccessibilityTool hazipaswi kutumia kitia alama na lazima zitimize masharti muhimu ya ufumbuzi na idhini kama inavyobainishwa katika Sera ya Data ya Mtumiaji kwa vile utendaji unaohusiana na ufikivu si bayana kwa mtumiaji. Tafadhali rejelea makala ya kituo cha usaidizi ya API ya Huduma ya Ufikivu ili upate maelezo zaidi. Ni lazima programu zitumie API na ruhusa zinazohusisha vipengele vichache zaidi badala ya API ya Ufikivu inapowezekana ili kufikia utendaji unaohitajika. |
Omba Ruhusa ya Kusakinisha VifurushiRuhusa hii ya REQUEST_INSTALL_PACKAGES inaruhusu programu kuomba usakinishaji wa vifurushi vya programu. Ili utumie ruhusa hii, utendaji wa msingi wa programu yako lazima ujumuishe:
Utendaji unaoruhusiwa unajumuisha:
Utendaji wa msingi unafafanuliwa kuwa ni lengo kuu la programu. Utendaji wa msingi, pamoja na vipengele vyovyote vya msingi vinavyojumuisha utendaji huu wa msingi lazima vitangazwe na kuonyeshwa kwa njia dhahiri kwenye maelezo ya programu. Huruhusiwi kutumia REQUEST_INSTALL_PACKAGES kufanya masasisho binafsi, marekebisho au kuunganisha APK nyingine kwenye faili ya kipengee isipokuwa kwa madhumuni ya usimamizi wa kifaa. Masasisho yote au usakinishaji wa vifurushi ni lazima zitii sera ya Google Play Dhidi ya Matumizi Mabaya ya Vifaa na Mtandao na lazima zianzishwe na ziendeshwe na mtumiaji. |
Ruhusa za Health Connect kutoka AndroidHealth Connect ni mfumo wa Android unaoruhusu programu za afya na siha kuhifadhi na kutuma data sawa ya kifaa, ndani ya mfumo uliosawazishwa. Inatoa pia sehemu moja kwa watumiaji kudhibiti programu zinazoweza kusoma na kuandika data ya afya na siha. Health Connect inasaidia kusoma na kuandika aina mbalimbali za data, kuanzia hatua hadi joto la mwili. Data inayofikiwa kupitia Ruhusa za Health Connect huchukuliwa kuwa data binafsi au nyeti ya mtumiaji kwa mujibu wa sera ya Data ya Mtumiaji. Ikiwa programu yako inastahiki kuwa programu ya afya au ina vipengele vinavyohusiana na afya na inafikia data ya afya ikiwa ni pamoja na data ya Health Connect, ni lazima itii pia sera ya programu za Afya. Tafadhali angalia mwongozo huu wa wasanidi programu wa Android kuhusu jinsi ya kuanza kutumia Health Connect. Ili uombe idhini ya kufikia aina ya data za Health Connect, tafadhali angalia hapa. Ni lazima programu zinazosambazwa kupitia Google Play zitimize masharti yafuatayo ya sera ili zisome na/au kuandika data kwenye Health Connect. Ufikiaji na Matumizi Sahihi ya Health ConnectHealth Connect inapaswa tu kutumika kwa mujibu wa sera, sheria na masharti yanayotumika pamoja na hali zilizoidhinishwa, kama ilivyobainishwa katika sera hii. Hatua hii inamaanisha kwamba unapaswa tu kuomba idhini ya kufikia ruhusa wakati programu au huduma yako itatimiza moja kati ya hali za matumizi zilizoidhinishwa. Hali za matumizi zilizoidhinishwa ni pamoja na: siha na ustawi, zawadi, mafunzo ya siha, ustawi wa mashirika, matibabu, utafiti wa afya na michezo. Programu zilizopewa idhini ya kufikia ruhusa hizi hazipaswi kuendeleza matumizi yake kwa madhumuni yasiyofichuliwa au yasiyoruhusiwa. Programu au huduma zenye kipengele kimoja au zaidi zilizoundwa kwa madhumuni ya msingi ya kunufaisha afya na siha ya mtumiaji zinaruhusiwa kuomba idhini ya kufikia Ruhusa za Health Connect. Maelezo haya ni pamoja na:
Uwezo wa kufikia Health Connect haupaswi kutumika kinyume cha sera hii au sera pamoja na sheria na masharti mengine ya Health Connect yanayotumika, ikiwa ni pamoja na madhumuni yafuatayo:
Pia, ni jukumu lako kuhakikisha kwamba unatii mahitaji yoyote ya mamlaka za usimamizi au sheria ambazo huenda zikatumika kulingana na matumizi uliyokusudia ya Health Connect pamoja na data yoyote kutoka Health Connect. Isipokuwa kama ilivyobainishwa dhahiri katika lebo au taarifa zilizotolewa na Google kwa bidhaa na huduma mahususi za Google, Google haiidhinishi matumizi ya au kuthibitisha usahihi wa data yoyote iliyo katika Health Connect kwa matumizi na madhumuni yoyote, hasa, kwa matumizi ya utafiti, afya au tiba. Google inakanusha dhima zote zinazohusiana na matumizi ya data inayopatikana kupitia Health Connect. Matumizi yaliyowekewa VizuiziWakati wa kutumia Health Connect, ni lazima ufikiaji na utumiaji wa data utii vikomo mahususi:
Upeo wa kiwango cha chiniNi lazima tu uombe idhini ya kufikia ruhusa ambazo ni muhimu ili kutekeleza vipengele au huduma za bidhaa yako. Maombi kama hayo ya ufikiaji yanapaswa kuwa mahususi na yahusiane tu na data inayohitajika. Ilani Wazi na Sahihi pamoja na UdhibitiHealth Connect hudhibiti data ya afya na siha, ikijumuisha taarifa nyeti na inahitaji programu zote ziwe na sera ya kina ya faragha. Sera ya faragha lazima ifumbue kwa uwazi jinsi programu inavyokusanya, kutumia na inavyoruhusu kufikiwa kwa data ya mtumiaji. Zaidi ya mahitaji ya kisheria, wasanidi programu lazima wawe na taarifa zifuatazo katika sera ya faragha:
Kwa maelezo zaidi kuhusu masharti ya programu zinazounganisha kwenye Health Connect, tafadhali angalia makala haya ya Kituo cha Usaidizi. |
Huduma ya VPNVpnService ni daraja la msingi kwa ajili ya programu kuendeleza na kutengeneza huduma yazo zenyewe za VPN. Programu zinazotumia VpnService tu, ambazo pia zina utendaji wa msingi wa VPN ndizo zinaweza kuunda njia salama ya upitishaji wa data kwenye seva ya mbali katika kifaa chenyewe. Hali zisizofuata kanuni hujumuisha programu zinazohitaji seva ya mbali kwa ajili ya utendaji wa msingi kama vile:
VpnService haiwezi kutumika:
Programu zinazotumia VpnService zinapaswa:
|
Ruhusa ya Kengele SahihiRuhusa mpya itakayoongezwa ya USE_EXACT_ALARM, itazinduliwa ambayo itatoa uwezo wa kufikia utendaji sahihi wa kengele katika programu kuanzia Android 13 (kiwango lengwa cha API 33). USE_EXACT_ALARM ni ruhusa inayodhibitiwa na programu zinapaswa tu kubainisha ruhusa hii ikiwa utendaji wake wa msingi unaonyesha hitaji la kufikia utendaji sahihi wa kengele. Programu zitakazoomba ruhusa hii inayodhibitiwa, zitakaguliwa na zile ambazo hazitatimiza kigezo cha hali ya matumizi yanayokubalika hazitaruhusiwa kuchapisha kwenye Google Play. Hali za matumizi zinazokubalika kutumia Ruhusa ya Kengele Sahihi Programu yako inapaswa tu kutumia utendaji wa USE_EXACT_ALARM wakati utendaji msingi wa programu yako kwa mtumiaji unahitaji vitendo vinavyolingana kwa usahihi na saa, kama vile:
Ukiwa una hali ya matumizi kwa ajili ya utendaji sahihi wa kengele ambayo haipo hapa juu, unapaswa kutathmini iwapo unaweza kutumia SCHEDULE_EXACT_ALARM kama chaguo mbadala. Ili upate maelezo zaidi kuhusu utendaji sahihi wa kengele, tafadhali angalia mwongozo huu wa msanidi programu. |
Ruhusa ya Utaratibu wa Kuratibu Skrini NzimaKwa programu zinazolenga toleo la Android 14 (kiwango lengwa cha API 34) na zaidi, USE_FULL_SCREEN_INTENT ni ruhusa ya ufikiaji wa programu maalum. Programu zitaruhusiwa tu kiotomatiki kutumia ruhusa ya USE_FULL_SCREEN_INTENT ikiwa utendaji wa msingi wa programu unapatikana chini ya moja ya aina zilizo hapa chini zinazohitaji arifa za kipaumbele cha juu:
Programu zinazoomba ruhusa hii zitakaguliwa na zile ambazo hazitimizi kigezo cha hapo juu hazitapewa ruhusa hii kiotomatiki. Kwa hivyo, lazima programu ziombe ruhusa kutoka kwa mtumiaji ili kutumia USE_FULL_SCREEN_INTENT. Kama kikumbusho, matumizi yoyote ya ruhusa ya USE_FULL_SCREEN_INTENT lazima yatii Sera zote za Google Play za Wasanidi Programu, ikiwa ni pamoja na sera za Programu za Simu Zisizotakikana, Matumizi Mabaya ya Kifaa na Mtandao na Matangazo. Arifa za utaratibu wa kuratibu skrini nzima hazipaswi kuathiri, kukatiza, kuharibu au kufikia kifaa cha mtumiaji kwa njia ambayo haijaidhinishwa. Pia, programu hazipaswi kuathiri programu nyingine au urahisi wa kutumia kifaa. Pata maelezo zaidi kuhusu ruhusa ya USE_FULL_SCREEN_INTENT katika Kituo chetu cha Usaidizi. |