Kutumia huduma za uadilifu na kuambatisha vyeti ili kulinda programu na watumiaji wako

Huduma za Google Play za uadilifu na kuambatisha vyeti hukusaidia kuhakikisha kuwa watumiaji wanatumia programu na michezo yako jinsi unavyokusudia. Unaweza kutumia ukurasa wa Uadilifu wa programu (Toleo > Uadilifu wa programu) katika Dashibodi ya Google Play ili:

  • Kuunganisha mradi wako wa Wingu la Google ili utumie Play Integrity API kulinda programu na michezo yako dhidi ya matumizi hatari
  • Kuweka mipangilio ya ulinzi otomatiki wa uadilifu ili kuzuia urekebishaji na usambazaji usioidhinishwa.
  • Kuweka mipangilio ya kuambatisha cheti kwenye programu katika Google Play ili kuruhusu Google Play idhibiti ufunguo wako wa kuambatisha cheti kwenye toleo la kila programu
  • Kuwasha ukaguzi wa uadilifu kwa ajili ya uonekanaji wa ukurasa wa programu yako katika Google Play ili vifaa visivyojulikana na visivyoaminika ambavyo havijatimiza ukaguzi wa uadilifu visiweze kupakua programu yako kutoka kwenye Google Play.

Unaweza pia kukagua hali ya kila mojawapo ya huduma hizi kwa haraka.

Muhtasari

Unaweza kutumia ukurasa wa Uadilifu wa programu (Toleo > Uadilifu wa programu) kudhibiti na kufuatilia huduma zote za uadilifu na kuambatisha vyeti katika Google Play. Kila huduma ina maelezo na nyenzo za kukusaidia kuanza. Baada ya kuwasha huduma, unaweza kuiwekea mipangilio na kufikia vipengele vingine kwenye menyu ya mipangilio yake. Utaanza pia kuona ripoti ya huduma hiyo, kama ipo.

Bofya sehemu iliyo hapa chini ili uipanue au uikunje.

Play Integrity API

Tekeleza Integrity API katika matukio muhimu kwenye programu yako ili uhakikishe kwamba ni mfumo wa jozi wa programu yako, uliosakinishwa na Google Play unaotumika kwenye kifaa halali cha Android. Seva inayoshughulikia sehemu ya nyuma ya mfumo wa programu yako inaweza kuamua hatua ya kuchukuliwa ili kuepuka matumizi mabaya, ufikiaji usiodhinishwa na mashambulizi. Baada ya kujumuisha Integrity API, unaweza kufuatilia maombi ya API ya programu yako na kuchanganua uamuzi kupitia ripoti zinazotolewa na usakinishaji wako.

Anza kutumia nyenzo zifuatazo:

Ulinzi otomatiki wa uadilifu

Tumia kipengele cha ulinzi otomatiki wa uadilifu cha Google Play ili kulinda programu na michezo yako dhidi ya matumizi mabaya ya uadilifu kwa njia ya ubadilishaji na usambazaji ambao haujaidhinishwa. Kipengele cha ulinzi otomatiki wa uadilifu hufanya kazi kwenye programu yako bila muunganisho wa data. Unaweza kukiwasha kwa kubofya mara moja katika Dashibodi ya Google Play na hakihitaji msanidi programu akiweke kabla ya majaribio na hakihitaji ujumuishaji wa seva inayoshughulikia sehemu ya nyuma ya mfumo wa programu.

Pata maelezo zaidi kuhusu kipengele cha ulinzi otomatiki wa uadilifu.

Mpango wa Google Play wa Kuambatisha Cheti kwenye Programu

Tumia Huduma ya Google Play ya Kuambatisha Cheti kwenye Programu ili kuruhusu Google Play idhibiti na kulinda ufunguo wako wa kuambatisha cheti kwenye programu na uitumie kuambatisha cheti kwenye kila toleo. Hatua hii huhakikisha kuwa masasisho yoyote yanatoka kwako.

Pata maelezo zaidi kuhusu jinsi ya kutumia mpango wa Google Play wa Kuambatisha Cheti kwenye Programu.

Uonekanaji wa ukurasa wa programu katika Google Play
Kumbuka:Ukaguzi wa uadilifu wa uonekanaji wa ukurasa wa programu katika Google Play hapo awali ulikuwa amri ya kutojumuisha kifaa kwenye Play Integrity katika Orodha ya vifaa (Ufikiaji na vifaa > Orodha ya vifaa). Tulibadilisha jina la kipengele na kukihamishia kwenye ukurasa wa Uadilifu wa programu ili iwe rahisi kukipata na kukitumia. 

Washa ukaguzi wa uadilifu wa ukurasa wa programu katika Google Play ili Google Play iweze kukagua kama vifaa vimepita ukaguzi wa uadilifu kabla ya kufanya ukurasa wa programu yako katika Google Play uonekane kwa watumiaji. 

Vidokezo:

  • Huduma hii haikuhitaji kujumuisha Play Integrity API katika programu yako. Programu ya Duka la Google Play hupata uamuzi wa kifaa kwenye kifaa chenyewe na kuutumia kubainisha uonekanaji wa ukurasa wa programu katika Google Play.
  • Kwa kuwasha ukaguzi wa uadilifu, unaweza kupunguza matukio ya upatikanaji wa programu yako kwenye vifaa hatari kama vile vifaa vyenye idhini maalum ya kudhibiti au vilivyoathiriwa, vinavyoiga na vinavyotumia mazingira yasiyojulikana. 
  • Unaweza kupata ufafanuzi wa kila ukaguzi wa uadilifu kwenye hati ya Play Integrity API
  • Hali hii haiwazuii watumiaji wasipate programu yako kwa njia nyingine kama vile kupitia mfumo mwingine wa usambazaji au kupitia upakiaji kutoka kifaa kingine, kwa hivyo unaweza kutumia ulinzi wa muda pia kama vile Play Integrity API au ulinzi otomatiki wa uadilifu. 

Ili utumie ukaguzi wa uadilifu:

  1. Fungua Dashibodi ya Google Play kisha uende kwenye ukurasa waUadilifu wa programu (Toleo > Uadilifu wa programu)
  2. Nenda kwenye sehemu ya "Uonekanaji wa ukurasa wa programu katika Google Play".
  3. Chagua kama ungependa kuwasha ukaguzi wa uadilifu wa ukurasa wa programu yako katika Google Play. Vifaa visivyojulikana na visivyoaminika visivyotimiza masharti ya ukaguzi wa uadilifu havitaweza kusakinisha programu yako kutoka kwenye Google Play:
    • Hakuna ukaguzi wa uadilifu: Ukurasa wa programu yako katika Google Play utaonekana kwa vifaa vyote unavyotumia.
    • Ukaguzi wa msingi wa uadilifu: Ukurasa wa programu yako katika Google Play utaonekana kwa vifaa vyote unavyotumia, vinavyotimiza masharti ya ukaguzi wa msingi wa uadilifu.
    • Ukaguzi wa uadilifu wa kifaa: Ukurasa wa programu yako katika Google Play utaonekana kwenye vifaa vyote unavyotumia, vinavyotimiza masharti ya ukaguzi wa uadilifu wa kifaa.
    • Ukaguzi thabiti wa uadilifu: Ukurasa wa programu yako katika Google Play utaonekana kwenye vifaa vyote unavyotumia, vinavyotimiza masharti ya ukaguzi thabiti wa uadilifu.
  4. Hifadhi mabadiliko uliyofanya.

Je, maelezo haya yamekufaa?

Tunawezaje kuboresha?

Je, unahitaji usaidizi mwingine?

Jaribu hatua zifuatazo:

Tafuta
Futa utafutaji
Funga kisanduku cha kutafutia
Menyu kuu
5098538157626684765
true
Tafuta kwenye Kituo cha Usaidizi
true
true
true
true
true
92637
false
false