Unda na usambaze sura ya saa kwenye Google Play

Ukurasa huu unaeleza hatua za msingi zinazohitajika ili kuchapisha sura ya saa iliyoundwa kwa kutumia Muundo wa Sura za Saa kwenye Google Play.

Unaweza kutumia Dashibodi ya Google Play ili uunde na udhibiti matoleo mengi ya sura zote tofauti za saa zako na usasishe kila sura ya saa panapohitajika.

Sura ya saa ni nini? 

Muundo wa Sura za Saa unakuruhusu uunde sura maalum za saa ambazo zinaweza kuonyesha wakati kwa njia halisi kwa kutumia uwezo wa onyesho na matumizi ya vifaa vya saa mahiri.

Sura ya saa ni moja ya njia za wazi zaidi ambazo watumiaji wanaweza kujieleza kwenye vifaa vyao vya Wear OS. Kuunda sura ya saa ni njia bora zaidi unayoweza kutumia kuangazia chapa na mawazo yako kwa watumiaji kwenye Wear OS.

Unda na usambaze sura ya saa yako

Ili uchapishe sura ya saa kwenye Google Play, lazima kwanza ufungue akaunti ya Msanidi Programu wa Google Play. Ikiwa bado huna akaunti, fuata hatua hizi ili ufungue akaunti ya Msanidi Programu wa Google Play. Ikiwa tayari una akaunti na programu, nenda katika Sehemu ya 2: Unda ukurasa wa kina wa programu katika Google Play.

Hatua ya 1: Unda programu yako

Fuata hatua hizi ili uunde na kuweka mipangilio ya programu yako. Wakati wa kubainisha iwapo unaunda programu au mchezo, chagua programu.

Hatua ya 2: Unda ukurasa wa kina wa programu katika Google Play

Hatua ya kuunda ukurasa wa kina wa programu katika Google Play itafanya sura ya saa yako iweze kutambulika zaidi kwenye Google Play na inasaidia watumiaji kuelewa wanachoweza kutarajia kabla ya kuipakua. Unaweza kudhibiti ukurasa wa programu katika Google Play wa sura ya saa yako kwenye Ukurasa mkuu wa programu katika Google Play (Kuza > Upatikanaji kwenye Duka > Ukurasa mkuu wa programu katika Google Play) katika Dashibodi ya Google Play.

Zifuatazo ni baadhi ya njia unazoweza kutumia kuhakikisha kwamba una ukurasa wa programu katika Google Play wa ubora wa juu:

Hatua ya 3: Unda kikundi cha Wear OS

Kwa sababu sura ya saa yako itapatikana tu kwa vifaa vya Wear OS, unaweza kuunda kikundi cha Wear OS na kuunda toleo la Wear OS:

  1. Fungua Dashibodi ya Google Play kisha nenda kwenye ukurasa wa Mipangilio ya kina (Toleo > Mipangilio > Mipangilio ya kina).
  2. Chagua kichupo cha Maumbo na ubofye Weka umbo jipya.
  3. Chagua Wear OS.
  4. Fuata maagizo yaliyo kwenye skrini ili:
  5. Rudi kwenye ukurasa wa Mipangilio ya kina na ubofye Dhibiti kwenye Wear OS.
  6. Kubali sheria na masharti ya usambazaji. 

Baada ya kujijumuisha na kuchapisha programu yako, timu yetu itaikagua ili kuhakikisha kuwa inafuata mwongozo wa Ubora wa programu ya Wear OS. Unaweza pia kuchagua kujiondoa ukibadili mawazo yako baadaye.

Hatua ya 4: Chapisha sura ya saa yako

Tunapendekeza ujaribu sura ya saa yako kabla ya kutayarisha na kusambaza toleo kwenye Toleo la umma la sura ya saa yako ili watumiaji waweze kuipata kwenye Google Play. Kuchapisha sura ya saa yako. Ili kutayarisha na kusambaza toleo kwenye Toleo la umma la sura ya saa yako na kuiwezesha ipatikane kwa watumiaji wa Google Play:

  1. Fungua Dashibodi ya Google Play kisha nenda kwenye ukurasa wa Toleo la umma . 
  2. Kwenye upande wa kulia juu ya ukurasa, chagua Wear OS pekee kwenye menyu kunjuzi ya umbo.  
  3. Bofya Unda toleo jipya na ufuate maagizo yaliyo kwenye skrini ili uunde toleo lako la umma.
    • Kidokezo: Unaweza kutembelea makala haya ya Kituo cha Usaidizi kwa maelekezo kuhusu jinsi ya kuunda toleo.
  4. Kwenye skrini ya "Kagua kwanza na uthibitishe", hakikisha hakuna matatizo yoyote kwenye toleo lako kabla ya kulisambaza kwa watumiaji.
    • Kumbuka: Ukiona hitilafu, maonyo au ujumbe wowote, bofya Onyesha zaidi ili usome maelezo na utatue matatizo yoyote. 
  5. Ikiwa unasasisha sura ya saa iliyopo, chagua asilimia ya usambazaji.
  6. Chagua Anza kusambaza.
    • Kama unasambaza sura ya saa yako mara ya kwanza katika toleo la umma, ukibofya Anza usambazaji wa toleo la umma utasambaza pia sura ya saa yako kwa watumiaji wote wa Google Play katika nchi ulizochagua.

Baada ya Google kukagua na kuidhinisha kazi yako, sura ya saa yako itapatikana kwa watumiaji kwenye Google Play.

Je, maelezo haya yamekufaa?

Tunawezaje kuboresha?

Je, unahitaji usaidizi mwingine?

Jaribu hatua zifuatazo:

Tafuta
Futa utafutaji
Funga kisanduku cha kutafutia
Menyu kuu
12635692337842073446
true
Tafuta kwenye Kituo cha Usaidizi
true
true
true
true
true
92637
false
false