Kudhibiti matoleo tofauti ya umbo kwenye vikundi mahususi

Tunafanya mabadiliko kuhusu jinsi programu za Wear OS zinachapishwa. Ili uchapishe machapisho ya Wear OS baada ya mwisho wa Agosti, anzisha kikundi lengwa maalum cha Wear OS. Angalia sehemu ya Hamisha matoleo yaliyopo ya Wear OS hapa chini kwa maelezo zaidi.
Unaweza kutumia vikundi mahususi ili kudhibiti matoleo ya programu ya maumbo tofauti — kama vile programu za Android TV na Wear OS — katika Dashibodi ya Google Play.

Kufahamu mabadiliko ya kikundi katika Dashibodi ya Google Play

Kwa sasa tunafanya mabadiliko kwenye jinsi wasanidi programu wanavyodhibiti matoleo yao kwa kila umbo kwa kuweka vikundi lengwa mahususi vya maumbo tofauti. Hii hufanya iwe rahisi kwa wasanidi programu

  • Kusambaza matoleo fulani (kwa mfano, toleo la Wear OS) yasiyotegemea matoleo ya maumbo mengine.
  • Kurahisisha kufanya majaribio kwa kuwa na vikundi mahususi vya kuweka mipangilio na kudhibiti wachunguzaji.

Mnamo Machi 2023, tuliwezesha kikundi cha "Wear OS Pekee" hasa kwa APK na App Bundle za Wear OS, ambacho kinadhibitiwa kivyake tofauti na kikundi lengwa cha kifaa cha mkononi. Mnamo Oktoba 2023, tulianzisha kikundi mahususi cha matoleo ya Android TV: "Android TV Pekee."

Ikiwa una toleo lililopo la Wear OS kwenye kikundi cha kawaida, lazima ulihamishie kwenye kikundi cha Wear OS. Soma sehemu iliyo hapa chini kwa maelezo zaidi.

Kuhamisha matoleo yaliyopo na kutumia vikundi mahususi

Iwapo kwa sasa una programu za Wear OS ambazo ungependa kuendelea kuzisambaza kwenye Google Play, ni lazima uhamishe matoleo haya kutoka kwenye kikundi lengwa cha kifaa cha mkononi hadi kwenye vikundi vyake mahususi. Unaweza pia kurahisisha udhibiti wa programu yako ya Android TV ukitumia kikundi mahususi cha Android TV.

Panua au ukunje sehemu zilizo hapa chini ili upate maelezo kuhusu jinsi ya kuhamishia matoleo yaliyopo kwenye vikundi vyake mahususi katika Dashibodi ya Google Play.

Kuhamisha toleo lililopo la Wear OS

Kufikia mwezi Septemba 2023, matoleo ya Wear OS ambayo bado hayajahamishwa kutoka kwenye vikundi lengwa vya kifaa cha mkononi bado yanatumiwa na watumiaji, lakini huwezi kuyasasisha. Lazima uhamishie matoleo haya kwenye kikundi cha Wear OS Pekee ili uyasasishe.

Ili uhamishe toleo lako:

  1. Fungua Dashibodi ya Google Play, nenda kwenye ukurasa wa Toleo la umma (Toleo > Toleo la umma)..
  2. Iwapo toleo lako lina App Bundle ya Wear OS, utaona arifa kwenye sehemu ya juu ya ukurasa inayobainisha kwamba App Bundle yako ina programu ya Wear OS na itazuiwa ili isisambazwe. Bofya Unda kikundi cha Wear OS chini ya arifa.
  3. Chagua mojawapo ya chaguo zifuatazo:
    • Nakili wachunguzaji, nchi na App Bundle kutoka kwenye vikundi vilivyopo: Wachunguzaji, nchi na App Bundle zitanakiliwa kutoka kwenye vikundi vyako vya majaribio na vya matoleo ya umma. Bado utaweza kufanya mabadiliko. App Bundle hazitanakiliwa katika vikundi ambavyo mchakato wa kusambaza kwa hatua unaendelea. Ili unakili App Bundle, kamilisha mchakato wako wa kusambaza kwa hatua kabla ya kuendelea. Ikiwa wewe ni mtumiaji wa API, utahitaji kusasisha mchakato wako wa ujumuishaji ili utumie kitambulisho kipya cha kikundi.
    • Usinakili wachunguzaji, nchi na App Bundle: Ukiteua chaguo hili, utahitaji kuweka maelezo haya wakati unatayarisha toleo lako la Wear OS.
  4. Bofya Unda vikundi
  • Baada ya kuanza kusambaza programu yako kwa watumiaji kupitia kikundi lengwa cha Wear OS Pekee, ondoa APK na App Bundle zisizohitajika za Wear OS kwenye kikundi chako lengwa cha kifaa cha mkononi. Kufikia hapa, unaweza kudhibiti watumiaji na matoleo yako ya Wear OS kivyake kwenye toleo lako la kifaa chako cha mkononi au matoleo mengine ya maumbo.
Kutumia kikundi lengwa mahususi kwa programu za Android TV

Si lazima utumie kikundi lengwa mahususi kwa programu za Android TV na unaweza kuendelea kusambaza programu ya Android TV kwa watumiaji kupitia kikundi chako lengwa cha kifaa cha mkononi. Hata hivyo, kama mbinu bora, tunapendekeza utumie kikundi lengwa mahususi kwa Android TV.

Ili utumie kikundi lengwa mahususi cha programu za Android TV:

  1. Fungua Dashibodi ya Google Play kisha uende kwenye ukurasa wa Mipangilio ya kina (Toleo > Mipangilio > Mipangilio ya kina).
  2. Chagua kichupo cha Umbo.
  3. Ikiwa bado hujalenga Android TV, bofya + Weka umbo kisha uchague Android TV. "Android TV" itawekwa kwenye kichupo cha Maumbo.
  4. Karibu na "Android TV," bofya Dhibiti.
  5. Karibu na "Matoleo," chagua Tumia kikundi lengwa mahususi cha Android TV.
  6. Chagua Jijumuishe kwenye Android TV. Programu yako itakaguliwa kulingana na mwongozo wa ubora wa Android TV.
    • Kumbuka: Ili ujijumuishe kwenye Android TV, lazima uwe umepakia picha za skrini za Android TV za kurasa zote za programu katika Google Play. Ikiwa bado hujafanya hivyo, unaweza kubofya Hifadhi, upakie picha zako za skrini za Android TV, kisha urudi kwenye mchakato wa kujijumuisha.
  7. Bofya Hifadhi.
    • Kumbuka: Baada ya kuhifadhi, utadhibiti watumiaji na matoleo yako ya Android TV kivyake kwenye toleo lako la programu ya kifaa cha mkononi (au lingine). Huwezi kubadilisha hatua hii.

Baada ya kuanza kusambaza programu yako kwa watumiaji kupitia kikundi lengwa cha Android TV, ondoa APK na App Bundle zisizohitajika kwenye kikundi chako lengwa cha kifaa cha mkononi. Kufikia hapa, unaweza kudhibiti watumiaji na matoleo yako ya Android TV kivyake kwenye toleo lako la kifaa chako cha mkononi au matoleo mengine ya maumbo.

Dokezo kwa watumiaji wa API

Baada ya kuunda vikundi lengwa maalum vya Wear OS, hutaweza tena kutumia API iliyopo kuchapisha APK au App Bundle ya Wear OS kwa kutumia kikundi chako cha kifaa cha mkononi. Lazima usasishe mchakato wako wa ujumuishaji ili utumie vitambulisho vipya vya kikundi cha Wear OS.

Pata maelezo zaidi kuhusu kutambua vikundi vya maumbo kwenye tovuti ya Wasanidi Programu wa Android.

Kutayarisha toleo jipya

Panua au ukunje sehemu zilizo hapa chini ili upate maelezo kuhusu jinsi ya kutayarisha toleo kwa vikundi tofauti vya maumbo katika Dashibodi ya Google Play.

Kutayarisha toleo jipya la Wear OS

Masharti ya msingi: Iwapo unaunda hali ya utumiaji wa Wear OS kwa mara ya kwanza, ni lazima utumie App Bundle inayoweza kutumia Wear OS. Hatua ya kutumia App Bundle inayoweza kutumia Wear OS inamaanisha kuwa unahitaji tu kuunda, kuambatisha cheti na kupakia kizalia kimoja cha programu mara moja ili uweze kutumia toleo lililosakinishwa la programu yako na huduma ya Wear OS.

Ili kutayarisha kwa ajili ya kusambazwa kwenye Wear OS:

  1. Fungua Dashibodi ya Google Play kisha nenda kwenye ukurasa wa Mipangilio ya kina (Toleo > Mipangilio > Mipangilio ya kina).
  2. Chagua kichupo cha Maumbo kisha ubofye Weka umbo jipya.
  3. Chagua Wear OS.
  4. Fuata maagizo yaliyo kwenye skrini ili:
  5. Rudi kwenye ukurasa wa Mipangilio ya kina, kisha ubofye Dhibiti katika sehemu ya "Wear OS".
  6. Kubali sheria na masharti ya usambazaji.

Baada ya kujijumuisha na kuchapisha programu yako, timu yetu itaikagua ili kuhakikisha kuwa inafuata mwongozo wa Ubora wa programu ya Wear OS. Unaweza pia kuchagua kujiondoa ukibadili mawazo yako baadaye. Unaweza pia kujiunga ili uweze kujumuishwa katika mikusanyiko ya Wear OS kwenye Google Play.

Pata maelezo zaidi kuhusu jinsi ya kusambaza programu yako kwenye Wear OS.

Kutayarisha toleo jipya la Android TV

Masharti: Ikiwa unatayarisha toleo la Android TV kwa mara ya kwanza, lazima utumie App Bundle ya Android TV. Hatua ya kutumia App Bundle ya Android TV inamaanisha unahitaji tu kuunda, kuambatisha cheti na kupakia kizalia kimoja cha programu mara moja ili uweze kutumia toleo lililosakinishwa la programu yako na tole la Android TV.

Ili utayarishe kwa ajili ya usambazaji kwenye Android TV:

  1. Fungua Dashibodi ya Google Play kisha nenda kwenye ukurasa wa Mipangilio ya kina (Toleo > Mipangilio > Mipangilio ya kina).
  2. Chagua kichupo cha Maumbo kisha ubofye Weka umbo jipya.
  3. Chagua Android TV.
  4. Fuata maagizo yaliyo kwenye skrini ili:
    • Upakie picha ya skrini ya Android TV; na
    • Upakie App Bundle ya Android TV kwenye kikundi cha kujaribu.
  5. Urudi kwenye ukurasa wa Mipangilio ya kina kisha ubofye Dhibiti kwenye sehemu ya "Android TV".
  6. Ukubali sheria na masharti ya usambazaji.

Baada ya kujijumuisha na kuchapisha programu yako, timu yetu itaikagua ili kuhakikisha kuwa inafuata mwongozo wa ubora wa programu ya TV. Unaweza pia kuchagua kujiondoa ukibadili mawazo yako baadaye. Unaweza pia kujijumuisha ili uweze kujumuishwa katika mikusanyiko ya Android TV kwenye Google Play.

Pata maelezo zaidi kuhusu jinsi ya kusambaza programu yako kwenye Android TV.

Kubatilisha uchapishaji wa programu

Unapobatilisha uchapishaji wa programu, watumiaji waliopo bado wanaweza kutumia programu yako na kupokea masasisho ya programu. Programu yako haitapatikana kwenye Google Play, kwa hivyo watumiaji wapya hawataweza kuipata na kuipakua.

Masharti: Kabla ya kubatilisha uchapishaji wa programu, ni lazima uhakikishe kuwa:

Ili ubatilishe uchapishaji wa programu yako:

  1. Fungua Dashibodi ya Google Play kisha uende kwenye ukurasa wa Mipangilio ya kina (Toleo > Mipangilio > Mipangilio ya kina).
  2. Kwenye kichupo cha Upatikanaji wa Programu, chagua Zilizobatilisha uchapishaji.

Iwapo ungependa kufanya programu yako ipatikane tena kwa watumiaji wapya, unaweza kurudi hapa kisha uchague Zilizochapishwa.

Maswali yanayoulizwa sana

Ni wakati gani ambapo kikundi chaguomsingi huacha kutumika kwa vifaa vya Wear OS?

Kikundi chaguomsingi kitaacha kiotomatiki kutumika kwa vifaa vya Wear OS wakati toleo lako la Wear OS katika kikundi cha "Wear OS Pekee" limekaguliwa, kuidhinishwa na linapatikana kwenye Google Play.

Ni nini kitafanyika kwa APK na App Bundle za Wear OS zilizosalia kwenye kikundi chaguomsingi wakati na baada ya kipindi cha uhamishaji?

Zitatumiwa kwa vifaa vya Wear OS katika kipindi cha uhamishaji kuanzia Mei hadi mwisho wa Agosti. Kuanzia Septemba, wakati kipindi cha uhamishaji kitaisha, utadokezwa uondoe APK na App Bundle zozote za Wear OS zitakazobaki kwenye vikundi chaguomsingi.

Je, maelezo haya yamekufaa?

Tunawezaje kuboresha?

Je, unahitaji usaidizi mwingine?

Jaribu hatua zifuatazo:

Tafuta
Futa utafutaji
Funga kisanduku cha kutafutia
Menyu kuu
16977680169486580640
true
Tafuta kwenye Kituo cha Usaidizi
true
true
true
true
true
92637
false
false