Kujiandikisha kwenye jaribio la chaguo mbadala la utozaji

Kuanzia tarehe 13 Machi, 2024, wasanidi programu wanaotoa mfumo mbadala wa utozaji kama sehemu ya jaribio la chaguo mbadala la utozaji, lazima watumie API za mfumo mbadala wa utozaji. Angalia maelezo hapa chini na utembelee mwongozo wetu wa ujumuishaji wa API ya mfumo mbadala wa utozaji ili uanze.

Jaribio hili limebuniwa ili kujaribu utoaji wa chaguo la mfumo mbadala wa utozaji sambamba na mfumo wa utozaji wa Google Play na kutusaidia kugundua namna za kutoa chaguo hili kwa watumiaji. Tunatumai kupokea maoni kutoka kwa masoko mbalimbali ili kuhakikisha kuwa tunadumisha hali bora ya utumiaji. Ada za huduma, ambazo hutumika katika uwekezaji wetu kwenye Google Play na Android, zitaendelea kutumika na sharti wasanidi programu walipe Google ada husika za huduma.

Wasanidi programu wanaotimiza vigezo na masharti yafuatayo wanaweza kujiunga kwenye jaribio.

Masharti ya Kujiunga

Ili utimize masharti ya kujiunga kwenye jaribio hili:

  • Ni lazima programu yako iwe:
    • Programu ya michezo au ya kawaida kwenye maumbo yoyote yanayowapatia watumiaji chaguo mbadala la utozaji katika eneo la EEA; au
    • Programu ya vifaa vya mkononi au vishikwambi isiyo ya michezo inayotumiwa na watumiaji katika maeneo mengine yote yaliyoorodheshwa hapo juu.
  • Msanidi programu ni lazima awe biashara iliyosajiliwa.

Masharti

Wasanidi programu wanaoshiriki katika jaribio hili ni lazima watii masharti yafuatayo:

  1. Wawe wanatoa tu chaguo mbadala la utozaji kwa watumiaji waliotimiza masharti katika masoko ambapo jaribio lilitangazwa kufanywa, ambayo kwa sasa ni:
    • Nchi Washirika katika Makubaliano ya Kiuchumi ya Ulaya (EEA)
    • Australia
    • Brazili
    • Indonesia
    • Japani
    • Afrika Kusini
    • Marekani
  2. Wawe wanatoa tu mifumo mbadala ya utozaji ndani ya programu.
  3. Kutii Kiwango cha Usalama wa Data cha Sekta ya Kadi za Malipo (PCI-DSS) (ikiwa unashughulikia data ya kadi ya mkopo na malipo).
  4. Kutoa huduma kwa wateja wanaotumia mfumo mbadala wa utozaji (ikijumuisha bidhaa zozote zinazouzwa kupitia mfumo mbadala wa utozaji) na mfumo mbadala wa utozaji ni lazima ubainishe mchakato wa kupinga miamala ambayo haijaidhinishwa.
  5. Walipe Google ada za huduma zinazotumika. Mtumiaji akinunua kupitia mfumo mbadala wa utozaji, ada ya kawaida ya huduma ambayo msanidi programu hulipa itapunguzwa kwa asilimia 4.
  6. Jumuisha API za mfumo mbadala wa utozaji, hatua inayorahisisha utekelezaji wa masharti ya hali ya utumiaji na kuripoti. Wasanidi programu ambao hawako tayari kujumuisha API za mfumo mbadala wa utozaji wana chaguo la kutekeleza skrini ya chaguo za mtumiaji wao wenyewe na kuripoti miamala hadi tarehe 13 Machi 2024.
  7. Kabla ya kujumuisha API za mfumo mbadala wa utozaji, wasanidi programu wanahitajika kufuata mwongozo wetu wa muda wa hali ya utumiaji ili kudumisha hali thabiti ya utumiaji na kuwasaidia watumiaji kufanya uamuzi sahihi.
  8. Tuarifu mapema kuhusu mabadiliko unayokusudia kufanya kwenye mapendeleo yako ya kuandikisha programu, kama vile kuzima au kuwasha kipengele cha chaguo mbadala la utozaji kwenye programu au soko linalotimiza masharti. Kwa maelezo zaidi kuhusu jinsi ya kuwasilisha mabadiliko, tembelea ukurasa wetu wa Maswali Yanayoulizwa Sana.

Tafadhali kumbuka kwamba vigezo na masharti vinaweza kubadilika na tunatarajia kuwa maelezo ya jaribio kuendelea kubadilika kadiri tunavyopata maelezo zaidi na kupokea maoni ya ziada.

Kujumuisha API za mfumo mbadala wa utozaji

Ikiwa ungependa kutoa chaguo mbadala la utozaji na utakuwa unatumia API za mfumo mbadala wa utozaji kuanzia tarehe ya kutoa chaguo hilo, sharti ukamilishe hatua zifuatazo:

  1. Kagua masharti kwenye ukurasa huu ili ubaini iwapo programu zako zinatimiza masharti ya kujiunga.
  2. Jaza fomu ya taarifa ya malipo, kubali Sheria na Masharti na ukamilishe hatua zozote za kuanza ushirikiano wa kimkataba zinazohitajika ili ujiandikishe kwenye mpango, kupitia kwa usaidizi wa timu ya usaidizi ya Google (kwa mfano, unahitajika kuweka mipangilio ya taarifa zako za malipo inavyohitajika).
  3. Kamilisha mchakato wa ujumuishaji wa API za mfumo mbadala wa utozaji kama inavyoelezwa kwenye mwongozo huu wa ujumuishaji wa API.
  4. Dhibiti mipangilio ya mfumo mbadala wa utozaji wa Dashibodi yako ya Google Play, ili kujijumuisha au kujiondoa kwenye kila programu yako, kupakia nembo za njia ya kulipa na URL za kudhibiti usajili.
  5. Ripoti kwa Google Play miamala yote iliyoidhinishwa kutoka kwa watumiaji katika masoko za majaribio ndani ya saa 24. Tumia API za mfumo mbadala wa utozaji kuripoti.
  6. Kwa usajili wowote unaoendelea ulioanzishwa ulipokuwa unatoa mfumo mbadala wa utozaji bila uwekaji otomatiki, utahitajika kuuhamisha kupitia ExternalTransactions API kabla ya kuripoti miamala inayorudiwa kupitia kwenye API. Uhamishaji huu wa mara moja lazima ufanyike kabla ya tarehe 13 Machi 2024, ambayo ni tarehe ya mwisho ya kuhamia kwenye API ya mfumo mbadala wa utozaji. Kwa maelezo zaidi, tembelea ukurasa wetu wa Maswali Yanayoulizwa Sana.

Ikiwa tayari unashiriki kwenye mpango huo na unahamia kwenye API za mfumo mbadala wa utozaji, unaweza kuruka hatua ya 1 na 2 hapo juu. Baada ya kukamilisha hatua zilizoainishwa hapo juu na kuanza kuripoti miamala kwa kutumia API, huhitaji tena kutuma miamala wewe mwenyewe.

Ujumuishaji bila uwekaji otomatiki

Ikiwa ungependa kutoa chaguo mbadala la utozaji lakini hauko tayari kujumuisha API za mfumo mbadala wa utozaji, sharti ukamilishe hatua zifuatazo ili ujiandikishe mwenyewe:

  1. Kagua masharti kwenye ukurasa huu ili ubaini iwapo programu zako zinatimiza masharti ya kujiunga.
  2. Jaza fomu ya taarifa ya malipo, kubali Sheria na Masharti na ukamilishe hatua zozote za kuanza ushirikiano wa kimkataba zinazohitajika ili kujiandikisha kwenye mpango, kupitia kwa usaidizi wa timu ya usaidizi ya Google (kwa mfano, unahitajika kuweka mipangilio ya taarifa zako za malipo inavyohitajika).
  3. Kwa kutumia fomu ya kujiandikisha ambayo utatumiwa kwa njia ya barua pepe baada ya kujaza fomu ya taarifa ya bili, bainisha programu na masoko yanayotimiza masharti, ambapo utakuwa ukitoa chaguo mbadala la utozaji.
  4. Fuata masharti kama yalivyoelezwa kwenye ukurasa huu.
  5. Piga hesabu ya kiasi cha miamala yote inayolipwa kupitia mfumo mbadala wa utozaji na uripoti kwa Google Play kwa madhumuni ya kutuma ankara. Maagizo ya jinsi ya kuripoti kila mwezi yatatolewa kwa wasanidi programu wanaojaza fomu ya taarifa na kukamilisha hatua za kujiunga kwenye jaribio.
  6. Kabla ya tarehe ya mwisho ya uhamisho, jumuisha API za mfumo mbadala wa utozaji, hamisha usajili wowote unaoendelea ambao ulianza ulipokuwa unatoa mfumo mbadala wa utozaji bila uwekaji otomatiki na usasishe mipangilio ya mfumo wako mbadala wa utozaji kwenye Dashibodi ya Google Play. Baada ya kuhamisha usajili unaoendelea na kuanza kutumia API kuripoti miamala, huhitaji tena kutuma miamala wewe mwenyewe. Uhamishaji huu wa mara moja lazima ufanyike kabla ya tarehe 13 Machi 2024, ambayo ni tarehe ya mwisho ya kuhamia kwenye API ya mfumo mbadala wa utozaji. Kwa maelezo zaidi, tembelea ukurasa wetu wa Maswali Yanayoulizwa Sana.

Ikiwa una maswali yoyote ya ziada, unaweza kuwasiliana na timu yetu ya usaidizi hapa.

Fungua fomu ya taarifa

Maswali yanayoulizwa sana

Kwa nini mfumo wa utozaji wa Google Play unahitajika pamoja na mfumo mbadala wa utozaji kwa jaribio hili?

Google Play inaamini kuwa watumiaji wanapaswa kuwa na chaguo la kutumia mfumo wa utozaji wa Google Play wanapofanya ununuzi wa bidhaa dijitali kwenye programu zilizosakinishwa kutoka Google Play. Tumeunda mfumo wa utozaji wa Google Play kwa viwango vya juu vya usalama na faragha ili watumiaji wawe na uhakika wanapofanya ununuzi wa ndani ya programu. Pia, mifumo mbadala ya utozaji huenda isitoe viwango vya ulinzi au chaguo na vipengele vya malipo sawa na vya mfumo wa utozaji wa Google Play — kama vile vidhibiti vya wazazi, njia za kulipa za familia, udhibiti wa usajili, kadi za zawadi za Google Play na Pointi za Google Play.

Kwa nini bado mnatoza ada ya huduma?

Ada ya huduma ya Google Play haijawahi kamwe kuwa ada ya uchakataji wa malipo tu. Huonyesha thamani inayotolewa na mfumo wa Android na Google Play na huendeleza uwekezaji wetu tunaoendelea kufanya katika mfumo wa Android na Google Play, ambao hutuwezesha kubuni vipengele vya watumiaji na wasanidi programu ambavyo watu hutegemea. Tembelea makala haya ili upate maelezo zaidi kuhusu ada ya huduma.

Kwa nini wasanidi wa michezo walio katika eneo la EEA pekee ndio wametimiza masharti ya kujiunga?

Kufikia tarehe 6 Machi 2024, programu za michezo ya video na zisizo za michezo ya video zinaweza kutoa chaguo mbadala la utozaji kwa watumiaji walio katika eneo la EEA. Katika masoko mengine yote yaliyotimiza masharti, programu zisizo za michezo ya video pekee ndizo zinaweza kutoa chaguo mbadala la utozaji. Tunatarajia kuwa maelezo ya jaribio yataendelea kubadilika kadiri tunavyopata maelezo zaidi na kupokea maoni zaidi.

Je, ni nchi zipi zinazounda nchi washirika katika Makubaliano ya Kiuchumi ya Ulaya (EEA)?

Hivi sasa EEA inajumuisha: Austria, Bulgaria, Denmaki, Estonia, Hangaria, Irelandi, Isilandi, Italia, Jamhuri ya Cheki, Jamhuri ya Saiprasi, Korasia, Lasembagi, Lishenteni, Litwania, Malta, Norwe, Polandi, Romania, Slovakia, Slovenia, Ubelgiji, Ufaransa, Ufini, Ugiriki, Uhispania, Uholanzi, Ujerumani, Ureno, na Uswidi.

Ninaweza kutoa chaguo mbadala la utozaji kwa aina zipi za bidhaa?

Kipengele cha chaguo mbadala la utozaji kinaweza kutumiwa kwa maudhui na huduma dijitali, kama vile ununuzi wa ndani ya programu na usajili, kwenye programu au mchezo wowote kwenye maumbo yoyote kikitolewa kwa watumiaji katika eneo la EEA au programu za vifaa vya mkononi na za vishikwambi zisizo za michezo ya video kinapotolewa kwa watumiaji katika masoko mengine yote yaliyotimiza masharti.

Je, ninaweza kutoa mfumo wa utozaji wa Google Play kwenye baadhi ya masoko huku nikitoa chaguo mbadala la utozaji kwenye masoko mengine?

Ndiyo. Wakati wa mchakato wa kujiandikisha, utahitajika kubainisha nchi zilizotangazwa katika jaribio, ambapo utatoa chaguo mbadala la utozaji.

Je, ninaweza kushiriki kwenye majaribio yaliyotangazwa ya chaguo mbadala la utozaji na lile la mpango mbadala wa utozaji bila kujumuisha chaguo kwa mtumiaji, ikiwa nimetii Sheria ya Masoko Dijitali (DMA) iliyopitishwa hivi karibuni kwa watumiaji wanaoishi kwenye nchi washirika katika Makubaliano ya Kiuchumi ya Ulaya (EEA)?

Ndiyo. Unaweza kushiriki kwenye majaribio yote, lakini wakati wa mchakato wa kujiandikisha, utahitajika kubainisha iwapo unatoa chaguo mbadala la utozaji au mpango mbadala wa utozaji bila kujumuisha chaguo kwa mtumiaji. Kwa programu husika, unaweza kuchagua mpango mmoja kwa wakati na nchi husika.

Tayari nimejiandikisha kwenye mpango wa nchi washirika katika Makubaliano ya Kiuchumi ya Ulaya (EEA) ya mpango mbadala wa utozaji bila kujumuisha chaguo la mtumiaji. Je, ninapaswa kujisajili tena ili kushiriki kwenye jaribio la chaguo mbadala la utozaji?

Ikiwa ulijisajili katika mpango wa EEA kabla ya tarehe 1 Septemba 2022 na ungependa kuwapa watumiaji chaguo la mfumo mbadala wa utozaji pamoja na mfumo wa utozaji wa Google Play, utahitaji kuwasilisha upya fomu ya taarifa ili ujiandikishe kwenye jaribio la chaguo mbadala la utozaji. Huhitaji kuwasilisha upya fomu ili kuendelea kutoa mpango mbadala wa utozaji bila kujumuisha chaguo kwa mtumiaji.

Ikiwa ulijisajili katika mpango wa EEA baada ya tarehe 1 Septemba 2022, huhitaji kuwasilisha upya fomu ya taarifa ili kushiriki kwenye jaribio la chaguo mbadala la utozaji. Hata hivyo, utahitajika kutujulisha kwa kuwasilisha fomu ya kujiandikisha iliyosasishwa ya kifurushi cha programu, iwapo unatoa chaguo mbadala la utozaji kwa kila moja ya nchi katika eneo la EEA.

Je, ninawezaje kutuma miamala iliyofanywa kupitia mfumo mbadala wa utozaji?

Kuanzia tarehe 14 Novemba 2023, miamala iliyofanywa kupitia mfumo mbadala wa utozaji inaweza kuripotiwa kupitia API za mfumo mbadala wa utozaji na ni sharti iripotiwe ndani ya saa 24 ya malipo kuidhinishwa. API hizi zinafanya iwe rahisi kwa wasanidi programu kuripoti na pia kuruhusu miamala iliyofanywa kupitia mfumo mbadala wa utozaji ionekane kwenye Chati Maarufu za Google Play. Tafadhali angalia Maswali Yanayoulizwa Sana hapo chini kwa maelezo zaidi kuhusu jinsi ya kuhamisha usajili unaoendelea ulioanza ulipokuwa unatoa mfumo mbadala wa utozaji bila uwekaji otomatiki.

Ikiwa bado hujajumuisha API za mfumo mbadala wa utozaji, bado unaweza kuendelea kuripoti miamala wewe mwenyewe hadi terehe 13 Machi 2024. Ukiripoti mwenyewe, unatakiwa uripoti mwenyewe kiasi cha miamala iliyolipwa mara moja kwa mwezi kufikia siku ya 5 ya kazi ya kila mwezi. Kwa mfano, ripoti ya miamala iliyofanywa mwezi Oktoba 2023 itapaswa kuripotiwa kufikia tarehe 7 Novemba 2023. Baada ya kujaza fomu ya taarifa, tutakagua maelezo yako na kukutumia maagizo kuhusu jinsi ya kuripoti miamala yako iliyolipwa na malipo unayopaswa kulipa kwa ajili ya ada za huduma na kodi zozote zinazokatwa.

Nimewasilisha fomu ya kujiandikisha ya kifurushi cha programu ili kubainisha masoko ambapo nitatumia chaguo mbadala la utozaji kwa programu yangu. Ninawezaje kuitaarifu Google kuhusu mabadiliko yoyote ya chaguo za kujiandikisha za kifurushi cha programu yangu?

Iwapo unatoa mfumo mbadala wa utozaji bila uwekaji otomatiki, unahitaji kuwasilisha fomu ya kujiandikisha ukibadilisha utoaji wa mfumo mbadala wa utozaji katika soko mahsusi kwa kifurushi fulani cha programu. Tafadhali kumbuka kuwa, masasisho yoyote yataanza kutumika tu tarehe moja ya mwezi unaofuata, majira ya (UTC), ikiwa ni pamoja na mabadiliko ya ada husika za huduma.

Iwapo unatoa mfumo mbadala wa utozaji ukitumia API za mfumo mbadala wa utozaji, unaweza kubadilisha utoaji wa mfumo mbadala wa utozaji katika soko mahususi kwenye kifurushi cha programu fulani kupitia kwa mipangilio ya mfumo mbadala wa utozaji kwenye Dashibodi ya Google Play. Masasisho yoyote yataanza kutumika mara moja ikiwa ni pamoja na ada husika za huduma.

Je, mpango huu unaruhusu watumiaji kutumia viungo kununua maudhui dijitali?

Ndiyo, mpango huu unaruhusu wasanidi programu kutumia malipo ya kwenye wavuti kama njia mbadala ya kulipa katika mwonekano wa wavuti uliopachikwa ndani ya programu zao. Kama zilivyo njia mbadala nyingine za kulipa, hizi zitategemea masharti ya mpango yaliyoorodheshwa kwenye ukurasa huu, ikijumuisha masharti ya usalama, uaminifu wa mtumiaji pamoja na ada ya huduma.

Je, ninapaswa kutoa chaguo mbadala la utozaji?

Hapana, hili ni jaribio la kujijumuisha. Ikiwa huhitaji kutoa chaguo mbadala la utozaji, huhitaji kuchukua hatua yoyote.

Je, mpango mbadala wa utozaji bado unapatikana Korea Kusini?

Ndiyo, ijapokuwa Korea Kusini si sehemu ya jaribio la chaguo mbadala la utozaji, tunazidi kuwapa wasanidi programu wote uwezo wa kutoa mfumo mbadala wa utozaji pamoja na mfumo wa utozaji wa Google Play kwa ajili ya watumiaji wao wa Korea Kusini wanaotumia vifaa vya mkononi na vishikwambi. Iwapo wewe ni msanidi programu ambaye programu yake inatumika nchini Korea Kusini, unaweza kupata maelezo zaidi kuhusu jinsi ya kutekeleza mfumo mbadala wa utozaji nchini Korea Kusini kwenye makala haya ya Kituo cha Usaidizi. Pia, ikiwa ungependa kushiriki kwenye jaribio hili la chaguo mbadala la utozaji kwa watumiaji wanaoishi katika nchi zinazoshiriki kwenye jaribio hili, utahitajika kujiandikisha kwenye jaribio hili kwa kujaza fomu ya taarifa ya utozaji.

Ikiwa ninapanga kutoa chaguo mbadala la utozaji au tayari nimelitoa, je, ninapaswa kutimiza masharti ya hali ya utumiaji yaliyobainishwa kwenye ukurasa huu kufikia lini?

Ikiwa unatoa chaguo mbadala la utozaji lenye ujumuishaji wa API za mfumo mbadala wa utozaji, masharti ya hali ya utumiaji yatatimizwa kwa kujumuisha na kutumia API za upande wa kiteja. Kuanzia tarehe 14 Machi 2023, wasanidi programu wote wanaoshiriki wanahitajika kujumuisha API za mfumo mbadala wa utozaji ili kutekeleza skrini ya chaguo la mtumiaji na kuripoti miamala.

Ikiwa bado hauko tayari kujumuisha API za mfumo mbadala wa utozaji, unatakiwa kutekeleza mwenyewe mwongozo wa muda wa hali ya utumiaji.

Je, mfumo mbadala wa utozaji bado unapatikana nchini India?

Ndiyo. Kutokana na kanuni za hivi karibuni nchini India, sasa tunawapa wasanidi programu wote uwezo wa kutoa mfumo mbadala wa utozaji pamoja na mfumo wa utozaji wa Google Play kwa watumiaji walioko India wanaofanya ununuzi wa ndani ya programu kwenye programu zinazosambazwa na Google Play kwenye simu za mkononi na kompyuta kibao. Kwa sababu huu ni mpango tofauti na jaribio letu la chaguo mbadala la utozaji, tafadhali tembelea Makala haya ya Kituo cha Usaidizi ili upate maelezo zaidi kuhusu masharti ya kutoa mfumo mbadala wa utozaji kwa watumiaji walioko India na wanaojiandikisha.

Programu yangu imeandikishwa kwenye jaribio la chaguo mbadala la utozaji kwa watumiaji walioko India. Je, ninapaswa kujisajili tena ili kushiriki kwenye mpango wa mfumo mbadala wa utozaji nchini India?

Ikiwa programu yako iliandikishwa kwenye jaribio la chaguo mbadala la utozaji kwa watumiaji walio nchini India kabla ya tarehe 22 Februari 2023, huhitaji kujiandikisha tena kupitia mpango wa mfumo mbadala wa utozaji wa nchini India. Hata hivyo, ukibadili nia yako kuhusu kutoa mfumo mbadala wa utozaji katika nchi mahususi kwa kifurushi cha programu husika, unatakiwa kufuata maagizo yaliyoainishwa katika Maswali Yanayoulizwa Sana.

Tayari nimejiandikisha kwenye jaribio kwa programu zangu zisizo za michezo ya video, je, ninahitaji kujisajili tena kwa programu yangu ya michezo ya video ili nishiriki katika jaribio la chaguo mbadala la utozaji katika eneo la EEA?

Hapana. Ikiwa unashiriki kwenye mpango wa jaribio kwa sasa, unaweza kuandikisha programu yako ya michezo ya video katika mpango wa jaribio kupitia Dashibodi ya Google Play na uanze kutoa chaguo mbadala la utozaji kwa watumiaji walio katika eneo la EEA. Fuata maagizo ya jinsi ya kuandikisha programu kwenye makala haya ya Kituo cha Usaidizi.

Ninawezaje kujumuisha API za mfumo mbadala wa utozaji katika maumbo tofauti na vifaa vya mkononi na vishikwambi ninapotoa chaguo mbadala la utozaji kwa watumiaji walio katika eneo la EEA?

API  za mfumo mbadala wa utozaji zinaweza kutekelezwa kwa njia sawa kwenye maumbo yote yaliyotimiza masharti. Unaweza kutumia mwongozo ule ule wa ujumuishaji ili upate maagizo ya kina na nyenzo za jinsi ya kuanza.

Ikiwa unapanga kutoa chaguo mbadala la utozaji kwenye kipengele cha Android Auto, tafadhali wasiliana nasi ili upate maelezo zaidi kuhusu jinsi ya kuanza.

API za mfumo mbadala wa utozaji zina manufaa yapi? Je, ninaweza kujumuisha API za mfumo mbadala wa utozaji kwa ajili ya kutekeleza skrini ya chaguo za mtumiaji kabla ya kutumia API kuripoti miamala?

Ili kurahisisha hali ya utumiaji ya msanidi programu, API za mfumo mbadala wa utozaji zimeundwa ili kujumuishwa na kutumiwa pamoja. API za mfumo mbadala wa utozaji zina manufaa yafuatayo:

  • Skrini za mfumo mbadala wa utozaji zinazotekelezwa na Google Play, kumaanisha kuwa huhitaji kuunda na kudumisha maelezo na/au skrini za chaguo wewe mwenyewe.
  • Mchakato wa kuripoti miamala uliorahisishwa. Hii huondoa chaguo la kugusa kwa mikono na hukabili hitilafu za ujumuishaji au ulinganishaji.
  • Miamala ya mfumo mbadala wa utozaji iliyoripotiwa kupitia API itaonyeshwa kwenye Chati Maarufu za Google Play.

Zaidi ya hayo, pia tumefanya maboresho yafuatayo ili iwe rahisi kwako kuanza kutumia mfumo mbadala wa utozaji:

  • Tumerahisisha hali ya utumiaji ya chaguo la mtumiaji.
  • Udhibiti wa hali ya kujihudumia katika mipangilio ya mfumo mbadala wa utozaji kupitia Dashibodi ya Google Play, kama vile kuwasha au kuzima kipengele cha chaguo mbadala la utozaji kwa kila programu inayotimiza masharti kwa kila soko, kudhibiti nembo za njia ya kulipa na URL za kudhibiti usajili.
  • Ripoti zinazoweza kuhamishwa za miamala za mfumo mbadala wa utozaji ambazo zimeripotiwa kupitia API zilizo na maelezo ya ziada kama vile kiwango cha ubadilishaji kilichotumika, kitambulisho cha kifurushi cha programu husika na kiwango cha ada ya huduma.
Ninaweza kupata wapi maelezo zaidi kuhusu jinsi ya kujumuisha API za mfumo mbadala wa utozaji?

Ni rahisi kupanua ujumuishaji wako uliopo wa mfumo wa utozaji wa Google Play ili utumie API za mfumo mbadala wa utozaji. API za mfumo mbadala wa utozaji zimeundwa kwa kutumia kanuni na miundo ile ile ya usanifu, sawa na Maktaba yetu ya Malipo kupitia Google Play na API za Msanidi Programu wa Google Play. Hii inamaanisha API hizi zinaoana na usanifu uliopo na timu zako zitakuwa na ufahamu nazo.

Katika mwongozo wetu wa ujumuishaji, tunatoa mwongozo wa kina na nyenzo kuhusu jinsi ya kuanza na kushughulikia masuala mbalimbali yanayohusu matumizi ya mfumo mbadala wa utozaji ikiwa ni pamoja na ununuzi wa mara moja na unaorudiwa. Kuna vijisehemu vya msimbo vya mfano ili kurahisisha utekelezaji. Tunakaribisha maoni kutoka kwa wasanidi programu kuhusu API hizi na nyenzo za ziada ambazo zitakuwa za manufaa. Ukiwa na maswali yoyote au maoni kuhusu API za mfumo mbadala wa utozaji, tafadhali wasiliana nasi hapa.

Tayari ninashiriki kwenye chaguo mbadala la utozaji, ninahitaji kufanya nini ili nianze kutumia API za mfumo mbadala wa utozaji?

Kabla ya tarehe ya mwisho ya kuhama, ambayo ni tarehe 13 Machi 2024, kamilisha hatua zilizoainishwa kwenye Ujumuishaji wa API za Mfumo Mbadala wa Utozaji. Baada ya kuhamisha usajili wowote unaoendelea kutoka kipindi cha kuripoti wewe mwenyewe na kuanza kuripoti miamala kwa kutumia API, huhitaji tena kutuma miamala wewe mwenyewe.

Je, ninaweza kuripoti vipi miamala inayorudiwa kupitia API mbadala za utozaji kwa usajili unaoendelea ambao ulianza nilipokuwa nikitoa mfumo mbadala wa utozaji bila uwekaji otomatiki?

Kwa usajili wowote unaoendelea ulioanzishwa ulipokuwa unatoa mfumo mbadala wa utozaji bila kuripoti otomatiki, utahitajika kuuhamisha kupitia ExternalTransactions API kabla ya kuripoti miamala inayorudiwa kupitia kwa API. Uhamishaji huu wa mara moja lazima ufanyike kabla ya tarehe 13 Machi 2024, ambayo ni tarehe ya mwisho ya kuhamia kwenye API ya mfumo mbadala wa utozaji. Baada ya kuhamisha, unahitaji tu kuripoti miamala inayorudiwa kupitia API na huhitaji tena kuripoti kupitia mfumo wa kuripoti mwenyewe.

Ikiwa bado hujahamisha usajili unaoendelea, bado unatakiwa kuendelea kuripoti miamala inayorudiwa kupitia maagizo yaliyopo ya kuripoti mwenyewe.

Je, maelezo haya yamekufaa?

Tunawezaje kuboresha?

Je, unahitaji usaidizi mwingine?

Jaribu hatua zifuatazo:

true
Tafuta
Futa utafutaji
Funga kisanduku cha kutafutia
Menyu kuu
8982966114973006383
true
Tafuta kwenye Kituo cha Usaidizi
true
true
true
true
true
92637
false
false