Kufahamu sera ya Google Play ya Better Ads Experiences

Katika sera yetu ijayo ya Better Ads Experiences, tumeweka mwongozo unaolenga matangazo ya katikati yasiyotarajiwa, mtumiaji anapotumia programu za Google Play. Kwa kutii viwango hivi vinavyotokana na Coalition for Better Ads(CBA), tunalenga kuboresha hali ya utumiaji ya ndani ya programu kwa watumiaji wote.

Hapa chini tumejumuisha maswali yanayoulizwa sana kuhusu sera ya Better Ads Experiences. Unaweza kubofya swali ili ulipanue au kulikunja.

Maswali Yanayoulizwa Sana

Kunja Zote Panua Zote

Kwa nini Google Play inazindua sera hii?

Matangazo yasiyotarajiwa huathiri hali ya utumiaji na hupunguza imani ya watumiaji katika mfumo, hivyo tungependa kuhakikisha kuwa watumiaji wanapata hali bora za utumiaji wanapotumia programu za Google Play. Kwa kuweka viwango kwenye matukio ya kuonyesha matangazo yasiyotarajiwa kwa watumiaji wanapotumia programu zao, tunalenga kuboresha hali nzima ya utumiaji ya ndani ya programu.

Je, nini kinachukuliwa kuwa ukiukaji wa sera hii?

Kanuni ya sera ya Better Ads Experiences ni kuzuia matangazo ya skrini nzima yasiyotarajiwa, kwa kawaida wakati mtumiaji amechagua kufanya shughuli nyingine. Yasiyotarajiwa mara nyingi humaanishwa kuwa mtumiaji yupo katikati ya shughuli nyingine au mtumiaji alibofya kitufe akitarajia kuanza kutumia programu na si kuona tangazo.

Je, neno "yasiyotarajiwa" linamaanisha nini?

CBA imetoa baadhi ya mifano ya jinsi matangazo yanayoonyeshwa kwa namna fulani huchukuliwa kuwa yasiyotarajiwa. Pia, tumeorodhesha mifano hii katika sera yetu ili tuwapatie wasanidi programu ufafanuzi zaidi. Baadhi ya mifano ni kama vile matangazo yanayoonekana mwanzoni mwa ngazi ya mchezo au mwanzoni mwa sehemu ya maudhui.

Tunapendekeza uweke matangazo mahali ambapo watumiaji watategemea kuyaona. Utafiti unaonyesha kuwa huenda watumiaji wakategemea kuona matangazo mwishoni mwa ngazi ya mchezo au sehemu ya maudhui, au tangazo linapowaruhusu kuendeleza shughuli zao ndani ya programu kama vile kupitia matangazo ya ndani ya programu au yasiyo ya skrini nzima.

Ninaweza kuonyesha wapi matangazo ya katikati?

Unaweza kuonyesha matangazo ya katikati kwenye sehemu zenye mapumziko ya kawaida ya maudhui kama vile mwishoni mwa ngazi ya mchezo au sehemu ya maudhui, ilimradi yatii sera ya Matangazo ya Google Play. Mifano ya mwisho wa ngazi ya mchezo na sehemu za maudhui inaweza kujumuisha pumziko linalotokea baada ya skrini inayoonyesha alama katika programu ya michezo ya video au mwisho wa sura kwenye kitabu cha kusikiliza.

Ninaweza kuonyesha wapi matangazo ya katikati kwenye programu zisizokuwa na ngazi kama vile michezo ya idle, chemshabongo au michezo yenye ngazi zinazochukuwa muda mrefu kukamilisha?

Kama msanidi programu, unafahamu programu yako vizuri na unaweza kuweka matangazo yasiyokatiza hali ya utumiaji. Ikiwa mchezo wako hauna sehemu zenye mapumziko ya kawaida ya maudhui, tunatarajia ufanye uamuzi unaofaa ukizingatia UX unapoonyesha matangazo ya katikati, kwa njia isiyo katiza hali ya utumiaji ya ndani ya programu kwa mtumiaji. 

Pamoja na hayo, unaweza kuendelea kutumia matangazo ya zawadi na matangazo ya ndani ya programu au yasiyo ya skrini nzima yasiyokatiza matumizi ya kawaida ya programu au uchezaji wa michezo (kwa mfano, maudhui ya video yenye matangazo ndani yake, matangazo ya mabango yasiyo ya skrini nzima) ilimradi yatii Sera ya Matangazo ya Google Play.

Tangazo la zawadi ni nini? Je, matangazo ya zawadi yanajumuishwa?

Matangazo ya zawadi yanawapatia watumiaji fursa ya kutazama video au kushiriki kwenye tangazo linaloweza kuchezwa ili wapate zawadi katika programu. Yanaweza kuonekana kama kidokezo cha tangazo, chaguo la kujijumuisha, tangazo lenye zawadi au mengineyo yanayofanana na hayo. Watumiaji wanapoonyesha kwa njia dhahiri kuwa wanataka kuonyeshwa tangazo, basi hakutakuwa na wasiwasi juu ya hali ya kutotarajiwa kwa tangazo hivyo sera hii haitatumika. 

Mifano inaweza kujumuisha tangazo ambalo programu ya mchezo imeweka dhahiri kwa mtumiaji kutazama ili kufikia kipengele fulani cha mchezo au kipande cha maudhui Kwa kuwa watumiaji wamejijumuisha kwa njia dhahiri kwenye matukio ya tangazo la zawadi, matangazo haya yataruhusiwa ilimradi yafuate Sera zetu zote za Mpango wa Wasanidi Programu.

Nini kitatokea ikiwa mtoa huduma wangu wa SDK akikiuka sera hii?

Wasanidi programu wote watawajibikia msimbo waliotumia kwenye programu zao ikiwa ni pamoja na SDK na maktaba kutoka wahusika wengine. Unaweza kubadilisha uwekaji na muundo wa tangazo lako katika msimbo wa programu yako, kuweka mipangilio ya SDK ya matangazo au ushauriane na mtoa huduma wako wa SDK ya matangazo kuhusu njia sahihi za kutii sera.

Je, skrini ya utangulizi ni sawa na ukurasa wa programu unaopakia?

Skrini ya utangulizi ni skrini ya mwanzo inayotokea programu yako inapopakia chinichini. Huenda ukaona nembo ya kampuni ikifuatiwa na maandishi machache au picha zaidi zenye lengo la kumvutia mtumiaji mara ya kwanza anapotumia programu. Hata hivyo, tafadhali kumbuka kuwa si kila programu ina skrini ya utangulizi, na programu inaweza tu kupakia ukurasa wa kwanza unapoifungua.

Mifano ya skrini ya utangulizi:

 

Je, ninaruhusiwa kuweka tangazo langu baada ya skrini ya utangulizi?

Ilimradi tangazo lako linatii Sera ya Matangazo ya Google Play, unaweza kuonyesha tangazo la katikati lisilobadilika baada ya programu yako kupakiwa. Endapo programu yako haina skrini ya utangulizi, subiri hadi skrini ya kwanza ya programu yako imalize kupakia kabla ya kuonyesha matangazo.

Ninaweza kupata wapi maelezo zaidi kuhusu CBA?

Kwa maelezo zaidi kuhusu Better Ads Standards, rejelea Coalition of for Better Ads.

Je, maelezo haya yamekufaa?

Tunawezaje kuboresha?

Je, unahitaji usaidizi mwingine?

Jaribu hatua zifuatazo:

true
Tafuta
Futa utafutaji
Funga kisanduku cha kutafutia
Menyu kuu
2501595640777333955
true
Tafuta kwenye Kituo cha Usaidizi
true
true
true
true
true
92637
false
false