Mabadiliko ya usajili ya hivi karibuni kwenye Dashibodi ya Google Play

Mnamo mwezi Mei 2022, tulifanya mabadiliko katika namna ambayo bidhaa zinazolipiwa zinabainishwa na kusimamiwa kwenye Dashibodi ya Google Play. Mabadiliko haya yanakupatia urahisi mkubwa katika jinsi unavyouza usajili na kukupunguzia ugumu wa kudhibiti usajili. Baada ya kusasisha programu yako na miunganisho ya sehemu ya nyuma ya mfumo wa kompyuta au programu ili utumie API mpya za usajili, unaweza kuuza:

  • Mipango ya kulipia mapema: Watumiaji hununua kipindi mahususi na wanaweza kuongeza pesa ili kuendeleza ufikiaji wao.
  • Ofa za kusasisha: Watumiaji hupokea punguzo kwa ajili ya kuboresha viwango vyao vya usajili, kurefusha vipindi vyao vya bili au kuhama kutoka kwenye mpango wa kulipia mapema hadi mpango unaojisasisha kiotomatiki.
  • Ustahiki maalum: unaamua mantiki ya biashara na kubainisha ustahiki kwenye programu yako.

Baada ya kusasisha, ni rahisi pia kuanzisha na kusimamia ofa nyingi kwa kila usajili. Ikiwa bado hujasasisha, soma makala haya ili uelewe jinsi usajili unavyofanya kazi. 

Usajili wako wote uliopo, programu na miunganisho ya sehemu ya nyuma ya mfumo wa kompyuta au programu hufanya kazi kama ilivyokuwa kabla ya masasisho haya. Hakuna chochote unachotakiwa kufanya papo hapo – unaweza kutumia vipengele vipya vya usajili baada ya kipindi fulani cha muda.

Mabadiliko ya utendaji kazi

Ikiwa umetumia Dashibodi ya Google Play hivi karibuni, utatambua kuwa kuna mabadiliko mengi kwenye ukurasa wa Usajili (Chuma mapato > Bidhaa > Usajili). Idadi kubwa ya mabadiliko haya hukuruhusu uweke na udhibiti usajili, mipango ya msingi na ofa. Pia, kuna namna kadhaa tofauti za kufanya vitu:

  • Mabadiliko ya bei: Unapobadilisha bei ya usajili, hatua hii hutumika tu kwa ununuzi mpya. Unabadilisha bei zinazolipwa na watumiaji waliopo kwa kutumia makundi ya bei iliyopitwa na wakati.
  • Upatikanaji kulingana na eneo: Unaweza kuchagua maeneo ambapo usajili wako unaweza kununuliwa. Pia, unaweza kuanzisha ofa za kikanda katika kikundi kidogo cha maeneo hayo.  
  • Uwekaji bei kulingana na maeneo: Unaweza kubainisha bei kulingana na kila eneo. Pia, unaweza kuchagua maeneo mengi (au yote), kutoa bei moja katika sarafu unayochagua na Google Play itafanya ubadilishaji wa sarafu mara moja katika maeneo yote yaliyochaguliwa. Unaweza kusasisha bei pale inapohitajika.

Kufanya kazi kwa usajili wa zamani

Usajili uliowekwa kabla ya Mei, 2022 ulijumuisha maelezo ya usajili na kipindi kimoja cha bili, bei pamoja na jaribio lisilolipishwa au mpangilio wa bei ya utangulizi. Usajili wa ziada ulikuwa unahitajika ikiwa ulitaka vipindi vingi vya bili au kuweka bei.

Kuanzia Mei, 2022, manufaa ya usajili (kwa maneno mengine, "nini" usajili hutoa) hufafanuliwa tofauti na ofa pamoja na mipango yake ya msingi ("jinsi" ambavyo usajili huuzwa). Muundo mpya hufanya iwe rahisi kuuza usajili wako katika namna mbalimbali. 

Kwenye picha hapo chini, upande wa kushoto unaonyesha jinsi usajili ulivyokuwa unafafanuliwa hapo awali kama vitu kamili vinavyojitegemea. Ikiwa aina tofauti za "usajili" zilitoa manufaa sawa yaliyo na vipindi tofauti vya bili au bei, hali hii ingekuwa ngumu zaidi. Kwa mfano, ulipaswa kuhakikisha kuwa manufaa na maelezo yanayowalenga watumiaji yanakuwa sawa kwenye aina zote za usajili, na programu yako hairuhusu watumiaji kununua usajili usio na umuhimu.

Upande wa kulia unaonyesha jinsi usajili wa sasa ulivyoundwa. Kila usajili unaweza kuwa na mipango ya msingi kadhaa, kila mmoja ukiwa na ofa kadhaa.

Usajili uliobadilishwa

Mabadiliko haya yalipozinduliwa mnamo Mei 2022, kila usajili uliokuwa unatumika ulibadilishwa kuwa muundo mpya. Matokeo ni: 

  • Usajili huhifadhi maelezo yasiyohusiana na jinsi usajili unavyouzwa, kama vile jina linalowalenga watumiaji, maelezo na manufaa.
  • Kila usajili una mpango mmoja wa msingi wenye kipindi cha bili cha usajili wa zamani na bei inayosasishwa kiotomatiki. 
  • Ikiwa usajili ulikuwa na jaribio lisilolipishwa au bei ya utangulizi, mpango wa msingi una ofa moja iliyo na masharti ya kujiunga ya mtumiaji mpya (kwa mfano, kwa watumiaji ambao hawajawahi kununua usajili kwenye programu hii), na bei (muda wa jaribio lisilolipishwa au bei ya utangulizi na muda).

Usajili, mipango ya msingi na ofa zilizopo zina utendaji sawa kama ilivyokuwa awali. Kwa mfano, unaweza kubadilisha muda wa jaribio lisilolipishwa, kusasisha maelezo ya usajili au kubadilisha urefu wa kipindi cha muda wa kutumia bila kutozwa.

Mfano wa 1: Kubadilisha SKU iliyopitwa na wakati iliyo na bei ya utangulizi

Hivi ndivyo usajili wa kila mwezi uliopitwa na wakati ulio na jina "Mpango Msingi", Kitambulisho cha msingi1 cha bidhaa na bei ya utangulizi ya mwezi mmoja ulivyobadilishwa kuwa muundo mpya:

Mfano wa 2: Kubadilisha SKU nyingi zilizopitwa na wakati zinazowakilisha manufaa sawa ya usajili yaliyo na mipangilio tofauti:

Usajili uliopitwa na wakati ulipobadilishwa kuwa muundo mpya, ulisalia ukiwa usajili tofauti. Ubadilishaji haukuunganisha SKU zozote kuwa bidhaa zinazolipiwa. 

Kwa mfano, hali ya matumizi ya kawaida ya mfumo uliopitwa na wakati ilikuwa ni kwamba msanidi programu anaweza kuwa na usajili wa aina tofauti kwa kipindi kimoja cha usajili. Katika hali hii, SKU ya “Mpango wa Msingi” ilio na Kitambulisho cha Bidhaa cha basic1 ambayo haina bei maalum na SKU ya "Mpango wa Msingi" ilio na Kitambulisho cha Bidhaa cha basic2 kilicho na jaribio lisilolipishwa kwa watumiaji ambao hawajawahi kununua usajili wowote kwenye programu. Kushawishika kunasababisha uwepo wa usajili wa aina mbili unaotumia jina sawa, "Mpango wa Msingi", na kila mmoja unatumia Kitambulisho chake cha Bidhaa.

Kila usajili una mpango wa msingi mmoja (wa kila mwezi, unaojisasisha kiotomatiki), na SKU iliyopitwa na wakati ilio na jaribio lisilolipishwa lililotokana na usajili kuwa na ofa moja.

Ofa zinazooana na ofa za zamani

Hapo awali, Dashibodi ya Google Play na API za wasanidi programu zilifafanua usajili kuwa na mpango mmoja wa uwekaji bei. Sasa, Dashibodi ya Google Play na API za msanidi programu zinaruhusu usajili kuwa na mipango mingi ya msingi na ofa nyingi. 

Kwa kuwa programu na miunganisho ya sehemu ya nyuma ya mfumo wa kompyuta au programu inayotumia API za zamani za msanidi programu inatarajia usajili ujumuishe mpango mmoja wa uwekaji bei, kwenye Dashibodi ya Google Play kila usajili una mpango wa msingi na ofa moja ambayo ni "oanifu kwa matoleo ya awali". 

Programu yako au sehemu ya nyuma ya mfumo wa kompyuta au programu inapotumia njia za zamani za API, mpango huu wa msingi au ofa inatumika kwa kipindi cha bili, bei na kipindi chochote cha kujaribu au bei ya utangulizi. Ikiwa usajili una mipango ya msingi mingine au ofa, zitapatikana tu kwa programu zinazotumia njia mpya zaidi za API.

Kuweka alama kwenye mpango wa msingi au ofa iwe oanifu na ya zamani.

Usajili wa zamani ulipobadilishwa na kuwa katika muundo mpya, ikiwa usajili ulikuwa na jaribio lisilolipishwa au bei ya utangulizi, ofa na mpango mpya wa msingi uliwekewa alama kuwa unaoana na mpango wa msingi na ofa za zamani. Vinginevyo, ni mpango wa msingi pekee uliwekewa alama kuwa unaoana na ule wa zamani. 

Ikiwa itahitajika, unaweza kubadilisha na kuweka mpango gani wa msingi au ofa iwe inaoana na ya zamani. Kabla ya kubadilisha mpango wa msingi au ofa inayooana na matoleo ya zamani, zingatia kwa makini athari inayoweza kutokea kwenye matoleo ya zamani ya programu yanayotumia mbinu za zamani za API na kwenye vipengele vingine vyovyote vinavyoitumia.

Unaweza tu kuweka alama kwenye ofa au mpango wa msingi wenye utendaji uliokuwepo awali. Kwa mfano, mipango ya kulipa mapema, ofa za kusasisha, ofa zilizobainishwa na wasanidi programu na lebo hazitumiki.

Uwekaji bei na upatikanaji kulingana na eneo

Sasa unaweza kudhibiti upatikanaji na mpangilio wa bei kwa kila nchi au eneo mahususi na kuweka mipangilio iwapo unahitaji mpango wa msingi au ofa yako ipatikane kwenye maeneo mapya yoyote ambayo huduma za Google Play zitapatikana hapo baadaye.

Tumejaza tena usajili wako wote uliopo ili ikiwa hapo awali ulilenga "Nchi au maeneo mengine," uendelee kulenga nchi zote zilizopo kwenye kikundi hiki. Ikiwa hapo awali hukuweka mipangilio ya mpango wako wa msingi au ofa ipatikane katika "Nchi au maeneo mengine," hakuna kilichobadilika.

Unapoweka au kubadilisha mipango ya msingi au ofa, unaweza kuchagua Dhibiti upatikanaji katika nchi au eneo na ufanye mpango wa msingi au ofa yako ipatikane katika maeneo yote au uziwekee mipangilio mahususi. Pia, utaona chaguo la “Nchi au maeneo mapya”. Ikiwa utabainisha “Nchi au maeneo mapya”, Google Play inapoweka huduma ipatikane katika nchi au maeneo ya ziada, tutatumia mipangilio hii ya upatikanaji na bei. Ikiwa upatikanaji wa huduma katika nchi au maeneo haya mapya unajumuisha sarafu ya nchi alimo mnunuzi, tutafanya ubadilishaji wa sarafu wa mara moja. Ikiwa hujabainisha “Nchi au maeneo mapya,” usajili wako hautapatikana kwenye nchi au maeneo haya kwa chaguomsingi. Baada ya huduma kuanza kupatikana katika nchi au maeneo mapya, unaweza kubadilisha usajili wako kwenye Dashibodi ya Google Play ili upatikane katika maeno hayo ikiwa utapenda.

Unapobadilisha bei, unaweza kuchagua maeneo yote, bei ya maeneo mahususi na kuweka bei kwa ajili ya nchi au maeneo ambayo huduma za Google Play zitapatikana hapo baadaye.

Utendaji kwa kuponi za ofa na vipengele maalumu

Kwa sasa, vipengele kadhaa vya usajili vinatumia tu ofa inayooana na ya zamani. Vipengele hivi ni:

  • Kuponi za ofa za usajili
  • Usajili unaoangaziwa
  • Jisajili kupitia Google 

Kwenye Dashibodi ya Google Play, vipengele hivi hukuruhusu uchague usajili na si mpango wa msingi wala ofa. Unapochagua usajili, ofa ya usajili huo inayooana na ya zamani itatumika.

Muhimu: Kwa usajili wowote ambao unatumia vipengele hivi, tunapendekeza usibadilishe ofa inayooana na ya zamani bila kuzingatia kwa umakini jinsi inavyoathiri matumizi yako ya vipengele hivi.

Kufanya mabadiliko kwenye bidhaa zako zinazolipiwa

Unaweza kuweka ofa na mipango ya msingi kwenye usajili wa zamani, uliobadilishwa. Ingawa unaweza kubadilisha ofa "inayooana na matoleo ya awali", zingatia athari zinazoweza kutokea kwenye matoleo ya awali ya programu yako. Vinginevyo, unaweza kutenganisha mipangilio ya zamani na mipya kwa kuacha usajili wa zamani, uliobadilishwa jinsi ulivyo na kuunda usajili mpya ulio na ofa pamoja na mipango yake ya msingi. Hatua hii hutenganisha vizuri usajili wa zamani uliobadilishwa, unaotumika kwenye mipangilio na programu za zamani. Iwapo utaamua kubadilisha usajili wako wa zamani uliobadilishwa au la, endelea kutumia mipangilio yake pamoja na ofa zake zinazooana ili ziweze kununuliwa na watumiaji wanaotumia matoleo ya zamani ya programu yako. 

Usajili mpya unaweza kuwekewa mipangilio kwa ofa pamoja na mipango mbalimbali ya msingi, mipango ya kulipia mapema, ofa za kusasisha na vipengele vingine vipya. Ili upate maelezo zaidi ya jinsi ya kufanya hivyo, soma makala haya.

Mfano wa 3: Kuunda usajili mpya ulio na ofa pamoja na mipango mingi ya msingi

Katika mfano huu, kuna bidhaa mpya inayolipiwa kwa "Mpango wa msingi", pamoja na Kitambulisho cha bidhaa basic_new. Kuna aina mbili za mipango ya msingi chini ya usajili huu: mpango unaojirudia kila mwezi na mpango unaojirudia kila mwaka. Kila mpango una bei ya msingi, ambayo ni kiasi ambacho mtumiaji atalipa katika mizunguko ya kawaida ya kusasisha usajili na katika ununuzi wake wa kwanza ikiwa hakidhi vigezo vya ofa zozote maalum. Kila ofa chini ya kila mpango ina vigezo tofauti vya ustahiki pamoja na punguzo. Hivyo, msanidi programu anapaswa kubainisha njia zote ambazo mtumiaji anaweza kuzitumia kupata "Mpango wa Msingi" katika usajili mmoja.

Unapoweka mipangilio ya usajili wako kwa ofa na mipango mingi ya msingi, utahitaji kusasisha muunganisho wako wa Malipo kupitia Google Play ili utumie matoleo sahihi ya API kushughulikia utendaji huu mpya. Ili upate maelezo zaidi kuhusu ya jinsi ya kufanya hivyo, soma mwongozo wa uhamishaji.

Kusitisha usajili uliobadilishwa

Baada ya kuunda orodha ya biashara inayotumia muundo mpya wa usajili, mpango wa msingi, ofa na kusasisha muunganisho wako ili kushughulikia kwa usahihi bidhaa hizi mpya, unaweza kusitisha usajili wako halisi uliobadilishwa. 

Ili kuwazuia watumiaji wapya waliojisajili kununua bidhaa husika ambazo utasitisha ofa na mipango yake ya msingi ya usajili. Usajili unaotumika utaendelea kujisasisha kiotomatiki hadi utakapoghairiwa au muda wake kuisha. 

Tunapendekeza usubiri kwa muda kabla ya kuzima usajili wako uliobadilishwa hadi kiasi cha ununuzi unaofanywa katika matoleo ya awali ya programu yako kipungue. Hili litafanyika taratibu kadiri muda unavyosonga na watumiaji watahama kutoka matoleo ya zamani na kutumia matoleo mapya zaidi. Matoleo haya ya zamani yanayotumia API zilizoacha kuendesha huduma zitaacha kufanya ununuzi polepole kwenye usajili wa zamani uliobadilishwa. Wakati fulani, unaweza kuacha kuuza usajili uliopitwa na wakati kwa kusitisha ofa na mipango yake msingi. 

Watumiaji walio na usajili unaotumika kwenye mipango hiyo ya zamani bado wataweza kusasisha na kutumia usajili wao, lakini hakuna ununuzi wowote mpya unaoweza kufanyika kwenye toleo lolote lile la programu.

Kudhibiti orodha ya usajili wako kwa kutumia API

Iwapo unadhibiti orodha yako ya usajili kwa kutumia API ya bidhaa za ndani ya programu, unaweza kuendelea kufanya hivyo kwa sasa. Hata hivyo, hali hii itasababisha upatikanaji wa usajili wa mpango wa msingi na ofa moja inayooana na ya zamani na hutaweza kutumia vipengele vyovyote vipya vya usajili. Usajili wako uliobadilishwa utaendelea kupatikana kwenye Dashibodi ya Google Play katika hali ya kusoma tu.

Tunapendekeza uhamie kwenye API mpya za Uchumaji wa Mapato ya Usajili ili udhibiti usajili wako ukitumia monetization.subscriptions, monetization.subscriptions.baseplans mpya na sehemu za mwisho za monetization.subscriptions.offers. API hizi mpya zitakuwezesha kudhibiti mipango yote ya msingi na ofa zilizopo (badala ya ofa zinazooana na za zamani tu). Ili upate maelezo zaidi kuhusu jinsi ya kuhamia kwenye API hii mpya, soma mwongozo wa uhamishaji.

Iwapo utapenda kubadilisha usajili wako kwenye Dashibodi ya Google Play unaweza kubofya Fanya usajili uweze kubadilishwa chini ya ujumbe ulioonyeshwa juu ya kila usajili.  

Muhimu: Baada ya kufanya usajili uweze kubadilishwa kwenye Dashibodi ya Google Play, hutaweza tena kutumia API ya bidhaa za ndani ya programu kusoma, kuweka mipangilio au kusasisha usajili na ni lazima uhamie kwenye API za Uchumaji wa Mapato ya Usajili ili uendelee kudhibiti usajili kwa kutumia michakato ya kiotomatiki ya programu. Mabadiliko haya hayawezi kutenduliwa.

Maudhui yanayohusiana

Je, maelezo haya yamekufaa?

Tunawezaje kuboresha?

Je, unahitaji usaidizi mwingine?

Jaribu hatua zifuatazo:

true
Tafuta
Futa utafutaji
Funga kisanduku cha kutafutia
Menyu kuu
6898166924109995201
true
Tafuta kwenye Kituo cha Usaidizi
true
true
true
true
true
92637
false
false