Mabadiliko kwenye mfumo wa utozaji wa Google Play kwa watumiaji walio nchini Urusi na Belarusi

Kutokana na kukatizwa kwa mfumo wa malipo, Google Play imesitisha mfumo wake wa utozaji kwa watumiaji walio nchini Urusi kuanzia tarehe 10 Machi, 2022. Hatua hii inamaanisha kuwa watumiaji hawawezi kununua programu na michezo, kufanya malipo ya usajili au kufanya ununuzi wowote wa ndani ya programu wa bidhaa dijitali kwa kutumia Google Play nchini Urusi. Programu zisizolipishwa zitaendelea kupatikana kwenye Duka la Google Play.

Kuanzia tarehe 2 Agosti, 2022, masharti ya Sera ya malipo yanayohitaji matumizi ya mfumo wa malipo wa Google Play hayatumiki kwa wasanidi wa programu zinazosambazwa na Google Play zinazohitaji au zinazokubali malipo kwa watumiaji nchini Urusi kwa wakati huu.

Kama sehemu ya juhudi zetu za kutii, Google Play inazuia upakuaji wa programu zinazolipishwa na masasisho ya programu zinazolipishwa nchini Urusi na Belarusi.

Hali inabadilika kwa haraka na tunakuhimiza urejee katika ukurasa huu ili upate taarifa mpya. Hapa chini tumejibu baadhi ya maswali ya ziada ambayo wasanidi programu wanaweza kuwa nayo na tutaendelea kuyasasisha.

Maswali Yanayoulizwa Sana

Je, bado watumiaji wanaweza kupakua programu na michezo isiyolipishwa kutoka Google Play?

Ndiyo, watumiaji walio nchini Urusi na Belarusi bado wataweza kupakua programu na michezo isiyolipishwa kwenye Duka la Google Play.

Je, bado watumiaji wanaweza kufikia programu na michezo ambayo tayari imepakuliwa na kununuliwa?

Watumiaji wanaweza tu kufikia programu zinazolipishwa na michezo ambayo tayari imepakuliwa. Watumiaji hawawezi kufikia programu na michezo iliyonunuliwa hapo awali ambayo haijapakuliwa kwa sasa kwenye kifaa cha mtumiaji, bila kujali tarehe ya ununuzi.

Je, nini kitatokea muamala wa mtumiaji ukishindwa kutekelezwa?

Wakati mtumiaji aliye nchini Urusi anajaribu kununua programu, kuanza kufanya ununuzi wa ndani ya programu au kujisajili kupitia mfumo wa utozaji wa Google Play, ujumbe kuhusu hitilafu utaonekana na hakuna muamala utakaochakatwa.

Watumiaji walio nchini Belarusi wataona pia ujumbe kuhusu hitilafu wanapojaribu kununua programu au kujisajili kupitia mfumo wa utozaji wa Google Play. Ununuzi wa ndani ya programu au usajili ndani ya programu zisizolipishwa haujazuiwa.

Je, nini kitatokea kwa usajili uliopo wa mtumiaji aliye nchini Urusi?

Usajili utaendelea hadi mwishoni mwa kipindi cha bili cha sasa, lakini hautaweza kusasishwa tena na utaghairiwa. Tutaendelea kuheshimu mipangilio iliyopo ya usajili iliyowekwa na msanidi programu ya muda wa kutumia bila kutozwa na majaribio yoyote yasiyolipishwa yataendelea kutumika hadi jaribio la malipo litakapofanyika.

Ninawezaje kuwasaidia wanaonifuatilia kupanua ufikiaji wa maudhui nikijua kwamba malipo yao yatakataliwa nchini Urusi?

Una chaguo mbili. Kwanza, unaweza kuongeza muda wa kutumia bila kutozwa kwa watu wanaokufuatilia waliopo ili wafikie maudhui baada ya kipindi chao cha bili kuisha kwa hadi siku 30 kwenye Dashibodi ya Google Play.

Pili, unaweza kuahirisha usasishaji wa mtumiaji kwa muda wa mwaka mmoja ukitumia API ya Wasanidi programu wa Google Play. Mtumiaji atabaki na uwezo kamili wa kufikia maudhui lakini hatatozwa katika kipindi cha kuahirisha. Tarehe ya usasishaji wa usajili itasasishwa ili ionyeshe tarehe mpya.

Programu yangu inatoa huduma nyeti inayowaweka watumiaji salama na kuwawezesha kupata habari, nifanye nini?

Ukipenda, unaweza kuchagua kutoa programu yako bila malipo au kuondoa usajili wako unaolipishwa wakati wa usitishaji huu.

Je, ninaweza kuchapisha programu mpya au kusasisha programu zilizopo wakati wa usitishaji huu?

Bado unaweza kuchapisha programu mpya zisizolipishwa na kusasisha programu zilizopo zisizolipishwa. Masasisho ya programu zinazolipishwa yamezuiwa kwa sababu za kutii. 

Je, hii inaathiri vipi sera ya malipo ya Google Play?

Hakuna athari kwenye sera za malipo ya Google Playnje ya Urusi. Tafadhali tembelea Kituo chetu cha Usaidizi ili upate maelezo zaidi.

Je, hii itaathiri vipi Duka la Google Play?

Tunazima chati Maarufu Zinazolipishwa na Zenye Mapato ya Juu nchini Urusi wakati wa usitishaji huu. Chati Maarufu Zisizolipishwa zitaendelea kuonekana.

Je, kusimamisha miamala ya malipo ya Google Play nchini Urusi kutaathiri malipo ya msanidi programu?

Hapana, usitishaji huu hauathiri malipo ya msanidi programu. Ikiwa una matatizo ya kupokea malipo, tunapendekeza utumie njia mbadala ya kulipa, kama vile akaunti kutoka benki nyingine au eWallet ambayo inaruhusu malipo. Unaweza kuangalia njia mbadala za malipo kwa kuweka njia mpya ya kulipa kwenye akaunti yako. Tutazuia salio la akaunti yako hadi pale utakapoweza kutoa njia sahihi ya kulipa.

Maudhui yanayohusiana

Rejelea makala haya ya Kituo cha Usaidizi ili upate maelezo kuhusu vikwazo vya kimataifa vilivyowekwa hivi karibuni.

Je, maelezo haya yamekufaa?

Tunawezaje kuboresha?

Je, unahitaji usaidizi mwingine?

Jaribu hatua zifuatazo:

true
Tafuta
Futa utafutaji
Funga kisanduku cha kutafutia
Menyu kuu
666234796557771723
true
Tafuta kwenye Kituo cha Usaidizi
true
true
true
true
true
92637
false
false