Mipangilio ya kodi na utii ya programu zinazolipishwa, usajili na bidhaa za ndani ya programu

Ikiwa unasambaza programu inayolipishwa au iwapo programu yako inatoa usajili au bidhaa za ndani ya programu, huenda ukahitajika kutoa maelezo kuhusu bidhaa unayosambaza kwa madhumuni ya sheria ya watumiaji au kodi.

Unaweza kutoa maelezo haya katika sehemu ya “Kodi na utii”  wakati wa kuweka bei za programu zako kwenye Dashibodi ya Google Play na unapodhibiti bei za usajili au bidhaa za ndani ya programu.

Kutoa maelezo ya kodi na utii kwenye Dashibodi ya Google Play

Unaweza kuweka na kudhibiti bei kwenye kurasa zifuatazo katika Dashibodi ya Google:

  • Bei ya programu (Chuma mapato > Bidhaa > Bei ya programu)
  • Bidhaa za ndani ya programu (Chuma mapato > Bidhaa > Bidhaa za ndani ya programu > Unda bidhaa au Angalia bidhaa ya ndani ya programu)
  • Usajili (Chuma mapato > Bidhaa > Usajili > Unda usajili au Angalia usajili > Badilisha maelezo ya usajili)

Unapoweka bei za programu zako na kudhibiti bei za usajili au bidhaa za ndani ya programu, chaguo zilizoorodheshwa hapo chini zinapatikana katika sehemu ya “Kodi na utii”. Marekebisho yoyote utakayofanya kwenye uainishaji wa kodi na ushughulikiaji wa kodi husika wa bidhaa zako yatatumika tu kwa miamala ya siku zijazo.

Uainishaji wa Maudhui Dijitali au Huduma

Ikiwa programu yako inaweza kusambazwa kwa watumiaji wa kwenye nchi washirika katika Makubaliano ya Kiuchumi ya Ulaya (EEA), unapaswa kutueleza ikiwa bidhaa yako ni Maudhui Dijitali au Huduma.

Lazima urejelee Agizo namba 2011/83/EU la Bunge la Umoja wa Ulaya na la Baraza na Agizo nambari (EU) 2019/770 la Bunge la Umoja wa Ulaya na la Baraza ili kubaini ikiwa bidhaa yako inapaswa kuainishwa kama "Huduma" au kama "Maudhui Dijitali." Ikiwa huna uhakika kama bidhaa yako ni  Maudhui Dijitali au Huduma, unaweza kuiainisha kama "Huduma.'

Kumbuka: Mfumo wa kujiondoa chini ya sheria ya watumiaji ya EEA unategemea uainishaji huu. Kwa bidhaa zinazoainishwa kama Maudhui Dijitali, haki ya kujiondoa haitajumuishwa. Bidhaa zinazoanishwa kama "Huduma" zinatimiza masharti ya kurejesha pesa ndani ya siku 14 za ununuzi.

Viwango vya VAT vilivyopunguzwa

Wasanidi programu wanaouza habari dijitali, magazeti, majarida, vitabu, video, muziki, maudhui ya sauti au vitabu vya kusikiliza kwenye nchi au maeneo mbalimbali wanaweza kutimiza masharti ya viwango vya VAT vilivyopunguzwa. Ni jukumu lako kutathmini kanuni za mahali ulipo ili kubaini iwapo umetimiza masharti.

Utakapokuwa umebaini viwango vyovyote vya kodi vilivyopunguzwa unavyostahiki kutumia, unaweza kuchagua viwango vya kodi vinavyofaa katika kila nchi au eneo unakotimiza masharti.

Zingatia: Programu yako lazima iwe kwenye kundi sahihi (kwa mfano "Muziki na maudhui ya Sauti" au "Vicheza video") ili uangalie na uchague viwango vyovyote vilivyopunguzwa unavyostahiki kutumia.

Kodi za Mawasiliano na Burudani Marekani

Ikiwa unataka kukusanya kodi za jimbo za mawasiliano na burudani zinazotozwa Marekani kwa kutumia Dashibodi ya Google Play, lazima ubainishe kuwa programu au bidhaa yako ni bidhaa ya kutiririsha maudhui na uchague aina sahihi ya utiririshaji. Unaweza kupata maelezo zaidi kuhusu majimbo ambapo unaweza kukusanya kodi za mawasiliano na burudani kwenye makala ya Angalia au badilisha kiwango cha kodi ya mauzo.

Maudhui yanayohusiana

Je, maelezo haya yamekufaa?

Tunawezaje kuboresha?

Je, unahitaji usaidizi mwingine?

Jaribu hatua zifuatazo:

true
Tafuta
Futa utafutaji
Funga kisanduku cha kutafutia
Menyu kuu
16066332268464808652
true
Tafuta kwenye Kituo cha Usaidizi
true
true
true
true
true
92637
false
false