Kuzuia ubadilishaji na usambazaji ambao haujaidhinishwa ukitumia kipengele cha ulinzi otomatiki wa uadilifu

KumbukaVipengele vinavyofafanuliwa kwenye ukurasa huu kwa sasa vinapatikana kwa washirika wa Google Play waliochaguliwa pekee.

Kipengele cha ulinzi otomatiki wa uadilifu kutoka Google Play ni huduma ambayo hukusaidia kulinda programu na michezo yako dhidi ya matumizi mabaya ya uadilifu kwa njia ya ubadilishaji na usambazaji ambao haujaidhinishwa. Kipengele cha ulinzi otomatiki wa uadilifu hufanya kazi kwenye programu yako bila muunganisho wa data. Unaweza kukiwasha kwa kubofya mara moja katika Dashibodi ya Google Play na hakihitaji msanidi programu akiweke kabla ya majaribio na hakihitaji ujumuishaji wa seva inayoshughulikia sehemu ya nyuma ya mfumo wa kompyuta au programu.

Jinsi kinavyofanya kazi

Kipengele cha ulinzi otomatiki wa uadilifu huweka ukaguzi kwenye msimbo ya programu yako inapotumika ili kuzuia ubadilishaji au usambazaji, na kisha hufanya ukaguzi huo kuwa mgumu kuondolewa kwa kutumia mbinu za kina za kufumba misimbo na kuzuia utafiti wa kihandisi. Ukaguzi wa kisakinishaji usipokamilika, watumiaji wataelekezwa kupakua programu yako kutoka kwenye Google Play. Ukaguzi wa ubadilishaji usipokamilika, programu haitafanya kazi. Hali hii husaidia kulinda watumiaji dhidi ya maudhui hatari ambayo yanaweza kuonekana kwenye matoleo yaliyobadilishwa ya programu yako.

Kipengele cha ulinzi otomatiki wa uadilifu kimebuniwa kwa ajili ya malengo yafuatayo:

  • Kuzuia ubadilishaji ambao haujaidhinishwa: Kipengele cha ulinzi otomatiki wa uadilifu husaidia kulinda programu yako dhidi ya ubadilishaji, hali inayofanya iwe vigumu kusambaza nakala zisizo rasmi zenye utendaji uliobadilishwa (kama vile kuondoa malipo, kuongeza matangazo, kubadilisha kitambulisho cha mmiliki wa matangazo, au kuweka programu hasidi).
  • Kuzuia ughushi wa programu zinazolipishwa: Kipengele cha ulinzi otomatiki wa uadilifu huzuia ughushi kwa kuwadokezea watumiaji ambao wanapakua toleo la programu yako ambalo halijabadilishwa kwenye Google Play kupitia chanzo kisicho rasmi, ili wainunue kwenye Google Play. Si lazima uwashe kidokezo hiki na unaweza kukizima kwa kubatilisha uteuzi wa "Inahitaji kusakinishwa kutoka Google Play" kwenye ukurasa wa mipangilio ya ulinzi otomatiki wa uadilifu.
  • Kuongeza idadi ya watumiaji wanaopokea masasisho rasmi: Kipengele cha ulinzi otomatiki wa uadilifu kinaweza kuwadokezea watumiaji ambao hupakia toleo la programu yako ya Google Play ambayo haijabadilishwa kutoka kifaa kingine, ili waiweke kwenye maktaba yao ya Google Play ili kuhakikisha kuwa wanaweza kupokea masasisho endelevu ya programu. Si lazima uwashe kidokezo hiki na unaweza kukizima kwa kubatilisha uteuzi wa "Inahitaji kusakinishwa kutoka Google Play" kwenye ukurasa wa mipangilio ya ulinzi otomatiki wa uadilifu.
Muhimu: Kipengele cha ulinzi otomatiki wa uadilifu hakikuhakikishii uzuiaji wa matukio yote ya kukwapua, kughushi, kurekebisha kifurushi kwa madhumuni ya ulaghai na kusambaza upya. Kipengele cha ulinzi otomatiki wa uadilifu hufanya vitendo hivi kuwa vigumu na vya gharama ya juu, kwa hivyo hupunguza uwezekano kutokea. Google Play itaendelea kuboresha kipengele cha ulinzi otomatiki wa uadilifu ili matoleo mapya ya programu yako yaweke kiotomatiki toleo jipya na thabiti zaidi la ulinzi.

Weka mipangilio ya ulinzi otomatiki wa uadilifu

Hatua zilizo hapa chini zinaelezea unachopaswa kufanya ili uanze kutumia kipengele cha ulinzi otomatiki wa uadilifu. Bofya sehemu ili uipanue.

Masharti ya msingi

Ukiwasha kipengele cha ulinzi otomatiki wa uadilifu kwenye programu mahususi, Google Play itaweka kiotomatiki ulinzi unapofanya kila toleo liwe tayari kusambazwa kwenye vifaa. Ulinzi unahitaji Google Play kubuni APK zilizobadilishwa na kuweka vyeti kwa niaba yako, kwa hivyo ni lazima:

Tafadhali zingatia matatizo yafuatayo:

  • Kipengele cha ulinzi otomatiki wa uadilifu hutumika tu kwenye Android 6.0 Marshmallow (Kiwango cha API cha 23) na mapya zaidi. Android M ilichapishwa 2015 na kufikia 2023, hatua ya kulenga midSDKVersion ya 23 na matoleo mapya zaidi itafikia zaidi ya asilimia 97 ya vifaa vya Android vinavyotumika.
  • Ulinzi otomatiki wa uadilifu unatumia ABI zifuatazo: x86, x86_64, armeabi-v7a na arm64-v8a. Ili usasishe ABI lengwa la programu yako, sasisha mipangilio ya Gradle. ABI zingine ambazo hazitumiwi na vifaa vya Android vinavyotumika zinaweza kuondolewa kwenye ulengaji wako bila kuathiri upatikanaji wa programu yako.
  • Kipengele cha ulinzi otomatiki wa uadilifu hufanya kazi nje ya mtandao. Hata hivyo, mipangilio ya "Inahitaji kusakinishwa kwenye Google Play" mara kwa mara huhitaji muunganisho wa data ikiwa programu ya Play Store kwenye kifaa imekuwa nje ya mtandao kwa muda mrefu.
  • Ikiwa tayari programu yako inatumia huduma ya Utoaji Leseni wa Google Play, unapaswa kuzima mipangilio ya "Inahitaji usanikishaji kutoka Google Play".
  • Unapopakia programu yako kupitia huduma ya kushiriki programu ndani, ulinzi hautumiki. Kuwa makini zaidi kushiriki tu viungo vya kushiriki programu ndani na wanatimu wanaoaminika na usishiriki kwingine matoleo ambayo hayajalindwa.
  • Kipengele cha Ulinzi otomatiki wa uadilifu hakioani na uthibitishaji wa msimbo wa App Bundle kwa sababu ulinzi wa uadilifu unajumuisha ubadilishaji wa msimbo. App Bundle zinazopakiwa zikiwa na uthibitishaji wa msimbo wakati kipengele cha ulinzi otomatiki wa uadilifu kimewashwa zitakataliwa.
  • Hali za matumizi ya papo hapo hazilindwi. App Bundle katika vikundi lengwa haipaswi kuwa inayofunguka papo hapo ili kupata ulinzi. Unaweza kupakia App Bundle kwa wakati mmoja kwenye kikundi chako lengwa kinachopata ulinzi na App Bundle inayofunguka papo hapo kwenye kikundi chako cha papo hapo pekee ambacho hakipati ulinzi.
Hatua ya 1: Washa ulinzi

Unda toleo kama ilivyoelezewa kwenye Hatua ya 1 ya Kutayarisha na kusambaza toleo.

Unaweza kuwasha ulinzi unapounda toleo (kama ilivyoelezewa kwenye Hatua ya 2 ya Kutayarisha na kusambaza toleo) au unaweza kuwasha ulinzi kwenye ukurasa wa Uadilifu wa programu (Toleo > Uadilifu wa programu), ambao una huduma za uadilifu na kuambatisha vyeti ambazo hukusaidia kuhakikisha hali ya utumiaji wa programu na michezo yako inapatikana kama unavyokusudia.

Unapotayarisha toleo lako, utaona kitufe cha Pata ulinzi wa uadilifu au Dhibiti ulinzi wa uadilifu. Kisha unaweza kuwasha ulinzi wa uadilifu kwa kubofya Ndiyo, washa chini ya "Ulinzi otomatiki wa uadilifu." Kisha Google Play itaambatisha cheti kwenye matoleo yako na kuweka ulinzi wa uadilifu ili kuzuia uvamizi na usambazaji usioidhinishwa. Hii inamaanisha kuwa kipengele cha ulinzi otomatiki wa uadilifu kimewashwa.

Kamilisha kutayarisha toleo lako na uhifadhi mabadiliko uliyofanya.

Hatua ya pili: Jaribu programu yako inayolindwa

Tumia kila kikundi cha majaribio ili ujaribu toleo la programu inayolindwa ili uhakikishe hamna athari isiyotarajiwa kwenye utendaji au hali ya utumiaji.

Tunapendekeza ujumuishe hatua zifuatazo kwenye ukaguzi wako:

  • Jaribu kufungua mchezo wako, ukitafuta matukio ya kuacha kufanya kazi wakati wa kufungua na matukio yoyote ya kufunguka polepole inapoanza.
  • Jaribu matukio ambako msimbo wa kifaa chako (C/C++) unatekeleza kwenye Java (katika msimbo wako au maktaba za wengine), kama vile matangazo, kuingia katika akaunti, ujumuishaji wa jamii, uthibitishaji au vipengele mahususi vya Android kama vile kushughulikia ruhusa.

Ukipata matatizo wakati wa mchakato wa kujaribu, una chaguo la kurejesha toleo la awali la ulinzi otomatiki wa uadilifu ambalo huenda ulikuwa tayari umetumia katika toleo la awali au unaweza kuzima ulinzi otomatiki wa uadilifu. Tunakushauri usitangaze matoleo ambayo hayajalindwa kwa umma au watumiaji wengi.

Ili uzime ulinzi wa uadilifu kwenye toleo mahususi:

  1. Unapotayarisha toleo lako, bofya Dhibiti ulinzi wa uadilifu.
  2. Chini ya "Ulinzi otomatiki wa uadilifu," chagua Ulinzi wa awali au Zima ulinzi wa toleo hili.
  3. Hifadhi mabadiliko uliyofanya. Mabadiliko yatatumika katika toleo hili. Utakapopakia tena toleo, toleo litapata toleo jipya zaidi la ulinzi thabiti zaidi.
Hatua ya tatu: Tangaza programu yako kwenye toleo la umma

Ukiwa tayari, unaweza kusambaza toleo lako la umma katika Dashibodi ya Google Play, hali inayofanya programu yako inayolindwa ipatikane kwa watumiaji wote wa Google Play katika nchi ulizochagua.

Kuweka mapendeleo kwenye ukurasa wako wa programu katika Google Play watumiaji wanapotembelea kutoka vidirisha vya ulinzi wa uadilifu

Kipengele cha ulinzi otomatiki wa uadilifu kinaweza kuwaomba watumiaji wanaopata programu yako kwa njia isiyo rasmi waipate kwenye Google Play. Watumiaji wanapogusa kwenye kidirisha, wataelekezwa kwenye ukurasa wako wa programu katika Google Play ambapo wanaweza kugusa kitufe cha kuweka kwenye kifaa (au kununua au kusasisha) ili wapate programu yako kwenye Google Play ili programu yako iwekwe katika maktaba ya Google Play ya mtumiaji.

Unaweza kuweka mapendeleo kwenye vipengee vya ukurasa wako wa programu katika Google Play kwa watu wowote wanaoutembelea wanaogusa vidirisha vya ulinzi wa uadilifu, ikiwa ni pamoja na jina la programu, aikoni, maelezo na vipengee vyako vya picha. Ili uweke mapendeleo kwenye ukurasa wako wa programu katika Google Play watumiaji wanapotembelea kupitia kidirisha cha ulinzi wa uadilifu:

  1. Fungua Dashibodi ya Google Play kisha uende kwenye ukurasa wa Uadilifu wa programu (Toleo > Uadilifu wa programu).
  2. Nenda kwenye sehemu ya “Play Integrity API”.
  3. Bofya Mipangilio.
  4. Nenda kwenye sehemu ya "Weka mapendeleo kwenye ukurasa wa programu katika Google Play".
  5. Bofya Unda ukurasa wa programu katika Google Play.
  6. Fuata maagizo kwenye ukurasa wa Unda ukurasa maalum wa programu katika Google Play kisha bofya Hifadhi.

Pia, unaweza kuunda kurasa maalum za programu katika Google Play kwa vidirisha vya ulinzi wa uadilifu moja kwa moja kwenye ukurasa waKurasa maalum za programu katika Google Play:

  1. Fungua Dashibodi ya Google Play kisha uende kwenye ukurasa wa Kurasa maalum za programu katika Google Play (Kukuza > Kurasa Maalum za Programu katika Google Play).
  2. Bofya Unda ukurasa wa programu katika Google Play, chagua ikiwa utaunda ukurasa mpya wa programu katika Google Play au utarudufisha uliopo, kisha ubofye Inayofuata.
  3. Katika sehemu ya "Maelezo ya ukurasa wa programu katika Google Play" nenda kwenye Hadhira.
  4. Chagua Kulingana na URL na uweke 'playintegrity' katika kisanduku cha maandishi.
  5. Jaza maelezo mengine yote kisha ubofye Hifadhi.

Kidokezo: Kigezo cha URL cha ‘playintegrity’ ni neno muhimu maalum ambalo limehifadhiwa kwa viungo vya kina vya uadilifu, kwa hivyo lazima liwekwe kikamilifu kama halijahaririwa unapoweka mipangilio ya ukurasa maalum wa programu katika Google Play.

Hatua zinazopendekezwa

Usichapishe matoleo ya programu ambayo hayajalindwa

Ukichapisha matoleo ambayo hayajalindwa kwa watumiaji wengi, au kupitia vituo vingine nje ya Google Play, ulinzi wa programu yako hautafanya kazi tena. Ili udumishe ulinzi wa uadilifu wa programu yako, unapaswa kuchapisha tu matoleo yaliyolindwa ya programu yako kwa umma na watumiaji wengi.

Kuwa makini unapochanganya suluhisho za vipengele vya kulinda alama

Huenda kipengele cha ulinzi otomatiki wa uadilifu kisitumiwe na suluhisho nyingine za muda wa kutekeleza za kulinda alama na hatua ya kuzitumia pamoja inaweza kusababisha matatizo mengine kwa mtumiaji. Ikiwa tayari unatekeleza Utoaji Leseni wa Google Play kwenye programu yako, basi unapaswa kuzima mipangilio ya "Inahitaji Usanikishaji kutoka Google Play." Iwapo programu yako inafanya ukaguzi mwingine wa muda wa kutekeleza, hakikisha kuwa unajaribu kwa kina programu yako inayolindwa ili kubaini matatizo kabla ya kuichapisha kwenye kikundi cha jaribio la watu wengi.

Jaribu programu yako inayolindwa

Google Play itatoa kiotomatiki miundo iliyolindwa kwenye makundi yote: majaribio ya ndani, ya watu wachache, ya watumiaji wengi na umma. Unapaswa kujaribu matoleo haya kwa kina kama kawaida.

Ukipakia muundo wa programu yako moja kwa moja kupitia huduma ya kushiriki programu ndani, Google Play haitaweka ulinzi. Hatua hii hukuruhusu utumie huduma ya kushiriki programu ndani ili kupakia miundo ya utatuzi na miundo mingine kama hiyo.

Unapofikia kiungo cha kushiriki programu ndani kwa toleo la programu iliyolindwa kwenye kichunguzi cha App Bundle, basi muundo hushirikiwa jinsi ulivyochakatwa na Google Play. Iwapo toleo hilo la programu lilipakiwa kwenye kikundi cha kujaribu na limelindwa, basi kiungo cha kushiriki programu ndani kutoka kwenye kichunguzi cha App Bundle kitatoa toleo lililolindwa. Unaweza kuona hali ya ulinzi kwenye kichupo cha Maelezo cha kichunguzi cha App Bundle.

Fuatilia matukio ya kuacha kufanya kazi

Huenda ukagundua ongezeko la matukio ya kuacha kufanya kazi, ambayo ni utendaji wa programu yako inapolindwa; hii inaweza kuashiria kuwa kipengele cha ulinzi otomatiki wa uadilifu kinafanya kazi ipasavyo. Mshambulizi akishindwa kubadilisha programu yako, ukaguzi wa programu inapotumika utazima programu yako, hasa kwa kufanya programu iache kufanya kazi.

Matukio ya kuacha kufanya kazi ambayo hayahusiani na Google Play hayaathiri vipimo vya uthabiti vya Android vitals. Iwapo unatumia zana nyingine kuchanganua matukio ya programu yako kuacha kufanya kazi kama vile Crashlytics na unahitaji jina la kifurushi ili uchuje kulingana na chanzo cha kusakinisha, jina la kifurushi cha Google Play Store huwa "com.android.vending".

Iwapo una hofu kuhusu ongezeko la juu la matukio ya programu kuacha kufanya kazi, unaweza kuyaripoti kwetu kwa kutoa maelezo mengi iwezekanavyo na timu itafanya uchunguzi. Tutashughulikia ripoti yako tukibaini kuwa matukio ya kuacha kufanya kazi yanahusiana na ulinzi.

Ripoti matoleo ya programu yako yaliyokwapuliwa

Toleo lililoshambuliwa ni toleo la programu yako ambalo bado linafanya kazi likiwa limebadilishwa au wakati limesakinishwa nje ya Google Play iwapo unahitaji usakinishaji kupitia Google Play.

Iwapo umetambua toleo lililoshambuliwa la programu yako, unaweza kuliripoti kwetu.

Maudhui yanayohusiana

Je, maelezo haya yamekufaa?

Tunawezaje kuboresha?

Je, unahitaji usaidizi mwingine?

Jaribu hatua zifuatazo:

Tafuta
Futa utafutaji
Funga kisanduku cha kutafutia
Menyu kuu
7231681501455856419
true
Tafuta kwenye Kituo cha Usaidizi
true
true
true
true
true
92637
false
false