Ukijiunga na huduma ya Google Darasani, baadhi ya taarifa zinazokuhusu huonekana kila wakati kwa wanafunzi wengine wa darasa lako. Taarifa binafsi unazoweza kupata kwenye huduma ya Google Darasani hulingana na jukumu lako na hatua zilizochukuliwa na walimu na wasimamizi wa Google Workspace au wa kikoa.
Watumiaji wa Google Workspace: Pata maelezo zaidi kuhusu mipangilio ya shirika lako ya
kutuma anwani.
Ni taarifa gani binafsi ambazo watu wanaweza kupata?
| Mimi ni… |
Nani anaweza kupata nini? |
| Mwanafunzi |
- Walimu kwenye madarasa yako wanaweza kupata anwani ya barua pepe, picha na jina lako.
- Viongozi wa elimu kama vile wakuu wa shule na wasimamizi wa idara wanaweza kupata anwani ya barua pepe, picha na jina lako wakati wanatembelea darasa.
- Wanafunzi wengine katika darasa lako wanaweza kupata picha na jina lako.
- Wanafunzi wengine katika madarasa yako wanaweza kupata anwani yako ya barua pepe katika huduma ya Google Darasani na huduma nyingine za Google, kama vile Hati za Google, Kalenda na Gmail.
- Walezi waliounganishwa na akaunti yako wanaweza kupata picha na jina lako.
- Wasimamizi wa Workspace wanaweza kupata anwani ya barua pepe, picha na jina lako.
|
| Mwalimu |
- Wasimamizi wa Workspace wanaweza kupata anwani ya barua pepe, picha na jina lako.
- Walimu wenza kwenye madarasa yako wanaweza kupata anwani ya barua pepe, picha na jina lako.
- Viongozi wa elimu kama vile wakuu wa shule na wasimamizi wa idara wanaweza kupata anwani ya barua pepe, picha na jina lako wakati wanatembelea darasa.
- Wanafunzi katika madarasa yako wanaweza kupata picha na jina lako.
- Walezi wanaohusishwa na wanafunzi wako wanaweza kupata jina na picha yako.
- Watu unaowaalika kujiunga na darasa lako wanaweza kupata jina na anwani yako ya barua pepe kwenye mwaliko.
- Wanafunzi wanaweza kupata anwani yako ya barua pepe katika huduma ya Google Darasani na huduma nyingine za Google, kama vile Hati za Google, Kalenda na Gmail.
- Ukiruhusu programu za wengine zifikie data ya huduma ya Google Darasani, programu hizo zinaweza kupata maelezo ya mawasiliano.
|
| Mlezi anayehusishwa na mwanafunzi (Google Workspace for Education pekee) |
- Walimu na walimu wenza wanaofunza wanafunzi wako wanaweza kupata jina na anwani yako ya barua pepe.
- Wakitembelea darasa, viongozi wa elimu kama vile wakuu wa shule na wa idara wanaweza kupata picha na anwani yako ya barua pepe.
- Mwanafunzi wako anaweza kupata jina lako.
- Wasimamizi wa Workspace wanaweza kufikia jina, picha na anwani yako ya barua pepe.
|
| Viongozi wa elimu |
- Wakati unachagua sababu za kutembelea darasa, mwalimu wa msingi hupokea barua pepe yenye anwani ya barua pepe, picha na jina lako.
- Ukichapisha, utoe maoni au ujibu wakati unatembelea darasa:
- Wasimamizi wa Workspace, walimu na walimu wenza wanaweza kupata anwani ya barua pepe, picha na jina lako wakati unatembelea na baada ya kutembelea darasa.
- Wanafunzi katika darasa wanaweza kupata picha na jina lako wakati unatembelea na baada ya kutembelea darasa.
- Wazazi na walezi wanaweza kupata jina lako wakati unatembelea na baada ya kutembelea darasa.
- Wakati unawaalika watu wajiunge na darasa, mwaliko huonyesha anwani ya barua pepe na jina lako.
- Msimamizi wako wa Google Workspace akiwasha kipengele cha kutuma anwani, wanafunzi wanaweza kupata anwani yako ya barua pepe katika huduma nyingine za Google, kama vile Hati za Google na Gmail.
- Ukiruhusu programu za wengine zifikie data ya huduma ya Google Darasani, programu hizo zinaweza kufikia maelezo yako ya mawasiliano.
|
Mada zinazohusiana