Makala haya ni ya wanafunzi. Kwa walimu, nendeni hapa.
Hivi ndivyo jinsi ya kurekebisha matatizo unayoweza kukumbana nayo wakati unatumia huduma ya Google Darasani.
Kurekebisha matatizo wakati wa kuingia katika akaunti
Ninashindwa kuingia katika huduma ya Google Darasani- Akaunti ya shuleni—Pia inajulikana kama akaunti ya Google Workspace for Education, akaunti hii hufunguliwa na shule iliyoidhinishwa. Inaonekana kama "yourname@yourschool.edu."
- Akaunti Binafsi ya Google—Akaunti hii hufunguliwa na wewe, mzazi au mlezi wako. Kwa kawaida, unatumia Akaunti ya Google ya binafsi nje ya eneo la shule, kama vile katika masomo ya nyumbani. Inaonekana kama you@example.com.
- Akaunti ya Google Workspace—Akaunti hii hufunguliwa na msimamizi wa shirika lako. Inaonekana kama "you@yourcompany.com."
- Sharti uwe na muunganisho wa intaneti unaotumika ili uingie katika akaunti yako.
- Iwapo huwezi kuingia ukitumia akaunti ya barua pepe na nenosiri sahihi, huenda msimamizi wa shule yako huwa hawashi kiotomatiki huduma ya Google Darasani kwa wanafunzi na watumiaji wapya. Ili upate usaidizi zaidi, wasiliana na mwalimu wako.
-
Ikiwa shule yako inatumia Google Workspace for Education—Mwombe mwalimu wako awasiliane na msimamizi ili abadilishe nenosiri lako.
-
Ikiwa wewe ni mwanafunzi anayetumia Akaunti ya Google ya binafsi nje ya shule, pata maelezo kuhusu jinsi ya kubadilisha nenosiri lako.
Kurekebisha matatizo wakati wa kujiunga na darasa
Msimbo wa darasa langu haufanyi kaziIwapo msimbo wa darasa haufanyi kazi, hakikisha kuwa:
- Umeingia katika huduma ya Google Darasani ukitumia akaunti sahihi. Pata maelezo kuhusu jinsi ya kuingia katika huduma ya Google Darasani.
- Msimbo unaoweka una urefu wa herufi 6 hadi 8 na unatumia herufi na namba. Misimbo haupaswi kuwa na nafasi au kutumia herufi maalum.
- Mfano:
- Huu ni mfano. Usitumie msimbo huu.
- Mfano:
- Umeweka msimbo kwa usahihi. Unajumuisha herufi zozote kubwa au maalum.
- Iwapo una uhakika kuwa umeweka msimbo kwa usahihi, wasiliana na mwalimu wako kwa sababu kunaweza kuwa na tatizo la kiufundi.
Iwapo bado unatatizika, mfahamishe mwalimu wako.
Kidokezo: Unatumia msimbo wa darasa mara moja tu ili kujiandikisha. Ukishajiunga, huhitaji kutumia msimbo tena.
- Ili ujiunge na darasa, unahitaji tu kuweka msimbo wa darasa mara moja. Ukishajiunga, huhitaji kuweka msimbo tena.
- Iwapo utasahau, kupoteza au kufuta msimbo kabla ya kujiunga na darasa, mwombe mwalimu wako akutumie.
- Kuwasiliana na mwalimu wako: Njia rahisi ya kupata msimbo wa darasa lako ni kumwomba mwalimu wako moja kwa moja.
- Kuangalia barua pepe yako: Mwalimu wako anaweza kutuma msimbo wa darasa kwenye barua pepe. Angalia kikasha na folda yako ya taka.
Ukipoteza mwaliko wako kabla ya kujiunga na darasa, mwombe mwalimu wako akutumie tena.
Kidokezo: Unatumia mwaliko wa darasa mara moja tu kujiandikisha.- Iwapo shule yako inatumia Google Workspace for Education: Wanafunzi hawawezi kuanzisha madarasa.
- Ikiwa wewe ni mwanafunzi aliye na Akaunti ya Google ya binafsi nje ya shule: Pata maelezo kuhusu jinsi ya kuanzisha darasa.
Kurekebisha matatizo yanayohusiana na barua pepe
Siwezi kutuma wala kupokea barua pepe- Iwapo shule yako inatumia Google Workspace for Education – huenda msimamizi wa shule yako amezima Gmail kwa wanafunzi. Mwombe mwalimu wako awasiliane na msimamizi.
- Ikiwa wewe ni mwanafunzi anayetumia Akaunti ya Google ya binafsi nje ya shule – nenda kwenye Kituo cha Usaidizi cha Gmail.
Kurekebisha matatizo yanayohusiana na mazoezi
Kitufe cha Kuwasilisha hakifanyi kaziIwapo utapokea ujumbe kuhusu hitilafu wakati umebofya Wasilisha, mfahamishe mwalimu wako.
Iwapo huwezi kuwasilisha kiambatisho ulichokabidhiwa, jaribu hatua hizi:
- Ili uhifadhi kazi yoyote uliyofanya kwenye kiambatisho, nakili na ubandike kazi yako kwenye hati isio na chochote.
- Katika zoezi katika huduma ya Google Darasani, kwenye kiambatisho, bofya Ondoa
Tayarisha nakala.
- Bofya kiambatisho kipya.
- Bandika kazi yoyote uliyohifadhi kwenye faili mpya.
- Bofya Wasilisha.
- Mfahamishe mwalimu wako ikiwa hutapata kiambatisho alichokukabidhi.
- Ili upate maelezo kuhusu viambatisho ulivyokabidhiwa, nenda katika sehemu ya kuwasilisha zoezi.
Ukipata ujumbe kuhusu hitilafu wa "Imeshindwa kuambatisha faili" wakati unawasilisha zoezi, jaribu njia hizi tofauti badala yake:
- Ambatisha faili kwenye Mkondo, kisha ubandike kiungo katika zoezi.
- Fungua folda ya Kazi ya darasani, pakia faili yako kwenye Hifadhi ya Darasa, kisha utume faili katika kikundi cha darasa.
- Pakia tena faili sawa kama nakala tofauti, kisha uambatishe faili kwenye darasa.
Kurekebisha mipangilio ya darasa
Ninaweza kubadilisha vipi lugha katika huduma ya Google Darasani?
Unabadilisha lugha unayopendelea kwenye Akaunti yako ya Google. Ili upate maelezo kuhusu jinsi ya kubadilisha lugha kwenye kompyuta na vifaa vya mkononi, nenda katika sehemu ya kubadilisha lugha yako kwenye wavuti.
Nyenzo zinazohusiana
- Ninaweza kuingia vipi katika huduma ya Google Darasani?
- Kupakua programu ya Google Darasani
- Kupokea barua pepe za mihtasari za huduma ya Google Darasani (kwa walezi)
- Kujiunga na darasa kwa kutumia kiungo cha darasa katika huduma ya Google Darasani
- Kujiunga na darasa kwa kutumia msimbo wa darasa katika huduma ya Google Darasani
- Kujiunga na darasa katika huduma ya Google Darasani kwa kutumia mwaliko uliotumwa kupitia barua pepe
Google, Google Workspace, and related marks and logos are trademarks of Google LLC. All other company and product names are trademarks of the companies with which they are associated.