Kurekebisha hitilafu za kupakua faili

Iwapo umepata ujumbe kuhusu hitilafu kwenye Chrome unapojaribu kupakua programu, mandhari, viendelezi au faili nyinginezo, jaribu hatua hizi za urekebishaji.

Kurekebisha hitilafu nyingi za upakuaji wa faili

Ukijaribu kupakua faili bila kufanikiwa, jaribu kwanza kurekebisha hitilafu hiyo kupitia hatua hizi za utatuzi:

  1. Hakikisha muunganisho wako wa intaneti unafanya kazi kama kawaida. Ikiwa muunganisho wako wa intaneti si thabiti, pata maelezo kuhusu jinsi ya kurekebisha hitilafu za muunganisho.
    • Chrome itaendeleza upakuaji kiotomatiki.
    • Unaweza pia kuendeleza upakuaji mwenyewe. Bofya sehemu ya Upakuaji unaendelea , elekeza kiteuzi kwenye jina la faili iliyositishwa kupakuliwa, kisha ubofye Endelea .
  2. Jaribu kupakua faili baadaye.
  3. Wasiliana na mmiliki wa tovuti.

Ili kukusaidia kupata faili uliyopakua, pata maelezo kuhusu jinsi ya kuangalia faili iliyopakuliwa.

Kupata usaidizi wa kushughulikia ujumbe mahususi kuhusu hitilafu

"Hitilafu ya mtandao"

Ukiona "NETWORK_FAILED" unapojaribu kusakinisha kitu kutoka katika Duka la Chrome kwenye Wavuti, huenda programu isiyotakikana inazuia usakinishaji.

Ili urekebishe hitilafu:

"Kipakuliwa kimezuiwa"

Hitilafu hii inamaanisha kuwa mipangilio ya usalama ya kompyuta yako imezuia faili.

Pata maelezo zaidi kuhusu vipakuliwa vilivyozuiwa.

Kwenye Windows: huenda Kidhibiti cha Viambatisho cha Windows kiliondoa faili uliyojaribu kupakua. Ili uone ni faili gani unazoweza kupakua au sababu ya faili yako kuzuiwa, angalia mipangilio yako ya usalama wa intaneti ya Windows.

"Hakuna faili" au "Faili haipo"

Hitilafu hii inamaanisha kuwa unajaribu kupakua faili ambayo haipo kwenye tovuti hii au imehamishiwa kwenye sehemu nyingine ya tovuti.

Ili urekebishe hitilafu, wasiliana na mmiliki wa tovuti au ujaribu kutafuta faili kwenye tovuti tofauti.

"Imeshindwa kukagua virusi" au "Imepata virusi"

Hitilafu hizi zinamaanisha kuwa huenda programu yako ya kukagua virusi imekuzuia usipakue faili.

  • Angalia programu yako ya kukagua virusi ili upate maelezo kuhusu sababu ya faili kuzuiwa.
  • Kwenye Windows: huenda Kidhibiti cha Viambatisho cha Windows kiliondoa faili uliyojaribu kupakua. Ili uone ni faili gani unazoweza kupakua au sababu ya faili yako kuzuiwa, angalia mipangilio yako ya usalama wa intaneti ya Windows.
"Diski imejaa"

Hitilafu hii inamaanisha kuwa hakuna nafasi inayotosha kupakua faili kwenye kompyuta yako.

Ili urekebishe hitilafu:

  • Futa baadhi ya faili kwenye kompyuta yako
  • Safisha Tupio lako
"Ruhusa hazitoshi" au "Mfumo unatumika"

Hitilafu hizi zinamaanisha kuwa Chrome imeshindwa kuhifadhi faili kwenye kompyuta yako.

Ili urekebishe hitilafu:

  • Ghairi upakuaji kisha ujaribu tena.
  • Badala ya kubofya faili ili uipakue, bofya kulia kwenye kiungo kisha uchague Hifadhi kiungo kama.
  • Hakikisha umepakua faili kwenye sehemu ya kompyuta yako unayoweza kuifikia, kama vile Eneo-kazi au folda yako ya Hati. Unaweza kubadilisha mahali pa kuhifadhi faili zilizopakuliwa.
“Unahitaji idhini”

Hitilafu hii inamaanisha kuwa huna ruhusa ya kupakua faili.

Ili urekebishe hitilafu, wasiliana na mmiliki wa tovuti au seva au ujaribu kutafuta faili kwenye tovuti tofauti.

"Huruhusiwi" au "Imeshindwa kupakua - Huruhusiwi"

Hitilafu hii inamaanisha huna ruhusa ya kupakua faili kutoka kwenye seva.

Ili urekebishe, nenda kwenye tovuti ambapo faili imepangishwa. Angalia iwapo unatakiwa kuingia katika akaunti (au kutoa uthibitishaji mwingine). Iwapo huwezi kuingia katika akaunti, wasiliana na mmiliki wa tovuti au seva au ujaribu kutafuta faili kwenye tovuti tofauti.

Bado hujafanikiwa? Pata usaidizi zaidi kwenye Chrome Help Forum.

Tafuta
Futa utafutaji
Funga kisanduku cha kutafutia
Menyu kuu
7362127321049976417
true
Tafuta kwenye Kituo cha Usaidizi
true
true
true
true
true
237
false
false