Fahamu ripoti yako ya kabla ya jaribio

Makala haya yanakusaidia uelewe matokeo ya ripoti yako ya kabla ya jaribio kwa kukupa muhtasari wa hitilafu, maonyo au matatizo ambayo yanaweza kutambuliwa na ripoti yako. Iwapo ungependa kujua jinsi ya kuweka na kutekeleza ripoti ya kabla ya jaribio, nenda kwenye Tumia ripoti ya kabla ya jaribio kubaini matatizo.

Wakati ripoti yako ya kabla ya jaribio inapatikana, unaweza kuona muhtasari wa jaribio ambao unaonyesha idadi ya hitilafu, maonyo na matatizo madogo yanayopatikana wakati wa kujaribu, yakiwa yamepangwa kulingana na aina ya tatizo. Utaona pia pendekezo kulingana na matokeo ya jaribio la programu yako.

Kumbuka: Ingawa ripoti ya kabla ya jaribio ni zana halisi na thabiti ambayo inaweza kukusaidia uboreshe programu yako, Google haiwezi kukuhakikishia kuwa majaribio yatabaini matatizo yote. Ili kuhakikisha kuwa matokeo yako ni ya kina na yanayokufaa iwezekanavyo, kagua na usasishe mipangilio ya ripoti yako ya kabla ya jaribio.

Muhtasari wa ripoti yako ya kabla ya jaribio

Ukurasa wa Muhtasari wa ripoti ya kabla ya jaribio huonyesha muhtasari wa hitilafu, maonyo na matatizo yoyote madogo mahususi yanayopatikana wakati wa kujaribu, yakiwa yamepangwa katika aina nne: Uthabiti, Utendaji, Ufikivu, na Usalama na uaminifu. Aina hizi zimefafanuliwa kwa kina hapo chini.

Pia, utaona idadi ya vifaa ambako programu yako ilijaribiwa, na kulingana na matokeo ya jaribio, maarifa na mapendekezo yanayoweza kukusaidia uboreshe programu yako.

Ifuatayo ni mifano michache ya matatizo yanayopatikana wakati wa jaribio:

  • Hitilafu: Hujumuisha matukio ya kuacha kufanya kazi, ANR, matumizi ya maktaba zenye hitilafu, na API zisizotumika ambazo zimezuiwa.
  • Tahadhari: Hujumuisha matukio ya kufungua na kupakia polepole, matatizo ya kutambaa au kuingia katika akaunti, matatizo ya hifadhi, utumiaji wa API zisizotumika ambazo bado hazijazuiwa.
  • Matatizo madogo: Hujumuisha kukosekana kwa lebo za maudhui, matatizo ya utofautishaji wa rangi, ukubwa wa sehemu ndogo ya kugusa kwenye skrini lengwa, matatizo ya utekelezaji.

 

Kunja Zote Panua Zote

Maelezo ya ripoti yako ya kabla ya jaribio

Uthabiti

Kila sehemu ya kichupo cha Uthabiti hufafanua matatizo yanayopatikana wakati wa kujaribu, ambayo yanaweza kujumuisha:

  • Aina na aikoni ya tatizo:
    • Nyekundu huashiria hitilafu
    • Manjano huashiria onyo
    • Kijani huashiria kuwa mchakato wa kujaribu haukupata matatizo yoyote
  • Idadi ya vifaa ambako tatizo lilipatikana
  • Ufuatiliaji wa rafu unaohusiana na tatizo
  • API inayofaa (ikiwa inatumika)
  • Mara ambazo tatizo lilitambuliwa wakati wa kujaribu (panapotumika)

Karibu na kila tatizo, unaweza kuchagua Onyesha zaidi ili upate maelezo ya kina kuhusu tatizo, kama vile jina la kifaa, ukubwa wa skrini, toleo la Android, RAM, kiolesura cha mfumo wa jozi ya programu (ABI) na lugha. Unaweza kuchagua kila muundo wa kifaa ili uone vipimo vya kifaa, kijipicha na video kutoka kwa jaribio, data ya maonyesho yanayojirudia na ufuatiliaji wa rafu (ambayo unaweza pia kupakua). Fahamu kuwa upatikanaji wa maelezo haya unaweza kutofautiana.

Kumbuka: Kwa kuwa matukio ya programu kuacha kufanya kazi yaliyopatikana wakati wa kutayarisha ripoti ya kabla ya uzinduzi yanatokana na vifaa vya jaribio, hayaathiri takwimu zako za matukio ya programu kuacha kufanya kazi.

Angalia vifaa vya kujaribu visivyo na matatizo

Chini ya kichupo cha Uthabiti, unaweza kuona jedwali la Vifaa vya kujaribu visivyo na matatizo ili uone maelezo kuhusu majaribio ambayo hayakupata matatizo yoyote. 

Kwa kila safu mlalo, utaona jina la kifaa kilichojaribu, toleo la Android la kifaa na aikoni inayoonyesha iwapo programu yako ilikumbwa na matatizo yoyote ya majaribio.

Uthabiti: Uoanifu kwenye Android

Iwapo progamu yako inatumia kiolesura kimoja au zaidi ambacho hakipatikani kwenye Android SDK ya umma (inajulikana mara nyingi kama “haitumiki” au “violesura visivyo vya SDK”), utaona hitilafu na maonyo yaliyoorodheshwa kwenye vichupo vya ripoti za kabla ya jaribio vya Muhtasari na Uthabiti.

Angalia matatizo mahususi

Ili kubaini violesura visivyotumika ambavyo vimewekwa, bofya viungo vya 'Angalia matatizo' vilivyo karibu na hitilafu na maonyo ya “Uoanifu wa Mfumo wa Uendeshaji” katika ripoti yako ya kabla ya jaribio. Ili kuona mahali ambapo kiolesura mahususi kimetumika katika programu yako, bofya kishale cha chini kilicho karibu nacho ili uone ufuatiliaji wa rafu. Kiolesura kimoja kinaweza kutumika mara nyingi katika jaribio moja.

Violesura visivyotumika vinawekwa katika makundi kulingana na kiwango cha athari. Ili kuepuka matatizo ya uthabiti, ni vizuri uache kutumia violesura visivyotumika kabisa, lakini unaweza kutumia makundi ili kukusaidia kuyapa kipaumbele matatizo unayoweza kuyashughulikia kwanza.

Ufuatao ni mpangilio unaopendekezwa wa kuweka kipaumbele:

  1. Vilivyozuiwa: Violesura vitakavyoacha kufanya kazi kwenye baadhi ya matoleo au matoleo yote ya Android.
  2. Visivyotumika lakini vinatarajiwa kuzuiwa: Violesura ambavyo hatutoi hakikisho kuwa vitafanya kazi na vitazuiwa kwenye matoleo yajayo.
  3. Visivyotumika, havitarajiwi kuzuiwa: Violesura ambavyo hatutoi hakikisho kuwa vitafanya kazi.

Kumbuka: Katika kila aina, violesura hupangwa kulingana na mara ambazo vinapatikana, hali inayoweza pia kukusaidia kuyapa kipaumbele masuala ambayo utashughulikia kwanza.

Utendaji

Kwa kila muundo wa kifaa, muhtasari wa jaribio la utendaji huwa na vipimo vifuatavyo:

Kumbuka: Huenda vifaa vya kufanyia majaribio vinavyotumia matoleo ya awali ya Android visizalishe data ya utendaji.

Angalia ripoti mahususi

Chagua kila muundo wa kifaa ili uone vipimo vya kifaa, takwimu za utendaji, utendaji baada ya muda fulani, na uone kijipicha na video kutoka kwa jaribio. Unaweza pia kuona grafu na rekodi ya kila takwimu iliyowekwa katika muda wote wa jaribio. 

Kwa mfano, unaweza kuangalia asilimia ya CPU ya programu yako jaribio linapoendelea. Kama utaona ongezeko la haraka la asilimia ya CPU, kagua hatua ambayo programu ya kutambaa imechukua ili ikusaidie kutatua tatizo hilo.

Kumbuka kuwa upatikanaji wa maelezo haya unaweza kutofautiana.

Ufikivu

Kila muhtasari wa jaribio la ufikivu unajumuisha idadi ya hitilafu, maonyo na matatizo madogo ya ufikivu yanayopatikana wakati wa kujaribu, yakiwa yametenganishwa katika aina zifuatazo:

Angalia ripoti kulingana na aina

Unaweza kusogeza chini ya muhtasari ulio juu ya kichupo cha Ufikivu ili uone sehemu zilizoainishwa zenye makundi ya skrini ambayo hutambua mahali ambapo matatizo ya ufikivu yamepatikana kwenye programu yako.

  • Kama matatizo yoyote yamebainishwa, utaona aikoni ya rangi nyekundu.
  • Kama maonyo yoyote yamebainishwa, utaona aikoni ya manjano.
  • Kama matatizo yoyote madogo yamebainishwa, utaona aikoni ya samawati.
  • Kama hakuna matatizo yaliyobainishwa, utaona alama ya kuteua ya rangi ya kijani.

Angalia matatizo mahususi

Unaweza kuchagua kundi la skrini ili uone mfano wa picha za skrini zinazowiana na majina ya muundo wa kifaa, mfumo wa uendeshaji, ukubwa wa skrini, uzito wa skrini na lugha pamoja na pendekezo linalotolewa.

Boresha ufikivu wa programu yako

Picha za skrini

Muhtasari wako wa jaribio la picha za skrini huonyesha: 

  • Picha zinazoonyesha jinsi programu yako inavyoonekana kwenye vifaa vya majaribio katika lugha mbalimbali.
  • Metadata kuhusu vifaa vilivyojaribiwa (ikiwa ni pamoja na jina la muundo, toleo la Android, lugha, ubora wa skrini na DPI).
  • Idadi ya vifaa vilivyo na picha za skrini.
  • Idadi ya vifaa ambavyo havikuweza kujaribiwa na Android App Bundle yako:
    • Vifaa havipatikana: App Bundle yako inaoana na vifaa hivi lakini tatizo lilitokea wakati wa majaribio. Ikiwa jaribio lako lilikuwa na vifaa vyovyote ambavyo havikupatikana, unaweza kuamua kupakia App Bundle nyingine kisha ujaribu tena.
    • Vifaa havioani: App Bundle yako haioani na vifaa fulani vya majaribio. Ukijaribu tena, hutapokea matokeo ya vifaa vyovyote visivyooana.

Kumbuka: Iwapo unafanya jaribio kwa kutumia maonyesho yanayojirudia, hutaona data yoyote kwenye kichupo cha Picha za Skrini.

Njia za kuangalia picha za skrini

Unaweza kupanga matokeo ya jaribio la picha za skrini ukitumia kiteua cha Panga kulingana na karibu na kichupo cha juu kulia cha Picha za Skrini. Kuna njia mbili za kupanga picha zako za skrini:

  • Makundi ya skrini: Chagua Makundi ya skrini ili uone jinsi picha zinazofanana huonekana kwenye vifaa mbalimbali. Katika mwonekano huu, ripoti ya kabla ya jaribio hupanga picha pamoja kulingana na vipengele au wijeti kwenye skrini. Makundi ya skrini huchaguliwa kwa chaguomsingi.
  • Vifaa: Chagua Vifaa ili uone picha zote za skrini zinazohusiana na kifaa mahususi. Katika mwonekano huu, unaweza kuona picha za skrini zikiwa zimepangwa kulingana na wakati zilizopigwa kwenye jaribio.

Unaweza kuchagua picha ya skrini ili uone vipimo na maelezo ya ziada ya kifaa.

Mapendeleo ya lugha

Ili uone picha za skrini katika lugha mahususi, unaweza kuweka mapendeleo ya lugha katika kichupo cha Mipangilio.

Usalama na uaminifu

Kila muhtasari wa jaribio unajumuisha jina na ufafanuzi wa athari zozote za usalama zinazopatikana kwenye App Bundle yako.

Kumbuka: Tunapendekeza uchukue hatua kuhusu athari zozote za kiusalama zilizoorodheshwa kabla ya kuchapisha yako kuwa toleo la umma.

Fanya jaribio maalum ukitumia Maabara ya Majaribio ya Firebase

Ikiwa programu au mchezo wako unahitaji jaribio lingine maalum, unaweza kutumia Maabara ya Majaribio ya Firebase. Baada ya kuanzisha mradi wako wa Firebase, unaweza kuchagua aina ya kifaa chako kutoka kwenye orodha ndefu ya vifaa na mbinu za kujaribu ili ufanye majaribio maalum. Kisha, unaweza kutekeleza na kuona matokeo ya jaribio maalum katika dashibodi ya Firebase. Vipimo 5 hadi 15 vya mwanzo utakavyotekeleza kwa siku havilipishwi.

Maudhui yanayohusiana

  • Pata maelezo zaidi kwenye Chuo cha Google Play kuhusu jinsi ya kutumia ripoti ya kabla ya uzinduzi kubaini matatizo.

Je, maelezo haya yamekufaa?

Tunawezaje kuboresha?

Je, unahitaji usaidizi mwingine?

Jaribu hatua zifuatazo:

Tafuta
Futa utafutaji
Funga kisanduku cha kutafutia
Menyu kuu
15445191154118182195
true
Tafuta kwenye Kituo cha Usaidizi
true
true
true
true
true
92637
false
false