Tunawaletea Vituo Rasmi vya Msanii

Ikiwa wewe ni msanii kwenye YouTube, Kituo chako Rasmi cha Msanii ("OAC") huleta pamoja maudhui na wote wanaofuatilia kituo chako kutoka kwenye vituo vyako tofauti vya YouTube katika sehemu moja. Utapata pia idhini ya kufikia kifurushi cha zana zilizoundwa kwa ajili ya wasanii, ikiwa ni pamoja na Takwimu za Wasanii.

Vipengele vya Kituo Rasmi cha Msanii

Mashabiki wako wote hukusanyika kwenye Kituo chako Rasmi cha Msanii

Unapopata Kituo Rasmi cha Msanii, huwa tunaunganisha wanaofuatilia kwenye kituo chako otomatiki cha msanii, kituo cha Vevo (ikiwa kipo) na kituo chako kilichopo na kuwaweka kwenye kituo chako kipya. Kitufe cha kufuatilia na idadi ya wanaofuatilia haitaonyeshwa kwenye kituo chako kilichopo au kituo otomatiki cha msanii.

Huenda ukaona ongezeko la idadi ya wanaofuatilia Kituo chako Rasmi cha Msanii tunavyokusanya pamoja hadhira yako.

Wanaofuatilia kituo chako watatazama video zako mpya za muziki bila kujali ikiwa wanafuatilia Kituo chako Rasmi cha Msanii au vituo vyako vingine. Kuunganisha huku kunapaswa kukusaidia kukuza na kusambaza muziki mpya kwa njia bora zaidi.

Vipengele vingine vinavyopatikana kwenye Kituo chako Rasmi cha Msanii (OAC) ni pamoja na Vipengele vya Tiketi, Bidhaa, na Takwimu za Wasanii.

Kidokezo: Ukiwa na hadhira iliyounganishwa, tumia nafasi hii kuwasiliana na mashabiki wako kwa kutumia Machapisho ya jumuiya, Kuweka emoji za moyo kwenye maoni na Mitiririko mubashara.

Vigezo na masharti ya kujiunga kwenye programu

Ili utimize vigezo vya kupata Kituo Rasmi cha Msanii (OAC), unahitaji kutimiza masharti yafuatayo:

  • Kumiliki na kuendesha kituo cha YouTube cha msanii mmoja au bendi kinachoangazia muziki wa msanii au bendi husika.
  • Uwe na angalau muziki 1 rasmi kwenye YouTube uliotolewa na kusambazwa na Msambazaji wa Muziki au Lebo
  • Kituo chako kiwe kinatii sera zote za YouTube ikiwa ni pamoja na Mwongozo wa Jumuiya ya YouTube, Sheria na Masharti na sera za Hakimiliki

Na angalau mojawapo ya yafuatayo:

  • Uwe unafanya kazi na Msimamizi wa Washirika wa YouTube
  • Uwe sehemu ya Mpango wa Washirika wa YouTube ("YPP")
  • Uwe sehemu ya mtandao wa lebo unaofanya kazi na Msimamizi wa Washirika
  • Muziki wako uwe unasambazwa na mshirika wa muziki aliyeorodheshwa katika Orodha ya Kampuni zenye Vyeti za YouTube kwa ajili ya Washirika wa Muziki.

Jinsi ya Kutuma Ombi la kupata Kituo Rasmi cha Msanii

Tafadhali wasiliana na lebo au msambazaji wako ili uombe kupata Kituo Rasmi cha Msanii. Ikiwa huna lebo au msambazaji, tafadhali wasiliana na Mshirika wa Huduma ya Muziki ambaye anaweza kuomba Kituo Rasmi cha Msanii kwa niaba yako. Unaweza kupata orodha ya Washirika wetu wa Huduma ya Muziki katika Orodha ya Kampuni zenye Vyeti kwenye YouTube. Washirika wa Huduma ya Muziki wanaweza kuomba Kituo Rasmi cha Msanii kwa niaba yako kama sehemu ya kuwasilisha maudhui ya muziki wako kwenye YouTube.

Sera na Mipango ya Kituo Rasmi cha Msanii

Sera na Mipango ya Kituo Rasmi cha Msanii

Iwapo una Kituo Rasmi cha Msanii kwenye YouTube, ni muhimu ufuate Mwongozo wa Jumuiya ya YouTube.

Kituo chako Rasmi cha Msanii kitasimamishwa na kufanywa kituo cha kawaida kikipokea onyo kwa kukiuka Mwongozo wa Jumuiya au kiwe na maudhui yenye vipengele vichache. Kituo chako kitarejeshwa kiotomatiki kuwa Kituo Rasmi cha Msanii ikiwa na wakati kituo chako hakitakuwa na maonyo kwa kukiuka Mwongozo wa Jumuiya au maudhui yenye vipengele vichache na kiwe kinatimiza vigezo vingine vyote vya mpango vilivyoorodheshwa hapo juu.

Msanii Anayechipukia

YouTube ni mahali ambapo ubinafsi hustawi, utofauti hushamiri na aina au miundo mipya ya maudhui hugunduliwa.

Tunawaangazia watayarishi na wasanii "Wanaochipuka" katika sehemu mpya ya Kichupo chetu cha Zinazovuma. 

Pata maelezo zaidi kwenye Kituo chetu cha Usaidizi kwa Wasanii Wanaochipukia.

Je, maelezo haya yamekufaa?

Tunawezaje kuboresha?
Tafuta
Futa utafutaji
Funga kisanduku cha kutafutia
Menyu kuu
1819351289598946953
true
Tafuta kwenye Kituo cha Usaidizi
true
true
true
true
true
59
false
false