Sera za kisheria

Chapa ya biashara

Si lazima uwe umekiuka sheria iwapo utatumia chapa ya biashara ya mtu mwingine katika jina la mtumiaji, lebo au mada ya video yako. Hata hivyo, iwapo kuna maudhui kwenye wasifu au video yako ambayo yanaweza kuwakanganya watazamaji waamini kuwa mmiliki wa chapa ya biashara alibuni au kufadhili ukurasa au maudhui yako, basi utakuwa umekiuka haki za mmiliki wa chapa ya biashara. Katika hali hizi, tunaweza kuondoa maudhui husika, kwa hivyo ni muhimu uzingatie haki za chapa ya biashara ya watu wengine wakati unachagua jina la mtumiaji au kuweka metadata kwenye video zako.

Iwapo wewe ni mmiliki wa chapa ya biashara na unaamini kuwa haki yako ya chapa ya biashara inakiukwa, tafadhali kumbuka kuwa YouTube haipo katika nafasi ya kusuluhisha mizozo ya chapa ya biashara kati ya watayarishi na wamiliki wa chapa za biashara. Kwa hivyo, tunawahimiza wamiliki wa chapa za biashara wasuluhishe mizozo yao moja kwa moja na mtayarishi aliyechapisha maudhui husika. Hatua ya kuwasiliana na aliyepakia inaweza kusaidia kusuluhisha dai lako kwa haraka. Wamiliki wa chapa za biashara wanaweza kuwasiliana na mtayarishi au kutuma malalamiko moja kwa moja kwa aliyepakia kupitia fomu yetu ya Malalamiko Kuhusu Chapa ya Biashara.

Baadhi ya watayarishi huorodhesha njia unazoweza kuwasiliana nao katika chaneli yao.

Iwapo wewe na mmiliki wa akaunti husika hampati suluhisho, tafadhali tuma dai la chapa ya biashara kupitia fomu yetu ya Malalamiko Kuhusu Chapa ya Biashara. YouTube iko tayari kufanya uchunguzi mdogo kuhusu malalamiko husika na itaondoa maudhui katika hali za ukiukaji wa wazi.

Kukashifu

Iwapo wewe au mwakilishi wako wa kisheria mnaamini kuwa maudhui yaliyopangishwa kwenye YouTube yanakashifu, tafadhali fungua fomu yetu ya wavuti mtandaoni, ambako unaweza kuwasilisha malalamiko.

Bandia

Google inakataza uuzaji au ukwezaji wa bidhaa bandia katika bidhaa zake, ikiwa ni pamoja na YouTube. Bidhaa bandia zina chapa za biashara au nembo ambayo inafanana na au ambayo ni vigumu kutofautisha na chapa ya biashara nyingine. Bidhaa hizo huiga vipengele vya chapa vya bidhaa katika jaribio la kuzifanya zionekane kama bidhaa halisi za mmiliki wa nembo, au hukweza bidhaa kama mfanano, mifano, uigaji, au kloni za bidhaa asili.

Kuripoti bidhaa bandia:

Iwapo unaamini kuwa maoni au video ya YouTube inauza au kutangaza bidhaa bandia, unaweza kuwasilisha malalamiko kuhusu bidhaa bandia kupitia fomu yetu ya wavuti. Timu yetu itachunguza malalamiko yako na kuondoa maudhui iwapo yatakiuka sera ya Google dhidi ya bidhaa bandia.

Je, maelezo haya yamekufaa?

Tunawezaje kuboresha?
false
Tafuta
Futa utafutaji
Funga kisanduku cha kutafutia
Menyu kuu
15759803470797443854
true
Tafuta kwenye Kituo cha Usaidizi
true
true
true
true
true
59
false
false