YouTube Kids ilibuniwa kuwa eneo la kufana, linalofaa familia na watoto. Programu ya YouTube Kids ina video maarufu za watoto na maudhui mengi mapya, yanayowasilishwa kwa njia ambayo ni rahisi kwa watoto kutumia.
Kabla ya mtoto wako kuanza kutumia programu, kuna mambo machache ambayo tungependa kuhakikisha kuwa unaelewa:
Wasifu wa YouTube Kids
YouTube Kids huruhusu wazazi ambao wameingia katika akaunti watengeneze wasifu tofauti kwa kila mtoto katika familia zao. Kila wasifu una mipangilio tofauti ya mapendeleo na mapendekezo ya kuangalia, hali inayoruhusu watoto wengi wanufaike zaidi kwenye programu ya YouTube Kids.
Wasifu hupatikana kwenye vifaa ambako:
- Mzazi ameingia katika akaunti, na
- Programu ya YouTube Kids imesakinishwa.
Unaweza kuwa na hadi wasifu nane. Pata maelezo kuhusu jinsi ya kutengeneza wasifu.
Kumbuka: Unaweza pia kutumia YouTube Kids bila kuingia katika akaunti.
Video zinazopatikana kwenye YouTube Kids huchaguliwa vipi?
Chaguo moja ni kuruhusu mtoto wako agundue video zote kwenye YouTube Kids. Wazazi wanaweza kuchagua kutoka kwenye mipangilio mitatu ya maudhui kulingana na umri:
- Watoto wa Chekechea (Umri usiozidi miaka minne)
- Watoto Wadogo (Umri wa miaka mitano hadi minane)
- Watoto Wakubwa (Umri wa miaka tisa hadi 12)
Mifumo yetu ya kiotomatiki huchagua maudhui kutoka video mbalimbali kwenye YouTube. Tunajitahidi kutenga maudhui ambayo hayafai watoto. Lakini hatuwezi kukagua video zote wenyewe na hakuna mfumo wa kiotomatiki ambao ni sahihi kikamilifu. Iwapo utapata maudhui yoyote yasiyofaa, unaweza kuyazuia au kuyaripoti ili tuyakague haraka.
Chaguo lingine ni kuchagua mwenyewe maudhui ambayo mtoto wako anaweza kufikia (Idhinisha Maudhui Mwenyewe). Ukiteua chaguo hili, mtoto wako hataweza kutafuta. Kwa maelezo zaidi kuhusu jinsi ya kutekeleza chaguo hili, rejelea mwongozo wa YouTube Kids kuhusu mipangilio na vidhibiti vya wazazi.
Teua chaguo ambalo unafikiri kuwa linafaa zaidi mtoto wako. Unaweza kubadilisha mipangilio hii wakati wowote. Tunatoa pia zana na mipangilio mbalimbali, inayofafanuliwa hapa chini, ambayo unaweza kutumia kudhibiti zaidi hali ya utumiaji wa mtoto wako. Pata maelezo zaidi kuhusu mipangilio na vidhibiti vya wazazi.
Mtoto hugundua vipi video kwenye YouTube Kids?
Video kwenye YouTube Kids zinaweza kugunduliwa kwa njia kadhaa:
Tafuta
Unapowasha
Utafutaji , unaruhusu mtoto wako apate na kutazama mamilioni ya video zinazopatikana kwenye YouTube Kids. Video hizi huchaguliwa na algoriti maalum iliyobuniwa kuonyesha matokeo yanayofaa.
Lakini video zinazopatikana kupitia Utafutaji, hazitegemei uhakiki unaofanywa na binadamu. YouTube hushughulikia maudhui mengi ya aina mbalimbali. Kwa hivyo, tunapojitahidi kuhakikisha kuwa kila kitu kiko sawa, mtoto wako anaweza kupata maudhui ambayo hungependa atazame.
Iwapo ungependa kudhibiti video ambazo mtoto wako anatazama ili ziwe na maudhui mahususi zaidi, unaweza
kuzima Utafutaji kwa kutumia vidhibiti vya wazazi. Kwa kuzima utafutaji, mtoto wako atakuwa tu na uwezo wa kufikia vituo ambavyo vimethibitishwa na YouTube Kids. Kumbuka, bila kujali hali ya
Utafutaji katika programu yako, bado kuna uwezekano kuwa mtoto wako atapata maudhui ambayo hungependa ayatazame.
Kumbuka: Unapozima Utafutaji, historia ya Video ulizotazama na Mambo uliyotafuta itafutwa, pamoja na orodha ya video Zinazopendekezwa na zilizo katika sehemu ya Itazame tena.
Mbali na kuzima Utafutaji, YouTube Kids ina vidhibiti zaidi vya wazazi vya kukusaidia uchague hali inayofaa mtoto wako. Pata maelezo zaidi kuhusu
mipangilio na vidhibiti vya wazazi.
Video kwenye skrini ya kwanza
Video kwenye skrini ya kwanza hupangwa katika
aina, kama vile “Vipindi” na “Muziki.” Wakati mwingine, YouTube Kids inaweza kuweka aina za kudumu kwa muda mfupi kama vile “Kusoma” ili kuadhimisha mwezi wa kusoma. Video hizi huchaguliwa na programu kwa kutumia algoriti iliyofunzwa kwa njia maalum pamoja na uhakiki unaofanywa na binadamu kwa kiasi fulani. Video zinaweza kuorodheshwa kulingana na maudhui ambayo mtoto wako ametazama au kutafuta. Video hizi zinawakilisha tu kundi ndogo la mamilioni ya video zinazopatikana kwenye YouTube Kids.
Ukichagua mipangilio ya “Maudhui yaliyoidhinishwa pekee”, kutakuwa na aina moja kwenye skrini ya kwanza ya mtoto wako. Aina hii, inayoitwa “Yaliyoidhinishwa kwa ajili yako," itakuwa na maudhui ambayo umechagua mwenyewe.
Video zinazopendekezwa
Video zinazopendekezwa huchaguliwa na algoriti yetu na mara nyingi hazitegemei uhakiki unaofanywa na binadamu. Video zinazopendekezwa huonekana wakati Utafutaji umewashwa au kuzimwa na huonyeshwa kama aina ya ziada kwenye skrini ya kwanza baada ya video nyingi kutazamwa kwenye YouTube Kids. Video zinazopendekezwa zinaweza pia kuonekana katika aina nne za video kwenye skrini ya kwanza na kama mapendekezo ili mtoto wako atazame baada ya kutazama video kwenye skrini ya kwanza au baada ya kutafuta video. Video zinazopendekezwa hulingana na maudhui ambao yametazamwa au kutafutwa kwenye programu na hutolewa kwenye kikundi kamili cha video zinazopatikana katika YouTube Kids.
Unaweza kubadilisha video kwenye sehemu ya
Zinazopendekezwa kwa kufuta historia ya programu katika
vidhibiti vya wazazi. Kumbuka, unapozima utafutaji, video
Zinazopendekezwa zitafutwa, pamoja na historia ya video ulizotazama na mambo uliyotafuta.
Wakati mipangilio ya Simamisha historia imewashwa, programu itaacha kutumia video mpya unazotazama au mambo unayotafuta, kubaini video Unazopendekezewa. Unaweza kuwasha au kuzima mipangilio ya Simamisha historia katika vidhibiti vya wazazi.
Iwapo mipangilio ya wasifu wa mtoto wako imewekwa kuwa 'Maudhui yaliyoidhinishwa pekee', Video zinazopendekezwa hutolewa tu kwenye maudhui ambayo umeidhinisha kwa ajili ya mtoto wako. Pata maelezo zaidi kuhusu
Video zinazopendekezwa.
Itazame tena
Sehemu ya
Itazame tena huruhusu mtoto wako kuchagua kutoka kwenye video ambazo alitazama awali katika programu.
Unaweza kubadilisha video kwenye sehemu ya
Itazame tena kwa kufuta historia ya programu katika
vidhibiti vya wazazi. Kumbuka kuwa unapozima utafutaji, video zako kwenye sehemu ya
Itazame tena zitafutwa, pamoja na historia ya video ulizotazama na mambo uliyotafuta.
Wakati mipangilio ya Simamisha historia imewashwa programu itaacha kutumia video mpya unazotazama au mambo unayotafuta, kubaini video zako za Itazame tena. Unaweza kuwasha au kuzima mipangilio ya Simamisha historia katika vidhibiti vya wazazi.
Ni vidhibiti vipi vya wazazi vinapatikana kwenye YouTube Kids?
Tumejumuisha vipengele ili uweze kuweka upendavyo hali ya utumiaji wa mtoto wako kwenye YouTube Kids. Kwa mfano, unaweza kuweka mipangilio ya kipima muda ili kudhibiti muda ambao mtoto anatumia kwenye programu. Vidhibiti vingine ni pamoja na:
Pata maelezo zaidi kuhusu mipangilio na vidhibiti vya wazazi.
Ni aina zipi za utangazaji au matangazo ya biashara huonekana kwenye YouTube Kids?
Tunaruhusu matangazo machache yanayolipiwa (“Matangazo Yanayolipiwa”) kwenye programu ili tuweze kuitoa bila malipo. Mtoto wako anapocheza video kwenye programu, anaweza kuona Tangazo Linalolipiwa, lililowekewa alama ya “Tangazo” na huwa na utangulizi wa tangazo. Lazima Matangazo haya Yanayolipiwa yafuate sera zetu za utangazaji, ambazo, kwa mfano, haziruhusu aina fulani kama vile vyakula na vinywaji. Pata maelezo zaidi kuhusu Matangazo katika YouTube Kids na sera zetu za utangazaji.
Video zinazopakiwa na watumiaji kwenye YouTube si Matangazo Yanayolipiwa, kwa hivyo haziwekewi alama kuwa Tangazo wala hazisimamiwi na sera zetu za utangazaji. Hili linaweza pia kujumuisha maudhui kuhusu au kutoka kwa kampuni ambazo huenda pia zimenunua Matangazo kwenye programu. Kwa mfano, utafutaji wa treni unaweza kuonyesha matokeo ya katuni za treni, nyimbo na video za treni halisi zilizopakiwa na mtumiaji au kampuni ya treni za watoto kuchezea. Hatuchukulii hali hizo zote kuwa Matangazo Yanayolipiwa kwa kuwa si sehemu ya mpango wa matangazo kwenye YouTube Kids. Vivyo hivyo, utafutaji wa chokoleti unaweza kuonyesha matokeo ya video iliyopakiwa na mtumiaji kuhusu kuandaa kipande cha chokoleti hata kama haturuhusu Matangazo Yanayolipiwa ya watengenezaji wa chokoleti. Pata maelezo zaidi kuhusu Video kwenye YouTube Kids.
Iwapo ungependa kutazama video pamoja na mtoto wako bila matangazo yanayolipiwa, jaribu Programu ya YouTube Kids ukiwa na usajili wa YouTube Premium. Pata maelezo zaidi.
Ukusanyaji na matumizi ya taarifa na data binafsi kwenye YouTube Kids
Kwa maelezo kamili kuhusu kanuni zetu za data, unaweza kuangalia Ilani ya Faragha ya YouTube Kids. Unaweza kupata ilani hii katika
kids.youtube.com/t/privacynotice au kwenye Mipangilio ya programu, katika sehemu ya 'Faragha'.
Tunachukua tahadhari ili kulinda faragha ya watumiaji wa programu yetu. Tunamshauri mzazi au mlezi anayetambulika kisheria wa mtoto atakayetumia programu hii, asome ilani hii kabla ya mtoto kuanza kuitumia. Iwapo wewe si mzazi au mlezi unayetambulika kisheria wa mtoto atakayetumia YouTube Kids, au iwapo wewe ni mzazi au mlezi unayetambulika kisheria lakini hukubali
desturi zetu za faragha, usimruhusu mtoto atumie programu.
Programu hii husimamiwa na Google LLC, kampuni inayopatikana 1600 Amphitheatre Pkwy, Mountain View, CA 94043, Marekani.