Vidokezo na nyenzo za wazazi wa vijana kwenye YouTube

Tunaelewa kuwa wakati mwingine wazazi na walezi huwa na maswali kuhusu tabia na maslahi ya vijana wao mtandaoni. Tumeweka pamoja zana na nyenzo fulani ili kukusaidia kudhibiti hali yao ya utumiaji kwenye YouTube.

Nyenzo za wazazi

Ili kuwasaidia wazazi na familia, tumetayarisha Mwongozo wa Familia kuhusu kuwasaidia vijana kutayarisha maudhui kwa ushirikiano na Common Sense Networks, mshirika wa Common Sense Media.

Ili upate vidokezo vya haraka na ushauri, angalia Vidokezo kwa Wazazi au utazame video hizi kwenye Mwongozo wetu wa Familia:

Unaweza pia kumtumia kijana wako nyenzo hizi ili umsaidie kuanza:

Masharti ya umri ya vijana

Ili kuingia katika akaunti ya YouTube, lazima kijana wako awe na Akaunti ya Google inayotimiza masharti ya umri wa chini zaidi katika nchi au eneo unakoishi.

Ikiwa mtoto wako hajafikisha umri unaohitajika, pata maelezo zaidi kuhusu akaunti anazoweza kutumia katika Kituo chetu cha Usaidizi cha YouTube Kwa Familia.

Zana za faragha na usalama

  • Maudhui yasiyofaa: Iwapo wewe au kijana wako amepata video ambayo inaonekana kuwa haifai au huenda inakiuka Mwongozo wetu wa Jumuiya, ripoti video hiyo.
  • Faragha: Iwapo unahisi kuwa faragha ya kijana wako imekiukwa, pata maelezo zaidi kuhusu sera yetu ya faragha na jinsi ya kutuma malalamiko kuhusu faragha.
  • Unyanyasaji na uchokozi wa mtandaoni:
  • Hali yenye Mipaka: Kuwasha mipangilio hii kwenye kifaa cha kijana wako huchuja maudhui ambayo huenda yakawa ya watu wazima kwenye YouTube. Pata maelezo zaidi kuhusu Hali yenye Mipaka.
  • Kudhibiti maoni kwenye chaneli: Kijana wako anaweza kuondoa maoni yaliyochapishwa kwenye chaneli yake au ayadhibiti kabla yaonekane. Pata maelezo zaidi kuhusu kudhibiti maoni kwenye chaneli.
  • Kukadiria umri: Mfumo wetu wa kukadiria umri hutumia ujifunzaji wa mashine ili kubaini iwapo mtumiaji ana umri wa chini ya miaka 18. Ikiwa akaunti imethibitishwa kuwa ya mtumiaji mwenye umri usiozidi miaka 18, ulinzi wa kawaida kwa vijana utatumika kwenye akaunti hiyo. Kwa mfano, zana za nidhamu dijitali kama vile vikumbusho vya kupumzika kidogo vitawashwa kwa chaguomsingi. Pata maelezo zaidi kuhusu ukadiriaji wa umri kwenye YouTube.

Akaunti zinazosimamiwa

Kwa hatua zaidi za usalama, unaweza kufungua akaunti inayosimamiwa kisha uunganishe akaunti yako na ya kijana wako. Wakati umeziunganisha, utaweza kupata maarifa kuhusu shughuli za kijana wako kwenye YouTube. Maarifa haya yanaweza kuibua fursa za kujifunza na mazungumzo ya muda muafaka kuhusu jinsi ya kutayarisha maudhui kwa njia salama kwenye YouTube. Pata maelezo zaidi kuhusu akaunti za vijana zinazosimamiwa.

Usaidizi wa nidhamu dijitali

Je, maelezo haya yamekufaa?

Tunawezaje kuboresha?
Tafuta
Futa utafutaji
Funga kisanduku cha kutafutia
Programu za Google
Menyu kuu
3642927754808615879
true
Tafuta kwenye Kituo cha Usaidizi
false
true
true
true
false
false
false
false
false