Kutatua matatizo ya malipo au ufikiaji yanayohusiana na uanachama unaolipiwa

Malipo yako ya uanachama yakikataliwa, tutakufahamisha kupitia barua pepe ili uweze kurejesha uanachama wako.

Baada ya kupokea barua pepe hii:

  • Utahitajika kurekebisha tatizo ndani ya siku 3 na usipofanya hivyo utapoteza uwezo wa kufikia manufaa yako ya uanachama unaolipiwa. Katika kipindi hiki cha siku 3, tutaendelea kujaribu kuchakata malipo yako ya kila mwezi.

  • Ikiwa baada ya siku 3, bado hatutaweza kukutoza, hali ya usajili wako itabadilika na kuwa "Umesitishwa" kwa siku 30. Usajili wako ukisitishwa, tutajaribu tena na tena kuchakata malipo yako ili kurejesha uanachama wako, isipokuwa ughairi usajili wako.

Ukisasisha maelezo yako ya malipo wakati huu, uanachama wako utarejeshwa kiotomatiki tutakapojaribu kukutoza tena kupitia njia yako ya kulipa. Ikiwa hungependa kusubiri mfumo ujaribu tena kukutoza, unaweza kughairi usajili wako kisha ujisajili upya ili ufikie tena manufaa ya uanachama papo hapo.

Fix billing issues with a Premium membership

Ikiwa unaamini kuwa umetozwa ada ya uanachama unaolipiwa lakini hufikii manufaa yako, angalia makala haya.

Kutatua matatizo ya utozaji kwenye YouTube

Bofya kitufe kilicho hapa chini ili utatue au upate maelezo kuhusu malipo yako kwenye YouTube.

KUTATUA MATATIZO YA UTOZAJI KWENYE YOUTUBE

Iwapo malipo yako ya uanachama unaolipiwa yamekataliwa, kuna uwezekano kuwa unahitaji kurekebisha tatizo kwenye njia yako ya kulipa. Angalia vidokezo vyetu hapa chini kuhusu jinsi ya kurekebisha matatizo hayo.

Kurekebisha tatizo la malipo yaliyokataliwa

Huenda malipo yako ya uanachama ya kila mwezi yamekataliwa kwa sababu kadi au njia yako ya kulipa ina tatizo. Baada ya kurekebisha matatizo yoyote ya malipo, mfumo utajaribu kukutoza tena kiotomatiki na kurejesha uwezo wako wa kufikia manufaa ya uanachama wako.

Hakikisha maelezo ya kadi yako yamesasishwa

Sasisha sasa                

Mara nyingi, malipo hukataliwa iwapo muda wa kutumia kadi ya mikopo umekwisha au ikiwa anwani ya kutuma bili si sahihi. Ili usasishe maelezo haya:

  1. Ikiwa unatumia kompyuta, nenda kwenye youtube.com/paid_memberships . Ikiwa unatumia programu ya YouTube ya vifaa vya mkononi, bofya picha yako ya wasifu  kisha Ununuzi na uanachama.
  2. Bofya  karibu na ujumbe wa "Imeshindwa kuchakata njia ya kulipa sasa ya kulipa ninayotumia sasa".
  3. Bofya Sasisha njia ya kulipa.

Tunapendekeza ukague maelezo yote ya kadi yako ili uhakikishe kuwa ni sahihi, ikiwa ni pamoja na tarehe ya mwisho wa matumizi. Pia, msimbo wa eneo kwenye njia yako ya kulipa unapaswa kulingana na msimbo wa eneo kwenye anwani yako ya sasa ya kutuma bili katika kadi yako.

Ikiwa njia yako ya kulipa iliyo kwenye rekodi zetu haitumiki tena, tafadhali ongeza au uchague njia nyingine ya kulipa.

Kidokezo: Ikiwa hakuna chaguo la "Sasisha njia ya kulipa", unaweza pia kusasisha njia ya kulipa katika Ukurasa wa Usajili na Huduma kwenye Google Pay.

Wasilisha maelezo yanayohitajika

Ukiona ujumbe wa hitilafu unaoomba uwasilishe maelezo zaidi kwa Google, fuata maagizo ili ushiriki maelezo hayo. Kwa mfano, huenda ukahitaji kuthibitisha utambulisho wako kwenye Google Pay kabla ya kufanya ununuzi ukitumia Akaunti yako ya Google.

Unaweza pia kuangalia Google Pay wakati wowote ili upate arifa au maombi ya kurekebisha matatizo ya akaunti.

Thibitisha una pesa za kutosha kufanya ununuzi

Wakati mwingine muamala hukataliwa kwa sababu pesa hazitoshi. Angalia akaunti yako ili uhakikishe kuwa una pesa za kutosha kukamilisha ununuzi.

Wasiliana na benki au kampuni iliyotoa kadi yako

Huenda kadi yako ina vikwazo mahususi vinavyosababisha malipo yako yasichakatwe. Wasiliana na benki au kampuni iliyotoa kadi yako ili uulize kuhusu muamala.

Jaribu kufanya malipo ukitumia njia tofauti ya kulipa 

Sasisha sasa

Tumia njia nyingine ya kulipa kwa kufuata hatua hizi:

  1. Ikiwa unatumia kwenye kompyuta, nenda kwenye youtube.com/paid_memberships. Ikiwa unatumia programu ya YouTube ya vifaa vya mkononi, bofya picha yako ya wasifu  kisha Ununuzi na uanachama.
  2. Bofya aikoni ya kwenye ujumbe "Imeshindwa kuchakata njia ya kulipa ninayotumia sasa".
  3. Bofya Sasisha njia ya kulipa.
  4. Chagua njia tofauti ya kulipa.

Kurekebisha matatizo ya ufikiaji wa manufaa baada ya kutozwa

Iwapo umefanya ununuzi lakini huna idhini ya kufikia kile ulichonunua, kuna uwezekano kuwa malipo yako bado yanachakatwa. Huenda pia usiweze kufikia ikiwa malipo yako yamekataliwa.

Kuhusu ada za muda za kuidhinisha akaunti na miamala ambayo inashughulikiwa

Utozaji unaoshughulikiwa kwenye Google Pay au kwenye kadi yako hubainishwa kama ada za muda za kuidhinisha akaunti ambazo bado hazijachakatwa.

Huenda usajili sawa ukawa na matukio kadhaa ya utozaji ambao unashughulikiwa, kwa kuwa kila utozaji ambao unashughulikiwa unawakilisha jaribio la kuidhinisha akaunti. Ikiwa hali ya utozaji ni "unashughulikiwa" badala ya kuonyesha kuwa umechakatwa, basi hujatozwa; na majaribio yoyote ya uidhinishaji wa kadi ambayo hayajafaulu yataondolewa kiotomatiki kwenye taarifa yako na hutatozwa.

Jinsi ya kuangalia utozaji unaoshughulikiwa

  • Angalia taarifa yako ya malipo au Google Pay. Ukibofya muamala kwenye Google Pay, hali ya ununuzi wako inafaa kuwa "Unashughulikiwa" wala si umekamilika.
  • Tafuta stakabadhi ya malipo kwenye barua pepe. Malipo yakichakatwa, YouTube itakutumia risiti kupitia barua pepe.
  • Unaweza pia kuangalia Google Pay wakati wowote ili upate arifa au maombi ya kurekebisha matatizo ya akaunti. Kwa mfano, huenda ukahitaji kuthibitisha utambulisho wako kwenye Google Pay kabla ya kufanya ununuzi ukitumia Akaunti yako ya Google. Iwapo hakuna arifa kwenye Google Pay, matozo haya yanayoshughulikiwa yatachakatwa ndani ya siku 1-14 za kazi, au yatatoweka malipo yakikataliwa. Malipo yasipochakatwa baada ya muda huu, wasiliana na mtoa huduma wako wa malipo.

Jinsi ya kuangalia malipo yaliyokataliwa

Unaweza kuthibitisha hali ya ununuzi wako kwenye Google Pay. Hali ya muamala kwenye Google Pay inapaswa kuwa "Umekataliwa". Hapa juu, angalia vidokezo vyetu kuhusu kurekebisha malipo yaliyokataliwa.
Ikiwa taarifa yako ya malipo bado inaonyesha "Unashughulikiwa", utozaji huu utachakatwa ndani ya siku 1-14 za kazi au utatoweka malipo yakikataliwa. Malipo yasipochakatwa baada ya muda huu, wasiliana na mtoa huduma wako wa malipo.

 

Je, maelezo haya yamekufaa?

Tunawezaje kuboresha?
Kompyuta Android
Tafuta
Futa utafutaji
Funga kisanduku cha kutafutia
Menyu kuu
7094923437644613531
true
Tafuta kwenye Kituo cha Usaidizi
true
true
true
true
true
59
false
false