Kutatua matatizo ya kulipa kupitia mtoa huduma wako wa vifaa vya mkononi (malipo ya moja kwa moja kupitia mtoa huduma wa simu)

Ikiwa una matatizo yanayohusiana na ununuzi uliotozwa kupitia mtoa huduma wako wa simu za mkononi, jaribu vidokezo hivi vya utatuzi.

Vidokezo kwa wateja wanaotumia kwa mara ya kwanza malipo ya moja kwa moja kupitia mtoa huduma wa simu

Ikiwa unatatizika kulipa kupitia kampuni ya simu, tunapendekeza uanze kuhakikisha kuwa:

  • Umeunganishwa kwenye mtandao wa mtoa huduma wako, iwapo hii ni mara yako ya kwanza kutumia njia ya kulipa kupitia kampuni ya simu kwenye YouTube.
  • Unatumia programu ya YouTube wala si kivinjari cha kifaa cha mkononi au kompyuta.

Pia tunapendekeza uzime kifaa chako, kisha usubiri kwa sekunde chache halafu ukiwashe tena. Baada ya kuwasha kifaa chako, jaribu kununua tena.

Vidokezo zaidi vya utatuzi

Ikiwa bado unakumbwa na matatizo:

  • Hakikisha kuwa unatumia akaunti ya kibinafsi. Huenda baadhi ya kampuni zikazuia malipo kupitia kampuni ya simu ukitumia akaunti za shirika.
  • Thibitisha kuwa hutumii kifaa kilichozibuliwa.
  • Ikiwa unatumia kifaa kilicho na SIM kadi mbili, hakikisha umeweka SIM kadi sahihi kuwa ya 1 na usiweke kadi kwenye nafasi ya SIM kadi ya 2.

Kukagua mipangilio ya mtoa huduma wako

Ikiwa bado unatatizika baada ya kujaribu haya, huenda kuna mipangilio ya mtoa huduma inayoathiri huduma yako. Wasiliana na mtoa huduma wako ili uthibitishe kuwa:

  • Hujafikia kikomo kilichowekwa na mtoa huduma cha ununuzi wa kibinafsi au kiasi unachoweza kutumia kila mwezi (ukifikia vikomo hivyo, chaguo la malipo hutoweka).
  • Una salio la kutosha kufanya ununuzi, ikiwa unatumia mpango wa kulipia mapema.
  • Kifaa chako na mpango wa huduma unaruhusu ununuzi wa maudhui yanayolipiwa.
  • Kifaa chako kinaweza kutumika kufanya malipo ya simu ya mkononi.

Ikiwa bado unatatizika baada ya kujaribu hatua hizi, wasiliana na mtoa huduma wako wa simu za mkononi ili upate usaidizi zaidi.

Vidokezo kuhusu uanachama unaotozwa kupitia mtoa huduma wa simu za mkononi

Kuanzia tarehe 24 Januari, 2023, Rogers Communications haitakubaliwa tena kuwa njia ya kulipa kwa malipo ya uanachama yanayorudiwa nchini Kanada. Ikiwa ulijisajili kwenye uanachama wa YouTube Premium, YouTube Music Premium au uanachama katika chaneli kupitia Rogers Communications, sasisha njia yako ya kulipa iwe mojawapo ya njia za kulipa zinazokubaliwa.

Iwapo umekuwa ukifanya malipo ya moja kwa moja kupitia mtoa huduma wa simu ili kulipia uanachama wa YouTube unaolipiwa na unatatizika kulipa, wasiliana na mtoa huduma wako ili ujue sababu ya malipo yako kukataliwa. Huenda akaunti yako ina tatizo, kama vile kupitisha kikomo cha kiasi unachokubaliwa kutumia.

Ikiwa hakuna tatizo kwenye akaunti yako ya mtoa huduma, jaribu kuiondoa kama njia ya kulipa kisha uirudishe:

  1. Nenda kwenye Ukurasa wa njia za kulipa kwenye Google Pay kisha uondoe njia ya kulipa kupitia kampuni yako ya simu. Kumbuka: Hutaweza kuondoa njia ya kulipa kupitia kampuni ya simu kwenye akaunti yako ikiwa unatumia njia hii kulipia uanachama wowote unaoendelea.
  2. Nenda kwenye programu ya YouTube kisha uguse picha yako ya wasifu .
  3. Gusa Ununuzi na uanachama kisha ukamilishe mchakato wa kujisajili tena.

Iwapo unatatizika kuweka upya njia ya kulipa kupitia kampuni ya simu, jaribu vidokezo vilivyo hapo juu vya utatuzi kwa wanaotumia huduma kwa mara ya kwanza.

Ikiwa bado unapata hitilafu, tafadhali wasiliana na mtoa huduma wako wa simu za mkononi ili upate usaidizi zaidi.

Je, maelezo haya yamekufaa?

Tunawezaje kuboresha?
Tafuta
Futa utafutaji
Funga kisanduku cha kutafutia
Menyu kuu
13810913149957836288
true
Tafuta kwenye Kituo cha Usaidizi
true
true
true
true
true
59
false
false