Fahamu kuhusu gharama unazotozwa bila kutarajia kutoka YouTube

Iwapo YouTube imetoza kadi yako ya mikopo au akaunti ya benki bila wewe kutarajia (iliyoonyeshwa kama “GOOGLE*YouTube”), soma hapa chini ili upate maelezo zaidi kuhusu sababu ya kutozwa.


Jinsi ya kukabiliana na gharama unazotozwa bila kutarajia kutoka YouTube

Fuatilia chaneli ya Watazamaji ya YouTube ili upate habari, taarifa na vidokezo vipya.

Nilitozwa pesa nyingi mno

  • Marekebisho ya kiwango cha ushuru: Huenda ukaona mabadiliko madogo katika malipo yako ya kila mwezi kutokana na kubadilika kwa viwango vya ushuru vinavyohusiana na uanachama wako unaolipiwa. Ushuru unaotozwa katika ununuzi kwenye YouTube hubainishwa kwa mujibu wa sheria za ushuru zinazotumika mahali ulipo na kiasi hicho kinachotozwa kinaweza kubadilika kulingana na masharti ya ushuru katika eneo husika. Unaweza kupata maelezo zaidi hapa na kuangalia stakabadhi za miamala yako, ikiwemo ushuru uliotozwa, kwenye Google Pay.

  • Umebadilisha usajili wako kuwa mpango wa familia: Ikiwa ulibadilisha usajili wako kuwa mpango wa familia hivi majuzi, malipo yako ya kila mwezi yatakuwa juu kuliko mpango wa awali wa kibinafsi. Tembelea http://youtube.com/purchases ili uone ada na hali ya mpango wako.

  • Ada: Huenda benki au kampuni ya kadi yako ikakutoza ada kwa miamala ya kimataifa, kulingana na eneo uliko. Pia, huenda kiasi cha jumla kikabadilika kutokana na ubadilishaji kati ya Dola za Marekani na sarafu ya nchi ulimo.

  • Ada za muda za kuidhinisha akaunti: Huenda ukatozwa ada ya muda ya kuidhinisha akaunti inayolingana na kiasi unachotozwa kila mwezi. Uidhinishaji huu hufanyika ili YouTube ithibitishe kuwa kadi ni sahihi na una pesa za kutosha katika akaunti yako kufanya ununuzi - lakini utozaji huu si malipo halisi. Pata maelezo zaidi kuhusu ada za muda za kuidhinisha akaunti hapa.

Unaweza kuona kiasi ulichotozwa kwa uanachama wako unaolipiwa kwenye YouTube, kwa kutembelea http://youtube.com/purchases.

Hitilafu ya bei ya YouTube Premium kwenye mipango ya wanafunzi: Kutokana na hitilafu ya kiufundi, baadhi ya wanachama wa YouTube Premium waliojisajili katika mpango wa wanafunzi unaojirudia walitozwa zaidi. Tumeanza kurejesha pesa kwa wanachama wote walioathiriwa. Iwapo wewe ni mwanafunzi na ungependa kuendelea na usajili wako wa Premium kwa ada iliyopunguzwa, hakikisha kuwa umethibitisha usajili wako wa sasa kabla ya kipindi chako cha sasa cha kutozwa kuisha. Ili kufanya hivyo, bofya kitufe cha "Thibitisha sasa" kilichopo ndani ya barua pepe tuliyotuma kwenye akaunti yako.

Nilitozwa kipindi cha kujaribu

Huenda ukatozwa baada ya kujisajili kujaribu ikiwa hujatimiza masharti. Wateja wanaojisajili kwa mara ya kwanza tu kwenye YouTube Premium, Music Premium na Muziki wa Google Play ndio wanatimiza masharti ya kupata vipindi vya kujaribu.

Ikiwa umejisajili kwa mara ya kwanza kujaribu, huenda ukaona ada ya muda ya kuidhinisha akaunti wala si utozaji halisi. Uidhinishaji huu hufanyika ili YouTube ithibitishe kuwa kadi ni sahihi na una pesa za kutosha katika akaunti yako kufanya ununuzi wakati kipindi cha kujaribu kitakwisha. Pata maelezo zaidi kuhusu ada za muda za kuidhinisha akaunti hapa.

Nilitozwa zaidi ya mara moja

Zifuatazo ni sababu za kawaida za kutozwa zaidi ya mara moja kwenye YouTube:

  • Una uanachama zaidi ya mmoja kwenye akaunti yako: Angalia hali hizi za kawaida kuhusu kujisajili zaidi ya mara moja ili uone ikiwa huenda umejisajili kimakosa kwenye uanachama unaolipiwa ambao unaingiliana.

  • Huenda umetozwa ada ya usajili au ya huduma tofauti ya Google: Angalia "Shughuli" katika akaunti yako ya Google Pay ili upate maelezo kuhusu utozaji huo na uthibitishe ikiwa umetokana na uanachama unaolipiwa kwenye YouTube.

  • Una zaidi ya akaunti moja iliyo na uanachama unaolipiwa wa YouTube. Huenda wewe au mtu mwingine aliye na idhini ya kufikia akaunti yako amejisajili kupitia anwani nyingine ya barua pepe, kifaa kingine au mfumo tofauti wa malipo. Ili uangalie akaunti zako zingine za Google:
    1. Bofya picha ya wasifu wako .
    2. Bofya Badilisha akaunti.
    3. Utaona alama ya kuteua kwenye akaunti ambayo umetumia kuingia kwa sasa. Ukiona akaunti yako nyingine imeorodheshwa, iguse ili uingie.
    4. Angalia ikiwa akaunti hiyo ya pili imesajiliwa katika uanachama unaolipiwa kwa kutembelea http://youtube.com/purchases. Ikiwa hakuna akaunti nyingine zilizoorodheshwa, unaweza kujaribu wakati wowote kuingia ukitumia Akaunti zako zingine za Google ili uangalie ikiwa zina uanachama unaoendelea.
  • Huenda unaona ada ya muda ya kuidhinisha akaunti au hali ya utozaji ya "unasubiri kuchakatwa”: Uidhinishaji huu hufanyika ili YouTube ithibitishe kuwa kadi ni sahihi na una pesa za kutosha katika akaunti yako kufanya ununuzi huo - lakini utozaji huu si malipo halisi. Pata maelezo zaidi kuhusu ada za muda za kuidhinisha akaunti hapa.

Ninaona muamala uliotozwa ambao sikufanya

Iwapo umetozwa kwenye akaunti yako na hutambui muamala huo, angalia maagizo na hatua hizi unazopaswa kuchukua ili uwasilishe dai la utozaji ambao haujaidhinishwa.

Je, maelezo haya yamekufaa?

Tunawezaje kuboresha?
Tafuta
Futa utafutaji
Funga kisanduku cha kutafutia
Menyu kuu
9086943337985612178
true
Tafuta kwenye Kituo cha Usaidizi
true
true
true
true
true
59
false
false