Kupata au kudhibiti uanachama wa YouTube Premium kupitia mshirika wa YouTube

Unaweza kununua, na kulipia uanachama wako wa YouTube Premium kupitia baadhi ya watoa huduma za simu za mkononi ambao wanashirikiana nasi ili kuwapa wanachama wao YouTube Premium. Utapokea manufaa yote ya YouTube Premium kama kununua moja kwa moja kutoka YouTube.

Watoa huduma za simu za mikononi tunaoshirikiana nao kwa sasa ni:

  • au by KDDI
  • TIM
  • Orange (Romania)

Ili ujisajili kwenye YouTube Premium kupitia mmojawapo wa watoa huduma hawa, soma zaidi hapa chini.

Kwa wakati huu, ni uanachama wa binafsi pekee wa YouTube Premium unaoweza kununuliwa kupitia kampuni hizi. Ikiwa ungependa kununua mpango wa familia, utahitaji kujisajili moja kwa moja kupitia YouTube.

au by KDDI

Ili ujisajili kwenye YouTube Premium kupitia au by KDDI, tembelea ukurasa huu.
Malipo: Ikiwa unatozwa kupitia au by KDDI, YouTube Premium itaonekana kama matumizi kwenye malipo yako ya kila mwezi ya simu ya mkononi.
Kughairi au kusimamisha uanachama: Huwezi kusimamisha uanachama wako wa YouTube Premium iwapo unatozwa kupitia au by KDDI. Ili ukatishe uanachama wako, wasiliana na au by KDDI - sera zake za kutamatisha na kurejesha pesa zitatumika.
Kubadilisha uanachama unaolipiwa: Haiwezekani kubadilisha kutoka Uanachama wa YouTube Premium kwenda Uanachama wa YouTube Music Premium kupitia au by KDDI. Uanachama wa YouTube Premium unajumuisha uwezo wa kufikia YouTube Music Premium bila gharama ya ziada.
Ili ubadilishe uanachama wako unaolipiwa wa YouTube Music Premium:
  1. Wasiliana na au by KDDI ili ughairi uanachama wako wa sasa.
  2. Subiri hadi uanachama wako unaolipiwa uishe (utapoteza uwezo wa kufikia manufaa ya uanachama wako mwishoni mwa kipindi chako cha kutozwa
  3. Jisajili kwenye uanachama wa YouTube Music Premium moja kwa moja kupitia YouTube.

TIM

Ili ujisajili kwenye YouTube Premium kupitia TIM, tembelea ukurasa huu.
 
Kughairi au kusimamisha uanachama: Huwezi kusimamisha uanachama wako wa YouTube Premium iwapo unatozwa kupitia au by TIM. Ili ukatishe uanachama wako, wasiliana na TIM - sera zake za kutamatisha na kurejesha pesa zitatumika.
Kubadilisha uanachama unaolipiwa: Haiwezekani kubadilisha kutoka Uanachama wa YouTube Premium kwenda Uanachama wa YouTube Music Premium kupitia TIM. Uanachama wa YouTube Premium unajumuisha uwezo wa kufikia YouTube Music Premium bila gharama ya ziada.

Orange (Romania)

Unaponunua kitu, utaona tozo katika akaunti ya mtoa huduma wako baada ya dakika 15.

Kumbuka: Huenda ukaona SMS (ujumbe wa maandishi) inayoanza kwa "DCB" au "DCB_Association" kwenye simu yako ukijisajili katika huduma ya kulipa kupitia simu ya mkononi. Ujumbe utazalishwa kiotomatiki na kutumwa ili kukamilisha uandikishaji wa malipo ya akaunti yako ya YouTube kupitia simu ya mkononi.

Je, maelezo haya yamekufaa?

Tunawezaje kuboresha?
Tafuta
Futa utafutaji
Funga kisanduku cha kutafutia
Menyu kuu
10919750742438663613
true
Tafuta kwenye Kituo cha Usaidizi
true
true
true
true
true
59
false
false