Kutumia Ulinganishaji wa Content ID kwenye mitiririko mubashara

 

Vipengele hivi vinapatikana tu kwa washirika ambao hutumia Kidhibiti Maudhui cha Studio ya YouTube. Wasiliana na Msimamizi wako wa Washirika wa YouTube ili uweze kuvitumia.

Washirika fulani wanaweza kutumia ulinganishaji wa Content ID kupata nakala ya mitiririko yao mubashara inayofanyika katika muda halisi. Idhini ya kufikia Ulinganishaji mubashara wa Content ID hutolewa katika kiwango cha Mdhibiti wa Maudhui. Hata hivyo, ulinganishaji unaweza kuwashwa na kudhibitiwa na kituo mahususi kinachotiririsha pekee.

Washa Ulinganishaji wa Content ID kwenye mtiririko wako mubashara

Kabla ya kuanza, hakikisha unaweka vituo vyovyote vilivyoidhinishwa ambavyo vitakuwa vinatiririsha mubashara tukio lako kwenye orodha yako ya vituo vilivyoruhusiwa.

Ili uanzishe mtiririko wako mubashara wenye Ulinganishaji wa Content ID:

  1. Ingia katika akaunti ya Studio ya YouTube na uchague TAYARISHA kisha Tiririsha mubashara.
  2. Katika menyu ya kushoto, bofya Mtiririko.
  3. Bofya Tukio jipya mubashara.
  4. Chagua kichupo cha Uchumaji wa mapato.
  5. Chini ya “Sera ya matumizi,” chagua sera ya mtiririko wako mubashara.
  6. Chagua kisanduku chini ya “Washa Ulinganishaji wa Content ID” na uteue sera ya zinazolingana ya kuzuia au kuchuma mapato. Kumbuka: Baadhi ya sera hufanya kazi kwa njia tofauti au haziwezi kutumika pamoja na Ulinganishaji wa Content ID. Tazama maelezo hapa chini.
  7. Weka maelezo kuhusu kipengee chako. Chagua Wavuti kama aina ya kipengee chako.
  8. Weka maelezo yaliyosalia ya mtiririko wako mubashara na uanze kutiririsha.

Pata maelezo kuhusu kutayarisha mitiririko mubashara.

Sera hufanyaje kazi na mitiririko mubashara?

Nakala za mtiririko mubashara haziwezi kufuatiliwa au kutumiwa kuchuma mapato. Unaweza kuamua sera ya zinazolingana na kuzuia au kuchuma mapato, lakini zote zitasababisha maonyo ya mtiririko mubashara na hatimaye kuondolewa. Sera za wimbo hazitafanya kazi kwa Ulinganishaji wa Content ID kwenye mitiririko mubashara.

Vile vile, sera zinazopeleka maudhui kwenye ukaguzi na sera zenye masharti ya asilimia ya kulingana kwa video haziwezi kutumika pamoja na Ulinganishaji mubashara wa Content ID.

Masharti ya Ulinganishaji wa Content ID kwenye mitiririko mubashara

Masharti ya kutumia

Kutumia Ulinganishaji wa Content ID kwenye mitiririko mubashara ni tukio nyeti sana na huongeza kiwango cha ugumu katika usimamizi wa haki. Ili upate idhini ya kufikia, ni sharti uwe na:

  • Rekodi inayothibitika ya kutumia Content ID bila matatizo.
  • Maudhui mubashara yanayotegemea muda, kama vile tukio la spoti au tamasha la muziki.
  • Uwezekano mkubwa kuwa watumiaji watatiririsha mubashara nakala za maudhui yako.

Masharti ya kutumia

Ukishapata idhini ya kutumia Ulinganishaji wa Content ID kwenye mitiririko mubashara, hakikisha kuwa mtiririko wako unatimiza masharti yafuatayo:

  1. Haki za kimataifa: Ulinganishaji wa Content ID kwenye mitiririko mubashara unaweza kutumika tu kwenye maudhui ambayo unamiliki haki zake katika maeneo yote duniani.
  2. Umiliki wa kipekee: Mtiririko wako mubashara haupaswi kujumuisha maudhui yoyote ya wahusika wengine, kama vile picha tuli, matangazo au muziki wa chinichini.

Pata maelezo kuhusu jinsi Ulinganishaji wa Content ID kwenye matukio mubashara unavyofanya kazi

Kutumia Ulinganishaji wa Content ID, tunalinganisha mtiririko wako mubashara na mitiririko mingine mubashara. Mtiririko unaolingana unapopatikana:

  • Mwanzoni, tutaonyesha ujumbe wa onyo kwa anayetiririsha moja kwa moja maudhui yako.
  • Ulinganishaji ukiendelea, mtiririko wao huenda ukabadilishwa kuonyesha picha tuli bila sauti.
  • Ulinganishaji ukiendelea bado, unaweza kusimamishwa na anayetiririsha moja kwa moja anaweza kupoteza uwezo wa kufikia vipengele vya moja kwa moja. Pata maelezo zaidi kuhusu matatizo ya hakimiliki kwenye mitiririko mubashara.

Linganisha Content ID ya kawaida na Ulinganishaji wa Content ID wa maudhui mubashara

Hizi hapa chini ni tofauti kuu kati ya Ulinganishaji wa Content ID wa maudhui mubashara na Content ID ya kawaida.
 

  Ulinganishaji wa Content ID wa maudhui mubashara Content ID ya kawaida 
Madai Hamna madai yaliyowasilishwa. Madai huwasilishwa kwa video zinazolingana ili kutumia sera za zinazolingana.
Udhibiti wa Content ID
 

Hudhibitiwa kwenye mtiririko wa kituo mahususi.

Mipangilio haiwezi kubadilisha baada ya kuanza kutiririsha.

Hudhibitiwa kwenye Kidhibiti chako cha Maudhui au kituo mahususi kinachopakia.

Mipangilio inaweza kubadilishwa wakati wowote.

Utekelezaji Maonyo huonyeshwa kwa anayetiririsha moja kwa moja kabla mtiririko haujakatizwa au kusimamishwa. Utiririshaji unaolingana unapopatikana, sera za zinazolingana hutumiwa kiotomatiki.
Sera Haifanyi kazi na aina za sera zifuatazo:
  • Sera za nyimbo
  • Sera za masharti ya kuelekeza maudhui ili yakaguliwe
  • Sera za masharti ya asilimia ya video inayolingana
Hufanya kazi na aina zote za sera.

Je, maelezo haya yamekufaa?

Tunawezaje kuboresha?
Tafuta
Futa utafutaji
Funga kisanduku cha kutafutia
Menyu kuu
13509675094168683303
true
Tafuta kwenye Kituo cha Usaidizi
true
true
true
true
true
59
false
false