Sura za Video

Sura za Video hugawanya video katika sehemu, kila moja ikiwa na kionjo chake. Sura za video huweka maelezo na muktadha kwa kila sehemu ya video na hukuruhusu kutazama tena sehemu mbalimbali za video kwa urahisi. Watayarishi wanaweza kujiwekea sura za video kwa kila video wanayopakia au wategemee sura za video zinazowekwa kiotomatiki. Sura zinaweza kuonekana kwenye manukuu. Wakati wowote, watayarishi wanaweza kuchagua kutotumia sura za video za kiotomatiki katika Studio ya YouTube.

Kumbuka: Si video zote zinastahiki sura za kiotomatiki na si video zote zinazostahiki zitakuwa na sura za kiotomatiki. Iwapo chaneli ina maonyo yoyote yanayoendelea au iwapo huenda maudhui hayafai kwa baadhi ya watazamaji, kipengele cha sura za video hakitapatikana.

How to Add Chapters to Your Videos Using Timestamps

Ili ujiwekee sura za video:

  1. Ingia katika akaunti ya Studio ya YouTube.
  2. Kwenye menyu ya kushoto, chagua Maudhui.
  3. Bofya video ambayo ungependa kuhariri.
  4. Katika Maelezo, weka orodha ya mihuri ya wakati na vichwa.
    • Hakikisha kuwa muhuri wa kwanza wa wakati unaoorodhesha unaanza kwa 00:00. 
    • Video yako inapaswa kuwa na angalau mihuri mitatu ya wakati iliyoorodheshwa katika mpangilio wa kupanda.
    • Muda wa chini zaidi wa sura za video unaoruhusiwa ni sekunde 10.

 5. Bofya HIFADHI.

Kumbuka: Chaguo hili litabatilisha sura za video zilizowekwa kiotomatiki.

Kutumia sura za kiotomatiki za video:

  1. Ingia katika akaunti ya Studio ya YouTube.
  2. Kwenye menyu ya kushoto, chagua Maudhui.
  3. Bofya video ambayo ungependa kuhariri.
  4. Bofya ONYESHA ZAIDI na chini ya Sura za Kiotomatiki chagua “Ruhusu sura za kiotomatiki (zinapopatikana na zinapostahiki)”. Kwa chaguomsingi, kisanduku hiki kitachaguliwa kwa video zote mpya unazopakia. Unaweza pia kuruhusu sura za kiotomatiki kwenye video nyingi kwa pamoja.
  5. Bofya HIFADHI.
Kumbuka: Si video zote zinastahiki sura za kiotomatiki na si video zote zinazostahiki zitakuwa na sura za kiotomatiki. Iwapo chaneli ina maonyo yoyote yanayoendelea au iwapo huenda maudhui hayafai kwa baadhi ya watazamaji, kipengele cha sura za video hakitapatikana.

Ili uhariri sura za kiotomatiki za video:

  1. Ingia katika akaunti ya Studio ya YouTube.
  2. Kwenye menyu ya kushoto, chagua Maudhui.
  3. Bofya video ambayo ungependa kuhariri.
  4. Bofya Sura zinazopatikanakisha WEKA SURA na sura zako za kiotomatiki zitaonekana kwenye maelezo yako ili uhariri. Unaweza kubofya Futa  ili uondoe sura za kiotomatiki za video kwenye video yako.
  5. Bofya HIFADHI.

Kuchagua kutotumia sura za kiotomatiki za video:

Ili uchague kutotumia sura za kiotomatiki za video kwenye video mahususi:

  1. Ingia katika akaunti ya Studio ya YouTube.
  2. Kwenye menyu ya kushoto, chagua Maudhui.
  3. Bofya video ambayo ungependa kuhariri.
  4. Bofya ONYESHA ZAIDI na chini ya Sura za Kiotomatiki acha kuchagua “Ruhusu sura za kiotomatiki (zinapopatikana na zinapostahiki)".
  5. Bofya HIFADHI.
Kumbuka: Unaweza pia kuchagua kutotumia sura za video za kiotomatiki kwenye video nyingi kwa pamoja.

Ili uchague kutotumia sura za kiotomatiki za video kwenye video mahususi:

  1. Ingia katika akaunti ya Studio ya YouTube.
  2. Bofya Mipangilio .
  3. Bofya Mipangilio chaguomsingi ya video zinazopakiwa.
  4. Bofya Mipangilio ya kina, batilisha uteuzi wa  "Ruhusu sura za kiotomatiki (zinapopatikana na zinapostahiki)".
  5. Bofya HIFADHI.

Je, maelezo haya yamekufaa?

Tunawezaje kuboresha?
Tafuta
Futa utafutaji
Funga kisanduku cha kutafutia
Menyu kuu
4865641676322164080
true
Tafuta kwenye Kituo cha Usaidizi
true
true
true
true
true
59
false
false