Zana na huduma za mshirika mwingine

Kumbuka: Huduma zilizo kwenye orodha hii zinatolewa na mshirika mwingine, Google haiwezi kukuhakikishia ubora wa huduma wala kukusaidia kuhusu mzozo wowote unaoweza kutokea kati yako na mtoa huduma. Pia, orodha hii si ya kina na haionyeshi kuwa Google ina uhusiano wowote rasmi na watoa huduma hawa. Ni hiari kushiriki katika orodha hii ya watoa huduma.

Unaweza kudhibiti manukuu, tafsiri na mahitaji yako ya manukuu kwa kutumia zana na huduma za mshirika mwingine. Zana na huduma hizi za wengine zinasimamiwa na sheria na masharti yao ambayo unapaswa kuyasoma na kuyaelewa. 

Watoa huduma za manukuu

Kampuni Maelezo
3Play Media 3Play Media ni mtoa huduma za manukuu na huduma za ufikivu za video za mtandaoni. Angalia makala haya kwenye tovuti ya 3Play Media ili upate maelezo zaidi.
Amara Amara ni mtoa huduma za manukuu na huduma za ufikivu za video (Amara On Demand) na zana zinazosaidia kudhibiti michango ya jumuiya (Jumuiya ya Amara). Angalia makala haya kwenye tovuti ya Amara ili upate maelezo zaidi.
Cielo24 Cielo24 ni mtoa huduma za manukuu na huduma za ufikivu za video za mtandaoni. Angalia makala haya kwenye tovuti ya Cielo24 ili upate maelezo zaidi.
Rev

Rev ni mtoa huduma za manukuu na huduma za ufikivu za video za mtandaoni. Angalia makala haya kwenye tovuti ya Rev ili upate maelezo zaidi.

Amberscript Amberscript hutoa huduma za manukuu, manukuu yaliyotafsiriwa, maelezo ya sauti na kuweka sauti nyingine kwenye maudhui. Kwa kuchanganya akiliunde na timu ya wataalamu wa lugha zaidi ya 1000, Amberscript inatoa manukuu ya kitaalamu kwa sehemu ndogo tu ya gharama. Angalia hapa ili upate maelezo kuhusu jinsi ya kuweka manukuu kwenye video yako ya YouTube au angalia tovuti ya Amberscript ili upate huduma za ziada.

Watoa huduma za kuweka sauti nyingine kwenye maudhui

Kampuni Maelezo
Creator Global CreatorGlobal ni watoa huduma za kuweka sauti nyingine kwenye maudhui inayosaidia watayarishi kuwa magwiji wa kimataifa kwa kujanibisha maudhui yao na kukuza vituo vyao katika masoko mapya. Angalia tovuti ya Creator Global ili upate maelezo zaidi na utume maswali hapa.
Air.io

AIR hutoa huduma tofauti za tafsiri na ujanibishaji kwa WanaYouTube katika lugha zaidi ya 50: kuanzia manukuu, tafsiri, ujanibishaji, uwekaji sauti nyingine kwenye maudhui unaofanywa na binadamu au kwa AI hadi vituo vya YouTube ambavyo vimeshatafsiriwa na vilivyojanibishwa. Angalia makala haya kwenye tovuti ya AIR ili upate maelezo zaidi na uwasilishe maswali hapa.

Papercup Teknolojia ya uwekaji sauti nyingine kwenye maudhui inayowezeshwa na AI ya Papercup inatoa huduma ya uwekaji sauti nyingine kwenye maudhui yenye bei nafuu, ubora unaokaguliwa na watafsiri. Sauti zetu zilizobuniwa na kompyuta zimewezesha mamia ya mamilioni ya utazamaji kwenye YouTube. Angalia tovuti ya Papercup ili upate maelezo zaidi na uwasilishe maswali hapa.
VITAC

VITAC, Kampuni ya Verbit, ni watoa huduma za sekta ya maudhui za uwekaji sauti nyingine kwenye maudhui, manukuu na tafsiri kwa kampuni zote kuu za utayarishaji wa maudhui ya TV, Mitandao na Watayarishi wa Maudhui wa YouTube duniani kote. Angalia VITAC ili upate maelezo zaidi na uwasilishe maswali hapa.

Vidby Vidby ni programu inayowezeshwa na AI kwa ajili ya tafsiri na uwekaji sauti nyingine katika video kwa haraka, kwa bei nafuu na usahihi wa asilimia 100 katika lugha 75 na lahaja 65 yenye maktaba ya kutosha ya sauti (ikijumuisha watoto, vijana, watu wazima na wakongwe) unazoweza kuchagua. Angalia makala haya kwenye tovuti ya Vidby ili upate maelezo zaidi na utume maswali hapa.
WellSaid Labs WellSaid Labs ni watoa huduma bora zaidi katika sekta ya sauti zilizobuniwa na kompyuta, wanaoaminiwa na maelfu ya kampuni kote duniani. Angalia tovuti ya WellSaid Labs ili upate maelezo zaidi na utume maswali hapa.
Shorthand Studios Shorthand Studios ni watoa huduma wa toleo jipya kwa ajili ya watayarishi na chapa za kidijitali kwanza wenye uwezo wa hali ya juu wa kutafsiri. Studio hiyo hutoa huduma za uchapishaji katika zaidi ya lugha 20 kwa chapa maarufu za kisasa. Angalia tovuti ya Shorthand Studios ili upate maelezo zaidi na uwasilishe maswali hapa.
Deep Media Deep Media hutoa huduma za tafsiri na uwekaji sauti nyingine kwenye maudhui bila malipo kwa kutumia DubSync. Zana hii ya kimapinduzi inayowezeshwa na AI huondoa vizuizi vya lugha kwa haraka na urahisi katika lugha zaidi ya 20. Angalia tovuti ya Deep Media ili upate maelezo zaidi na uwasilishe maswali hapa.
XTracks XTracks hutoa huduma ya ubora wa juu ya Kuweka sauti nyingine kweye maudhui na Maelezo ya Sauti ili kujanibisha maudhui yako na kuyafanya yafikiwe na hadhira za vipofu na wenye uwezo mdogo wa kuona. Angalia tovuti ya XTracks ili upate maelezo zaidi.
Ollang Ollang ni mfumo wa duka la pamoja linalotoa huduma ya ujanibishaji wa mwanzo hadi mwisho. Unatoa huduma za manukuu, uwekaji wa sauti nyingine kwenye maudhui wa ubora wa juu uliofanyika studio na ule wa AI kwa TV, filamu, watayarishi na mifumo ya mafunzo ya kielektroniki. Angalia tovuti ya Ollang ili upate maelezo zaidi na uwasilishe maswali hapa.
Dubverse Dubverse.ai hutoa huduma ya muda halisi iliyowezeshwa na AI ya Uwekaji Sauti Nyingine kwenye Video na Manukuu katika lugha zaidi ya 30 na mfumo wa kujihudumia, kuanzia toleo la BILA MALIPO lililoubuniwa kwa ajili ya watayarishi. Angalia makala haya kwenye tovuti ya Dubverse.ai ili upate maelezo zaidi.

Kuondoa ufikiaji wa washirika wengine

Ikiwa hutaki tena ufikiaji wa washirika wengine kwenye akaunti yako ya Google, unaweza kuuondoa wakati wowote.

Je, maelezo haya yamekufaa?

Tunawezaje kuboresha?
Tafuta
Futa utafutaji
Funga kisanduku cha kutafutia
Menyu kuu
2123923790398511616
true
Tafuta kwenye Kituo cha Usaidizi
true
true
true
true
true
59
false
false