Tumia Takwimu za YouTube ili ufahamu mahali ambako wanaokufuatilia walikuwa walipogusa kitufe cha “Fuatilia”. Maelezo haya yanakusaidia kuelewa ni maudhui au kurasa zipi za YouTube zinazowashawishi zaidi watazamaji waanze kufuatilia kituo.
Kuangalia vyanzo vya wanaofuatilia chaneli yako
- Ingia katika Studio ya YouTube.
- Kwenye menyu ya kushoto, chagua Takwimu .
- Kwenye kadi yoyote, bofya ANGALIA ZAIDI.
- Kutoka sehemu ya juu, chagua chanzo cha Wanaofuatilia .
Kumbuka: Ikiwa video au kituo chako hakina idadi ya kutosha ya watazamaji katika kipindi kilichochaguliwa, huenda usione kipimo cha chanzo cha wanaokufuatilia.
Fahamu vyanzo tofauti vya wanaofuatilia
Ukurasa wa kutazama wa YouTube | Ufuatiliaji kutoka kwenye kitufe cha fuatilia katika kurasa za kutazama video. |
---|---|
Chaneli yako ya YouTube | Ufuatiliaji unaotokana na kitufe cha kufuatilia kwenye ukurasa wa kwanza wa chaneli yako. |
Chaneli nyingine ya YouTube | Ufuatiliaji unaotokana na vituo vingine vinavyoangazia kituo chako. |
Vipengele shirikishi | Ufuatiliaji unaotokana na vipengele vinavyoshirikisha mtumiaji katika video zako, kama vile skrini za mwisho au alama maalum katika video. |
Ukurasa wa kwanza wa YouTube | Ufuatiliaji unaotokana na ukurasa wa kwanza wa YouTube. |
Utafutaji kwenye YouTube | Ufuatiliaji unaotokana na matokeo ya utafutaji. Unaweza pia kusoma ni hoja zipi za utafutaji ambazo watazamaji waliweka katika upau wa kutafutia kabla ya kuanza kufuatilia. |
Utangazaji wa YouTube | Ufuatiliaji unaotokana na matangazo. |
Machapisho | Ufuatiliaji unaotokana na Machapisho ya Jumuiya. |
Mpasho wa chaneli unazofuatilia | Kupungua kwa idadi ya wanaofuatilia kutokana na mipasho ya vituo wanavyofuatilia. Maelezo haya yanaweza kukusaidia kuelewa jinsi mara ambazo unapakia video zinavyoathiri idadi yako ya wanaofuatilia. |
Orodha ya vituo unavyofuatilia | Kujiondoa kwenye orodha ya usajili ya vifaa vya mkononi na kidhibiti cha kujisajili cha kompyuta. |
Akaunti zilizofungwa | Kupungua kwa idadi ya wanaofuatilia kumesababishwa na kuondolewa kwa taka na akaunti zilizofungwa. |
Ya nje | Ufuatiliaji unaotokana na video au vitufe vya kufuatilia vilivyopachikwa kwenye tovuti zingine kando na YouTube. |
(Wasanii pekee) Vituo Rasmi vya Msanii |
Iwapo una Chaneli Rasmi ya Msanii, wanaofuatilia moja kwa moja kwenye ukurasa wa kwanza wa Chaneli yako Rasmi ya Msanii watahesabiwa katika safu mlalo ya "Chaneli yako ya YouTube". Wafuatiliaji kutokana na chaneli otomatiki ya msanii au ukurasa uliotangulia wa kwanza wa chaneli watahesabiwa katika safu mlalo ya "Chaneli Rasmi ya Msanii". |
Sababu nyingine | Ufuatiliaji unaotokana na vyanzo visivyojulikana. |
Kumbuka: Katika Takwimu za YouTube, unaweza kuona uchanganuzi wa idadi ya wanaofuatilia ambao walifuatilia kutokana na video, Video Fupi, mtiririko mubashara, machapisho yako na mengine. Pata maelezo zaidi.