Jinsi ambavyo matangazo hufanya kazi kwenye YouTube katika akaunti zinazodhibitiwa na maudhui yaliyobainishwa kuwa "yanalenga watoto"

Sera za utangazaji za maudhui yanayolenga watoto zinaweza kubadilika kulingana na muda. Tunakuhimiza uangalie tena mara kwa mara ili usome taarifa mpya zaidi.

Ili kutii Sheria ya Kulinda Faragha ya Watoto Mtandaoni na sheria nyinginezo, matangazo yaliyowekewa mapendeleo, kurudia matangazazo na vipengele vinginevyo vinavyolenga kuweka mapendeleo haviruhusiwi kwenye YouTube kwa:

Matangazo yenye muktadha yanaweza kuonyeshwa kwenye YouTube katika akaunti zinazodhibitiwa na maudhui yaliyobainishwa kuwa yanalenga watoto. Matangazo haya yanalingana na vigezo kama vile:

  • Maudhui yanayotazamwa
  • Utafutaji wa sasa wa mtazamaji
  • Mahali mtazamaji alipo (kama vile jiji au jimbo)

Ni lazima matangazo yafuate sera ya matangazo ya maudhui yanayolenga watoto ili yaweze kustahiki kuonyeshwa kwenye YouTube katika akaunti zinazodhibitiwa na katika maudhui yaliyobainishwa kuwa yanalenga watoto.

Kutazama matangazo kwenye maudhui "yanayolenga watoto"

Huenda matangazo ya aina fulani yakaonekana kwenye maudhui yaliyobainishwa kuwa "yanalenga watoto". Watazamaji wa maudhui "yanayolenga watoto" wanaweza kuona bamba la tangazo kabla na baada ya tangazo la video kuonyeshwa. Bamba hili husaidia kuwaarifu tangazo linapoanza na linapomalizika. 

Ili kuelewa sera za utangazaji kuhusu matangazo kwenye maudhui "yanayolenga watoto," angalia sera yetu ya matangazo ya maudhui "yanayolenga watoto".

Sera kuhusu watangazaji

Watangazaji hawaruhusiwi kuonyesha matangazo yaliyowekewa mapendeleo kwenye YouTube kwa akaunti zinazodhibitiwa wala maudhui yaliyobainishwa kuwa yanalenga watoto.

Utangazaji ambao unalenga watoto au maudhui yaliyobainishwa kuwa yanalenga watoto ni lazima yatii sheria na kanuni zote husika. Hauwezi:

  • Kuwa danganyifu, usio wa haki au kutofaa kwa hadhira inayokusudiwa
  • Kutumia vifuatiliaji vya wengine au kujaribu kukusanya taarifa binafsi

Zifuatazo ni baadhi ya bidhaa ambazo watangazaji hawaruhusiwi kutangaza kwenye YouTube kwa akaunti zinazodhibitiwa au maudhui yaliyobainishwa kuwa yanalenga watoto:

  • Maudhui yasiyofaa kwa watoto: Maudhui (Filamu, Vipindi vya televisheni, nk.) ambayo ni nyeti kuonyeshwa kwa watumiaji walio na umri wa chini ya miaka 13.
  • Michezo ya video isiyofaa kwa watoto: Michezo ya kielektroniki ya video (na vifuasi vinavyohusiana) vinavyoweza kuchezwa kwenye kifaa cha michezo ya video, kompyuta au kifaa kingine cha kielektroniki kama vile simu ya mkononi au kompyuta kibao haviruhusiwi ikiwa ukadiriaji wa kisekta wa mchezo utaonyesha haufai kwa hadhira zilizo na umri wa chini ya miaka 13.
  • Kuchumbiana na mahusiano: Matangazo ya tovuti za kuchumbiana, ushauri nasihi kwa familia na huduma za ndoa au talaka.
  • Urembo na kupunguza uzito: Bidhaa zinazohusiana na utunzaji wa mwili (kwa nje), bidhaa za siha zinazohusiana na kupunguza uzito, lishe na ulaji mlo kamili.
  • Chakula na Vinywaji: Bidhaa zinazohusiana na chakula na vinywaji haziruhusiwi, bila kujali lishe.
  • Bidhaa Haramu au Zinazodhibitiwa: Bidhaa zinazodhibitiwa au haramu kutangazwa kwa watoto, ikiwa ni pamoja na Maudhui Yaliyopigwa Marufuku na Maudhui Yaliyozuiwa haziruhusiwi. Hii pia inajumuisha bidhaa ambazo zinaweza kuhatarisha usalama wa watoto.
  • Matangazo ya kisiasa: Matangazo ya kisiasa yanayolipiwa ya aina yoyote ikijumuisha maelezo kuhusu wagombea au sera zao, vyama vya siasa, kamati za kisiasa au uchangishaji fedha au ajenda zao.
  • Matangazo ya kidini: Matangazo ya kidini ya aina yoyote hayaruhusiwi, k.m, sadaka zinazohusiana na dini fulani, imani za kidini, ikiwa ni pamoja na shule, vitabu vya kidini, nk.
  • Matangazo yanayohusiana na maudhui ya watu wazima: Maudhui ya ngono na ya watu wazima ambayo yanalenga hadhira ya watu wazima na ambayo hayafai kutazamwa na watumiaji walio na umri wa chini ya miaka 13.
  • Maudhui Hatari: Maudhui ambayo ni hatari na yasiyofaa kwa watumiaji walio na umri wa chini ya miaka 13 au ambayo kwa ujumla yanahitaji usimamizi wa watu wazima.
  • Maudhui ya Vurugu: Maudhui ya vurugu na ya kuogofya ambayo yanalenga hadhira za watu wazima na yasiyofaa kwa watumiaji walio na umri wa chini ya miaka 13.

Je, maelezo haya yamekufaa?

Tunawezaje kuboresha?
Tafuta
Futa utafutaji
Funga kisanduku cha kutafutia
Menyu kuu
2436284995511549396
true
Tafuta kwenye Kituo cha Usaidizi
true
true
true
true
true
59
false
false