Angalia iwapo hadhira ya video yako imewekwa kuwa inalenga watoto

Bila kujali mahali ulipo, watayarishi wanahitajika kisheria kutii Sheria ya Kulinda Faragha ya Watoto Mtandaoni na/au sheria zingine. Unatakiwa kutueleza iwapo video zako zinalenga watoto

Ili kukusaidia kutii, mnamo Novemba 2019, tulianzisha mipangilio mipya ya hadhira katika Studio ya YouTube. Katika mipangilio hii, unaweza kubainisha iwapo maudhui yako yanalenga watoto au la. Unaweza kubainisha hadhira yako:

  • Katika kituo ili uteuzi wako ubainishe maudhui yaliyopo au ya baadaye kuwa yanalenga au hayawalengi watoto. 
  • Au katika kiwango cha video. Ukiteua chaguo hili, utahitaji kubaini kila hadhira ya video mpya na ya sasa kuwa inalenga watoto au haiwalengi. 

Angalia iwapo hadhira ya video yako imewekwa kuwa inalenga watoto

Unaweza kuangalia iwapo video yako imewekwa kuwa inalenga watoto na wewe mwenyewe au na YouTube. Pata maelezo kuhusu kinachofanyika maudhui yako yanapowekwa kuwa yanalenga watoto.

  1. Ingia katika akaunti ya Studio ya YouTube.
  2. Kwenye menyu ya kushoto, chagua Maudhui.
  3. Bofya Kichujio chuja matokeo na uchague kichujio/vichujio:
    • Zinazolenga watoto (ulizobainisha): Video zote ulizobainisha kuwa zinalenga watoto. 
    • Zilizowekwa kuwa zinalenga watoto (zilizobainishwa na YouTube): Video zote ambazo YouTube imebainisha kuwa zinalenga watoto.
    • Hazilengi watoto: Video zote unazobainisha kuwa hazilengi watoto. 
    • Hazijabainishwa: Video zote ambazo hazijabainishwa kuwa "zinalenga watoto".  

Unaweza pia kuangalia vizuizi katika programu ya Studio ya YouTube kwenye kifaa chako cha mkononi.

 

Je, maelezo haya yamekufaa?

Tunawezaje kuboresha?
Tafuta
Futa utafutaji
Funga kisanduku cha kutafutia
Menyu kuu
6004853565124687420
true
Tafuta kwenye Kituo cha Usaidizi
true
true
true
true
true
59
false
false