Regardless of your location, you’re legally required to comply with the Children’s Online Privacy Protection Act and/or other laws. You’re required to tell us that your videos are made for kids if you make kids content.
As a YouTube creator, you are required to set future and existing videos as made for kids or not. Even creators who don’t make content for kids need to set their audience. This will help ensure that we offer the appropriate features on your content.
To help you comply, we are introducing a new audience setting on YouTube Studio. You can set your audience:
- At the channel level, which will set all of your future and existing content as made for kids or not.
- Or, at the video level. If you choose this option, you’ll need to set each existing and future video as made for kids or not.
Kidokezo Muhimu: Umuhimu wa kila mtayarishi kubainisha hadhira yake
Mabadiliko haya yanahitajika kama sehemu ya makubaliano na Tume ya Biashara ya Marekani (FTC) na Mwanasheria Mkuu wa New York na yatakuwezesha kutii Sheria ya Kulinda Faragha ya Watoto Mtandaoni (COPPA) na/au sheria zingine husika. Bila kuzingatia mahali uliko, tunahitaji utueleze iwapo video zako zinalenga watoto au haziwalengi. Iwapo hutabainisha hadhira yako kwa njia sahihi, huenda ukapata matatizo ya ukiukaji wa sheria kwa mujibu wa FTC au mamlaka zingine na huenda tukachukua hatua dhidi ya akaunti yako ya YouTube. Pata maelezo zaidi kuhusu jinsi FTC hutekeleza COPPA.
Note: We’ll also use machine learning to help us identify videos that are clearly directed to young audiences. We trust you to set your audience accurately, but we may override your audience setting choice in cases of error or abuse. However, do not rely on our systems to set your audience for you because our systems may not identify content that the FTC or other authorities consider to be made for kids. If you need help determining whether or not your content is made for kids, check out this Help Center article or consult legal counsel.
Kuweka hadhira ya chaneli yako
Rahisisha utaratibu wa kazi kwa kuchagua mipangilio ya chaneli. Mipangilio hii itaathiri video zilizopo na za baadaye. Ukichagua kutoteua mipangilio fulani ya chaneli, utatakiwa kuthibitisha kila video kwenye chaneli yako inayolenga watoto. Mipangilio ya video mahususi itabatilisha mipangilio ya chaneli.
Hatua hii pia itazuia vipengele fulani kwenye chaneli yako. Iwapo huna uhakika kama video zako zinalenga watoto au la, angalia makala haya ya Kituo cha Usaidizi.
Kutoka kwenye akaunti yako ya Kidhibiti Maudhui cha Studio ya YouTube
Kumbuka: Akaunti yako unayotumia kuingia katika akaunti ya Kidhibiti Maudhui cha Studio ni sharti pia iweze kutumika kuingia katika akaunti ya chaneli yako unayotaka kusasisha.
- Ingia katika akaunti kwenye studio.youtube.com.
- Kwenye menyu ya kushoto, chagua Chaneli .
- Bofya chaneli unayotaka kusasisha. Ukurasa wa chaneli hiyo utafunguka.
- Bofya picha ya wasifu katika kona ya juu kulia chagua Studio ya YouTube.
- Kwenye menyu ya kushoto, chagua Mipangilio .
- Bofya Chaneli.
- Bofya kichupo cha Mipangilio ya Kina.
- Chini ya Hadhira, teua chaguo:
- "Ndiyo, bainisha kuwa chaneli hii inalenga watoto. Mimi hupakia maudhui ambayo yanalenga watoto."
- "Hapana, bainisha chaneli hii kuwa hailengi watoto. Huwa sipakii maudhui ambayo yanalenga watoto."
- "Ningependa kukagua mipangilio hii kwa kila video."
- Bofya HIFADHI.
Kutoka kwenye ukurasa wa chaneli yako ya Studio ya YouTube
- Ingia katika akaunti kwenye studio.youtube.com.
- Kwenye menyu ya kushoto, chagua Mipangilio .
- Bofya Chaneli.
- Bofya kichupo cha Mipangilio ya Kina.
- Chini ya Hadhira, teua chaguo:
- "Ndiyo, bainisha kuwa chaneli hii inalenga watoto. Mimi hupakia maudhui ambayo yanalenga watoto."
- "Hapana, bainisha chaneli hii kuwa hailengi watoto. Huwa sipakii maudhui ambayo yanalenga watoto."
- "Ningependa kukagua mipangilio hii kwa kila video."
- Bofya HIFADHI.
Weka hadhira yako wakati unapakia
- Ingia katika akaunti ya Studio ya YouTube.
- Katika kona ya juu kulia, bofya TAYARISHA Pakia video .
- Chagua faili ambayo ungependa kupakia.
- Kwenye ukurasa wa Maelezo, chini ya sehemu ya Hadhira, chagua moja:
- “Ndiyo, inalenga watoto".
- “Hapana, hailengi watoto”.
- Bofya INAYOFUATA ili uendelee na mchakato wa kupakia.
Baada ya kupakia video yako, itawekewa lebo kuwa “Inalenga watoto - uliyobainisha” kwenye ukurasa wako wa Maudhui.
Sasisha mipangilio ya hadhira kwenye video zilizopo
Huenda ukatambua kuwa YouTube tayari imebainisha video fulani kuwa “zinalenga watoto”. Kwa kuwa hujapata nafasi bado ya kubainisha video au chaneli kuwa inalenga watoto au la, utaweza kufanya hivyo sasa:
- Ingia katika akaunti ya Studio ya YouTube.
- Kwenye menyu ya kushoto, chagua Maudhui.
- Chagua visanduku karibu na video ambazo ungependa kubadilisha.
- Kumbuka: Unaweza kuchagua video zote kwa kuteua kisanduku kando ya “Video” katika sehemu ya juu ya orodha.
- Chagua Badilisha Hadhira.
- Chagua moja:
- “Ndiyo, inalenga watoto.”
- "Hapana, hailengi watoto."
- Chagua SASISHA VIDEO.
Kupakia video inayolenga watoto kwa kutumia violezo vya CSV
Ikiwa ungependa kutumia violezo vya CSV kupakia video kwa wingi, angalia makala haya ya Kituo cha Usaidizi.
Kupakia video inayolenga watoto kwa kutumia DDEX
Ikiwa wewe ni lebo ya muziki inayotumia DDEX kuwasilisha Video za Muziki au Video za Wavuti, angalia makala haya ya Kituo cha Usaidizi kwa maagizo kuhusu jinsi ya kujumuisha maudhui yanayolenga watoto katika mipasho yako.
Kupakia Video ya Picha kuwa inayolenga watoto
YouTube itatumia aina ya video ya picha kubaini iwapo video ya picha inalenga watoto. Angalia makala haya ya Kituo cha Usaidizi ili uone orodha ya aina zinazolenga watoto pamoja na jinsi ya kubainisha video ya picha kuwa hailengi watoto.
Kinachofuata unapobainisha maudhui yako kuwa yanalenga watoto
Maudhui yako yanapobainishwa kuwa "yanalenga watoto", tutadhibiti data tunayokusanya kuhusu maudhui hayo ili kutii sheria. Hii inamaanisha kuwa tutazima vipengele fulani kama vile maoni, arifa, na mengine.
La muhimu zaidi, hatutaonyesha matangazo yaliyowekewa mapendeleo kwenye maudhui yanayolenga watoto, kwa mujibu wa Sheria ya Ulinzi wa Faragha ya Watoto Mtandaoni (COPPA) na/au sheria nyingine zinazotumika. Kutoonyesha matangazo yaliyowekewa mapendeleo kwenye maudhui yanayolenga watoto kunaweza kupunguza mapato kwa baadhi ya watayarishi ambao hubainisha maudhui yao kuwa yanalenga watoto. Tunatambua kuwa hali hii si rahisi kwa baadhi ya watayarishi, lakini ni muhimu kuchukua hatua hizi ili kuhakikisha kuwa tunatii sheria ya COPPA na sheria nyingine zinazotumika.
Orodha ya vipengele vitakavyoathiriwa inapatikana hapa chini:
Ukibainisha kuwa video au mtiririko mubashara unalenga watoto
- Utangazaji uliowekwa mapendeleo
- Maoni
- Kutia alama ya chapa kwenye chaneli
- Kitufe cha kuchanga
- Kadi au skrini za mwisho
- Gumzo la moja kwa moja au michango ya gumzo la moja kwa moja
- Kengele ya arifa
- Kucheza ukitumia Kichezaji kidogo
- Super Chat au Super Stickers
- Kuhifadhi kwenye orodha ya video
Kumbuka: Kitufe cha "jiunge" kwenye uanachama katika chaneli na rafu ya bidhaa havitapatikana kwenye maudhui yaliyobainishwa kuwa yanalenga watoto.
Ukibainisha chaneli yako kuwa inalenga watoto
- Hadithi
- Kichupo cha jumuiya kwenye Ukurasa wa chaneli
- Kengele ya arifa
- Uanachama katika Chaneli
Frequently Asked Questions
What happens if I set my video’s audience incorrectly?
How do I know if I’ve set my video’s audience correctly?
- Nenda kwenye studio.youtube.com.
- Kwenye menyu ya kushoto, chagua Maudhui.
- Nenda kwenye video ambayo ungependa kuhariri na ubofye kijipicha.
- Chini ya Hadhira, chagua “Hapana, hailengi watoto”.
Kama tayari umebainisha hadhira ya video yako na YouTube itambue hitilafu au matumizi mabaya, utaona video yako ikiwa na alama ya "Inalenga watoto - Imewekwa na YouTube". Hutaweza kubadilisha mipangilio yako ya hadhira. Iwapo hukubali, unaweza kutumia kitufe cha "Tuma Moani".
- Kwenye kompyuta, nenda kwenye studio.youtube.com.
- Kwenye menyu ya kushoto, chagua Maudhui.
- Bofya video ambayo ungependa kutuma maoni kuihusu.
- Bofya Tuma maoni.