Tumia kipengele cha kuweka video katika foleni ili uweke mipangilio ya video zitakazocheza baada ya video unayotazama bila kukatiza kipindi chako cha sasa cha kutazama. Pata maelezo kuhusu jinsi ya kuweka video katika foleni kwenye kompyuta ya mezani au wavuti au ujiunge na YouTube Premium ili utumie kipengele hiki katika vifaa vyako vya mkononi na vishikwambi.
Jinsi ya kuongeza video kwenye foleni katika kompyuta yako
Fuatilia Chaneli ya Watazamaji wa YouTube ili upate habari, taarifa na vidokezo vipya.
Ili uweke video kwenye foleni katika kompyuta yako, unaweza:
- Kutafuta video ambayo ungependa kuweka kwenye foleni yako.
- Bofya Zaidi karibu na jina la video.
- Chagua Weka kwenye foleni .
Au unaweza:
- Kutafuta video ambayo ungependa kuweka kwenye foleni yako.
- Wekelea kiashiria kwenye video.
- Chagua 'Weka kwenye foleni' .
Kumbuka: Foleni yako haitahifadhiwa ukishafunga kivinjari chako. Iwapo ungependa kuendelea kutazama baadaye, tunapendekeza uhifadhi video kwenye orodha yako ya Tazama Baadaye.
Ili uhifadhi foleni yako kwenye orodha:
- Fungua foleni yako.
- Bofya Zaidi chagua Hifadhi kwenye orodha.
- Chagua orodha iliyopo kama vile Tazama Baadaye, orodha ambayo tayari umetayarisha au ubofye Orodha mpya .
- Iwapo unatayarisha orodha mpya, weka jina kisha uchague mipangilio ya faragha ya orodha yako kwenye menyu kunjuzi ya Uonekanaji bofya Tayarisha.
Kumbuka: Ikiwa ni ya faragha, ni wewe tu unayeweza kuona orodha hiyo.
- Ujumbe utaibuka katika sehemu ya chini ya skrini yako ukithibitisha orodha ambako foleni imewekwa.