Ripoti utozaji ambao haujaidhinishwa

Ukiona utozaji kwenye kadi au taarifa yako ya benki kuhusu ununuzi dijitali kwenye YouTube ambao hukufanya, unaweza kuripoti utozaji huo kwa timu yetu ya usaidizi ndani ya siku 120 tangu muamala ulipofanyika.

Hatua ya 1: Tambua gharama za YouTube

Ununuzi wote wa YouTube utaonekana kwenye taarifa yako kama GOOGLE*YouTube [service name]. Kwa mfano, gharama ya YouTube TV itaonekana kama GOOGLE*YouTube TV.

Ikiwa gharama husika haiko kwenye mojawapo wa miundo hii, basi haikutoka kwenye YouTube. Wasiliana na benki au kampuni iliyotoa kadi yako kwa maelezo zaidi.

Hatua ya 2: Wasiliana na familia na marafiki zako

Ikiwa hutambui muamala wa YouTube, wasiliana na familia na marafiki zako ili kuona iwapo:

  • Walifanya ununuzi au
  • Huenda mtoto alicheza mchezo ambao ulisababisha gharama isiyokusudiwa

Ukigundua kuwa gharama haikuidhinishwa na haikukusudiwa lakini si tukio la ulaghai, unaweza kutuma ombi la kurejeshewa pesa.

Hatua ya 3: Wasilisha na ufuatilie dai lako

Baada ya kuthibitisha kuwa utozaji huo umetoka YouTube na haukufanywa na mtu yeyote unayemjua, ripoti utozaji huo kwa timu yetu ya usaidizi ndani ya siku 120 tangu muamala ulipofanyika. Ili kupata dai lako, unahitaji anwani ya barua pepe uliyotumia kuwasilisha dai na kitambulisho cha dai kilichotumwa kwenye barua pepe yako.

Je, maelezo haya yamekufaa?

Tunawezaje kuboresha?
Tafuta
Futa utafutaji
Funga kisanduku cha kutafutia
Menyu kuu
2257058572105365753
true
Tafuta kwenye Kituo cha Usaidizi
true
true
true
true
true
59
false
false