Kubainisha hadhira ya chaneli au video yako

Bila kujali mahali ulipo, unatakiwa kisheria kutii Sheria ya Kulinda Faragha ya Watoto Mtandaoni na/au sheria zingine. Unatakiwa kutueleza kwamba video zako zinalenga watoto ikiwa unatayarisha maudhui yanayolenga watoto.

Kama mtayarishi wa YouTube, unahitajika kubainisha video zijazo au zilizopo kuwa zinalenga watoto au haziwalengi. Hata watayarishi wasiotayarisha maudhui ya watoto wanapaswa kubainisha hadhira lengwa. Hatua hii itasaidia kuhakikisha kuwa tunatoa vipengele vinavyoendana na maudhui yako.

Important Update for All Creators: Complying with COPPA

Ili kukusaidia kutii, kuna mipangilio ya hadhira ya maudhui yanayolenga watoto kwenye Studio ya YouTube. Unaweza kubainisha hadhira yako:

  • Katika kiwango cha chaneli ili uteuzi wako ubainishe maudhui yaliyopo au utakayopakia baadaye kuwa yanalenga watoto au la.
  • Au katika kiwango cha video. Ukiteua chaguo hili, utahitaji kubainisha kila video iliyopo na utakayopakia baadaye kuwa inalenga watoto au la.

Kumbuka:

  • Tutafanya zana ya kuteua hadhira ipatikane kwenye programu za wengine na Huduma za API za YouTube hivi karibuni. Kwa sasa, tafadhali tumia Studio ya YouTube ili upakie maudhui yanayolenga watoto.

Kidokezo Muhimu: Umuhimu wa kila mtayarishi kubainisha hadhira yake

Mabadiliko haya yanahitajika kama sehemu ya makubaliano na Tume ya Biashara ya Marekani (FTC) na Mwanasheria Mkuu wa New York na yatakuwezesha kutii Sheria ya Kulinda Faragha ya Watoto Mtandaoni (COPPA) na/au sheria zingine husika. Bila kuzingatia mahali uliko, tunahitaji utueleze iwapo video zako zinalenga watoto au haziwalengi. Iwapo hutabainisha hadhira yako kwa njia sahihi, huenda ukapata matatizo ya ukiukaji wa sheria kwa mujibu wa FTC au mamlaka mengine na huenda tukachukua hatua dhidi ya akaunti yako ya YouTube. Pata maelezo zaidi kuhusu jinsi FTC hutekeleza COPPA.

Madokezo machache:
  • Tunatumia mfumo wa mashine kujifunza ili kutuwezesha kutambua video zinazowalenga watoto moja kwa moja. Tunaamini kuwa utabainisha hadhira yako kwa njia sahihi lakini tunaweza kubatilisha chaguo la mipangilio ya hadhira yako katika hali ambapo umekosea au ikiwa kuna matumizi mabaya.
  • Usitegemee mifumo yetu kubainisha hadhira kwa niaba yako kwa sababu huenda ikashindwa kutambua maudhui ambayo FTC au mamlaka mengine yanachukulia kuwa yanalenga watoto.
  • Ikiwa unahitaji usaidizi kubaini iwapo maudhui yako yanalenga watoto au la, angalia makala haya ya Kituo cha Usaidizi au uwasiliane na mshauri wa kisheria.
  • Video unazobainisha kuwa “zinalenga watoto” zina uwezekano mkubwa wa kupendekezwa pamoja na video nyingine za watoto.
  • Ikiwa tayari umebainisha hadhira ya video yako na YouTube itambue kosa au matumizi mabaya, unaweza kuona video yako ikiwa na alama ya “Inalenga Watoto". Hutaweza kubadilisha mipangilio yako ya hadhira. Iwapo unafikiri kuwa tumefanya kosa, unaweza kukata rufaa.

Kuweka hadhira ya chaneli yako

Rahisisha utaratibu wa kazi kwa kuchagua mipangilio ya chaneli. Mipangilio hii itaathiri video zilizopo na za baadaye. Ukichagua kutoteua mipangilio fulani ya chaneli, utatakiwa kuthibitisha kila video kwenye chaneli yako inayolenga watoto. Mipangilio ya video mahususi itabatilisha mipangilio ya chaneli.
Hatua hii pia itazuia vipengele fulani kwenye chaneli yako. Iwapo huna uhakika kama video zako zinalenga watoto au la, angalia makala haya ya Kituo cha Usaidizi.
  1. Ingia katika akaunti kwenye studio.youtube.com (Studio ya wavuti pekee).
  2. Kwenye menyu ya kushoto, bofya Mipangilio.
  3. Bofya Chaneli.
  4. Bofya kitufe cha Mipangilio ya Kina
  5. Chini ya sehemu ya Hadhira, chagua:
    1. "Ndiyo, weka kuwa chaneli hii inalenga watoto. Mimi hupakia maudhui ambayo yanalenga watoto."
    2. "Hapana, bainisha chaneli hii kuwa hailengi watoto. Sipakii maudhui ambayo yanalenga watoto."
    3. "Ningependa kukagua mipangilio hii kwa kila video." 
  6. Bofya Hifadhi.
Kuweka hadhira ya video yako
Unaweza kuweka video mahususi kuwa zinalenga watoto. Hili ni chaguo nzuri iwapo ni baadhi tu ya video zako zinalenga watoto. Iwapo huna uhakika ikiwa maudhui yako yanalenga watoto au la, angalia makala haya ya Kituo cha Usaidizi

Weka hadhira yako wakati unapakia

  1. Nenda kwenye studio.youtube.com. Kumbuka: ili uweke hadhira yako kuwa inalenga watoto, unahitaji kutumia Studio ya YouTube. Hutaweza kufanya hivyo katika Studio ya Watayarishi ya Kawaida. 
  2. Kwenye kona ya juu kulia, bofya aikoni ya kupakia. 
  3. Bofya Pakia video (Beta). Usipoona hii, bofya Pakia video. 
  4. Kwenye kichupo cha Maelezo ya msingi, nenda katika Hadhira
  5. Chagua:
    • “Ndiyo, inalenga watoto".
    • “Hapana, hailengi watoto”
  6. Bofya Inayofuata ili uendelee kupakia maudhui yako. 

Baada ya kupakia video yako, itawekewa lebo kuwa “Inalenga watoto - uliyoweka” kwenye orodha yako ya Upakiaji

Kusasisha mipangilio ya hadhira kwenye video zilizopo

Huenda ukatambua kuwa YouTube tayari imebainisha video fulani kuwa “zinalenga watoto”. Kwa kuwa hujapata nafasi bado ya kubainisha video au chaneli kuwa inalenga watoto au la, utaweza kufanya hivyo sasa:

  1. Ingia katika akaunti kwenye studio.youtube.com.
  2. Kwenye menyu ya kushoto, chagua Maudhui.
  3. Chagua visanduku karibu na video ambazo ungependa kubadilisha. Kumbuka: Unaweza kuchagua video zako zote kwa kuteua kisanduku kando ya “Video” katika sehemu ya juu ya orodha yako ya upakiaji. 
  4. Chagua Badilisha kisha Hadhira kisha “Ndiyo, inalenga watoto.”
  5. Chagua SASISHA VIDEO.
Madokezo machache: 
  • Tunatumia mfumo wa mashine kujifunza ili kutuwezesha kutambua video ambazo dhahiri zinalenga hadhira za watoto. Tunaamini kuwa utaweka hadhira yako kwa usahihi lakini tunaweza kubatilisha chaguo la mipangilio ya hadhira yako katika hali ambapo umekosea au ikiwa kuna matumizi mabaya. 
  • Usitegemee mifumo yetu kuweka hadhira kwa niaba yako kwa sababu huenda ikashindwa kutambua maudhui ambayo FTC au mamlaka nyingine huchukulia kuwa yanalenga watoto. 
  • Ikiwa unahitaji usaidizi kubaini iwapo maudhui yako yanalenga watoto au la, angalia makala haya ya Kituo cha Usaidizi au uwasiliane na mshauri wa kisheria.
  • Video unaweka kuwa “zinalenga watoto” zina uwezekano mkubwa wa kupendekezwa pamoja na video nyingine za watoto. 
  • Ikiwa tayari umebainisha hadhira ya video yako na YouTube itambue kosa au matumizi mabaya, unaweza kuona video yako ikiwa na alama ya “Inalenga Watoto". Hutaweza kubadilisha mipangilio yako ya hadhira. Iwapo unafikiri kuwa tumefanya kosa, unaweza kukata rufaa.

Weka hadhira ya mtiririko wako mubashara

Weka hadhira yako unapoanzisha mtiririko mubashara

Iwapo huna uhakika ikiwa maudhui yako yanalenga watoto au la, angalia makala haya ya Kituo cha Usaidizi

  1. Nenda kwenye studio.youtube.com.
  2. Kwenye kona ya juu kulia, bofya aikoni ya kupakia.
  3. Bofya Tiririsha mubashara. Kumbuka: Kubofya huku kutakutuma kwenyeUkurasa wa kudhibiti utiririshaji wa moja kwa moja. Hutaweza kuweka hadhira ya mtiririko wako mubashara ukitumia zana zetu za Kawaida za kutiririsha mubashara, kwa hivyo utahitaji kufanya hivyo ukitumia Ukurasa wa kudhibiti utiririshaji wa moja kwa moja.
  4. Baada ya kujaza maelezo ya msingi na kuchagua mpangilio wa faragha, nenda kwenyeHadhira
  5. Chagua:
    • “Ndiyo, inalenga watoto”.
    • "Hapana, hailengi watoto".
  6. Bofya Inayofuata ili uendelee kuweka mipangilio ya mtiririko wako mubashara.

Sasisha mipangilio ya hadhira kwenye mitiririko mubashara iliyohifadhiwa kwenye kumbukumbu

Huenda ukatambua kuwa YouTube tayari imeweka mitiririko mubashara fulani iliyohifadhiwa kwenye kumbukumbuku kuwa “inalenga watoto”. Kwa kuwa hujapata nafasi bado ya kuweka mitiririko yako mubashara iliyohifadhiwa kwenye kumbukumbukua kuwa inalenga watoto au la, utaweza kufanya hivyo sasa:

  1. Ingia katika akaunti kwenye studio.youtube.com.
  2. Kwenye menyu ya kushoto, chagua Maudhui.
  3. Bofya kichupo cha Mubashara.
  4. Chagua visanduku karibu na video ambazo ungependa kubadilisha. Kumbuka: Unaweza kuchagua video zako zote kwa kuteua kisanduku kando ya "Mtiririko mubashara" katika sehemu ya juu ya orodha. 
  5. Chagua Badilisha kisha Hadhira kisha “Ndiyo, inalenga watoto" ikiwa ni maudhui ya watoto. Au chagua “Hapana, hailengi watoto” ikiwa si maudhui ya watoto.
  6. Chagua SASISHA VIDEO.
Madokezo machache
  • Tunatumia mfumo wa mashine kujifunza ili kutuwezesha kutambua video ambazo dhahiri zinalenga hadhira za watoto. Tunaamini kuwa utaweka hadhira yako kwa usahihi lakini tunaweza kubatilisha chaguo la mipangilio ya hadhira yako katika hali ambapo umekosea au ikiwa kuna matumizi mabaya. 
  • Usitegemee mifumo yetu kuweka hadhira kwa niaba yako kwa sababu huenda ikashindwa kutambua maudhui ambayo FTC au mamlaka nyingine huchukulia kuwa yanalenga watoto. 
  • Ikiwa unahitaji usaidizi kubaini iwapo maudhui yako yanalenga watoto au la, angalia makala haya ya Kituo cha Usaidizi au uwasiliane na mshauri wa kisheria.
  • Video unazobainisha kuwa “zinalenga watoto” zina uwezekano mkubwa wa kupendekezwa pamoja na video nyingine za watoto.
  • Ikiwa tayari umebainisha hadhira ya video yako na YouTube itambue kosa au matumizi mabaya, unaweza kuona video yako ikiwa na alama ya “Inalenga Watoto". Hutaweza kubadilisha mipangilio yako ya hadhira. Iwapo unafikiri kuwa tumefanya kosa, unaweza kukata rufaa.

Kinachofuata unapobainisha maudhui yako kuwa yanalenga watoto

Tunaweka mipaka ya ukusanyaji na utumiaji wa data kwenye maudhui yanayolenga watoto ili kutii sheria. Hatua hii inamaanisha kuwa tunahitaji kudhibiti au kuzima baadhi ya vipengele kama vile maoni, arifa na vinginevyo.

La muhimu zaidi, hatuonyeshi matangazo yaliyowekewa mapendeleo kwenye maudhui yanayolenga watoto, kwa mujibu wa Sheria ya Ulinzi wa Faragha ya Watoto Mtandaoni (COPPA) na/au sheria nyingine zinazotumika. Kutoonyesha matangazo yaliyowekewa mapendeleo kwenye maudhui yanayolenga watoto kunaweza kupunguza mapato kwa baadhi ya watayarishi ambao hubainisha maudhui yao kuwa yanalenga watoto. Tunatambua kuwa hali hii si rahisi kwa baadhi ya watayarishi, lakini ni muhimu kuchukua hatua hizi ili kuhakikisha kuwa tunatii sheria ya COPPA na sheria nyingine zinazotumika.

Orodha ya vipengele vitakavyozimwa inapatikana hapa chini:

Ukibainisha kuwa video au mtiririko mubashara unalenga watoto

Unapobainisha hadhira yako kuwa "inalenga watoto", tutazuia vipengele fulani ili kutii sheria ya Ulinzi wa Faragha ya Watoto Mtandaoni (COPPA) na sheria zingine husika. Hili likitokea, vipengele vifuatavyo havitapatikana kwenye video au mtiririko mubashara mahususi:

  • Kucheza kiotomatiki kwenye ukurasa wa kwanza
  • Kadi na skrini za mwisho
  • Alama maalum za video
  • Uanachama Katika Chaneli
  • Maoni
  • Kitufe cha kuchanga
  • Alama za Nimeipenda na Sijaipenda kwenye YouTube Music
  • Michango ya gumzo la moja kwa moja au magumzo ya moja kwa moja
  • Bidhaa na vipengele vya tiketi
  • Kengele ya arifa
  • Utangazaji uliowekewa mapendeleo
  • Uchezaji katika Kichezaji Kidogo
  • Super Chat au Super Stickers
  • Kuhifadhi kwenye orodha ya video na Kuhifadhi ili utazame baadaye
Ukibainisha kuwa chaneli yako inalenga watoto

Kama chaneli yako inalenga watoto, video au mitiririko yako mubashara haitakuwa na kipengele chochote kati ya vilivyotajwa hapo juu. Chaneli yako pia haitakuwa na vipengele vifuatavyo: 

  • Uanachama Katika Chaneli
  • Kengele ya arifa
  • Machapisho

Maswali Yanayoulizwa Sana

Kwa nini vipengele vya arifa, maoni na vinginevyo huzimwa kwenye maudhui yaliyobainishwa kuwa yanalenga watoto?

Ili kutii Sheria ya Kulinda Faragha ya Watoto Mtandaoni (COPPA) na sheria zingine zinazotumika, tunaweka mipaka ya ukusanyaji data kwenye maudhui yaliyobainishwa kuwa yanalenga watoto. Kutokana na hayo, baadhi ya vipengele vinaweza kudhibitiwa au kuzimwa kwenye maudhui haya, ikijumuisha arifa na maoni.

Itakuwaje iwapo nimebainisha hadhira ya video yangu kwa njia isiyo sahihi?

Mabadiliko haya yanahitajika kama sehemu ya makubaliano na Tume ya Biashara ya Marekani (FTC) na Mwanasheria Mkuu wa New York na yatakuwezesha kutii Sheria ya Kulinda Faragha ya Watoto Mtandaoni (COPPA) na/au sheria zingine husika. Bila kuzingatia mahali uliko, tunahitaji utueleze iwapo video zako zinalenga watoto au haziwalengi. Usipobainisha hadhira yako kwa usahihi, huenda ukakumbwa na matatizo ya ukiukaji wa sheria za FTC au mamlaka zingine, na tunaweza kuchukua hatua dhidi ya akaunti yako ya YouTube. Pata maelezo zaidi kuhusu jinsi FTC hutekeleza COPPA.

Kidokezo: Tutatumia pia mfumo wa mashine kujifunza ili kutuwezesha kubaini video zinazowalenga watoto moja kwa moja. Tunaamini kuwa utabainisha hadhira yako kwa njia sahihi lakini tunaweza kubatilisha chaguo la mipangilio ya hadhira yako katika hali ambapo umekosea au ikiwa kuna matumizi mabaya. Hata hivyo, usitegemee mifumo yetu ibainishe hadhira kwa niaba yako kwa sababu mifumo yetu inaweza kukosa kubaini maudhui ambayo FTC au mamlaka mengine huchukulia kuwa yanalenga watoto. Usipobainisha maudhui yako kwa usahihi kuwa yanalenga watoto, huenda ukachukuliwa hatua za kisheria au ukachukuliwa hatua kwenye YouTube. Ikiwa unahitaji usaidizi kubaini iwapo maudhui yako yanalenga watoto au la, angalia makala haya ya Kituo cha Usaidizi au uwasiliane na mshauri wa kisheria.

Je, nitajuaje kuwa nimebainisha hadhira ya video yangu kwa usahihi?

Tunasikitika kuwa hatuwezi kukupa mwongozo kuhusu iwapo umebainisha kwa usahihi hadhira lengwa kuwa watoto, lakini FTC imetoa mwongozo kuhusu maana ya kulenga watoto (au "yanalenga watoto"). Kwa sasa, FTC inazingatia masasisho mbalimbali kwenye COPPA, hali ambayo huenda ikatoa mwongozo zaidi kuhusu tatizo hili.

Tutatumia pia mifumo ya mashine kujifunza ili kutusaidia kugundua maudhui yanayolenga watoto moja kwa moja. Lakini tafadhali usitegemee mifumo yetu kubainisha maudhui yako -- kama ilivyo kwa mifumo yote ya kiotomatiki, mifumo yetu huenda ikawa na hitilafu zake. Huenda tukahitaji kubatilisha mipangilio yako ya hadhira tukigundua kuwa umekosea au ikiwa kuna matumizi mabaya. Lakini mara nyingi, tutategemea mipangilio yako ya hadhira kubaini ikiwa video inalenga watoto.

Iwapo hujabainisha hadhira lengwa kuwa watoto; na FTC au mamlaka mengine yanafikiri kuwa maudhui husika yanafaa kubainishwa kuwa yanalenga watoto, unaweza kuchukuliwa hatua za kisheria. Kwa hivyo soma makala haya ya Kituo cha Usaidizi au upate ushauri wa kisheria ikiwa huna uhakika kuhusu iwapo maudhui yako yanapaswa kubainishwa kuwa yanalenga watoto.

Nitafanyaje iwapo YouTube inasema kuwa video yangu inalenga watoto, lakini sikubali maelezo hayo?

Iwapo bado hujabainisha hadhira ya video yako: Huenda YouTube tayari imebainisha hadhira yako kwa niaba yako. Hatua hii inakusaidia utii sheria ya COPPA na/au sheria nyingine zinazotumika. Hata hivyo, ikiwa hukubaliani na jinsi YouTube ilivyobainisha maudhui yako, mara nyingi bado unaweza kubadilisha mipangilio ya hadhira ya video yako.

Iwapo tayari umebainisha hadhira ya video yako: na YouTube itambue kosa au matumizi mabaya, unaweza kuona video yako ikiwa na alama ya “Inalenga Watoto.” Hali hii ikitokea, hutaweza kubadilisha mipangilio ya hadhira yako.

Hata hivyo tunafahamu kuwa wakati mwingine tunakosea. Iwapo unafikiri kuwa tumekosea, unaweza kukata rufaa dhidi ya uamuzi huu.

 Ili uanzishe mchakato wa kukata rufaa kwenye kompyuta yako:

  1. Kwenye kompyuta, nenda katika studio.youtube.com.
  2. Kwenye menyu ya kushoto, chagua Maudhui.
  3. Nenda kwenye video ambayo ungependa kukatia rufaa.
  4. Wekelea kiashiria juu ya “Bainisha kuwa inalenga watoto” na ubofye Kata rufaa.
  5. Weka sababu yako ya kukata rufaa kisha ubofye Wasilisha.

Ili uanzishe mchakato wa kukata rufaa kwenye simu yako:

  1. Fungua programu ya Studio ya YouTube.
  2. Gusa Menyu kisha Video.
  3. Kwenye kichupo cha Zilizopakiwa, gusa video unayotaka kuikatia rufaa.
  4. Katika mipangilio ya Vizuizi, gusa Bainisha kuwa Inalenga Watoto.
  5. Gusa Kata Rufaa na uweke sababu yako ya kukata rufaa.
  6. Gusa Wasilisha.

Ukishawasilisha rufaa

Utapokea barua pepe kutoka YouTube inayokufahamisha matokeo ya ombi lako la kukata rufaa. Mojawapo kati ya yafuatayo litafanyika:

  • Rufaa yako ikikubaliwa, tutaondoa mipangilio ya hadhira ya “inalenga watoto”.
  • Rufaa yako ikikataliwa, mipangilio ya hadhira ya “inalenga watoto” itasalia kwenye maudhui yako. Kuanzia sasa, tafadhali kagua mipangilio ya hadhira ya chaneli na/au video yako mahususi. Kushindwa kubainisha hadhira yako ipasavyo kunaweza kusababisha kuchukuliwa hatua za kisheria kwa mujibu wa COPPA na/au sheria zingine au hatua kwenye mfumo wa YouTube.

Unaweza kukatia rufaa kila video mara moja tu.

Je, maelezo haya yamekufaa?

Tunawezaje kuboresha?
Tafuta
Futa utafutaji
Funga kisanduku cha kutafutia
Menyu kuu
15400382784802137174
true
Tafuta kwenye Kituo cha Usaidizi
true
true
true
true
true
59
false
false