Kuchagua mipangilio ya maoni

Unaweza kubadilisha mipangilio yako ya maoni kwenye Studio ya YouTube au kwenye ukurasa wa kutazama wa programu ya YouTube. Pata maelezo kuhusu mipangilio mbalimbali ya maoni.

YouTube Comments: Replying, Filtering and Moderating

Huwezi kubadilisha mipangilio ya maoni ikiwa:

Kubadilisha mipangilio yako ya maoni chaguomsingi

Mipangilio yako chaguomsingi ya maoni hutumika kwenye video na Machapisho mapya ya jumuiya. Video na Machapisho ya jumuiya yaliyopo hayataathiriwa.

Ili kubadilisha mipangilio ya maoni kwenye Studio ya YouTube:

  1. Ingia katika akaunti ya Studio ya YouTube.
  2. Kwenye menyu ya kushoto, chagua Mipangilio.
  3. Chagua Jumuiya kisha Mipangilio chaguomsingi.
  4. Chagua mipangilio yako chaguomsingi chini ya "Maoni kwenye chaneli yako."
  5. Chagua Hifadhi.

Kubadilisha mipangilio ya maoni kwenye video

Unaweza kubadilisha mipangilio ya maoni katika video mahususi kutoka kwenye ukurasa wako wa Maudhui. Unaweza pia kubadiliisha mipangilio ya maoni kwa zaidi ya video moja kwa wakati mmoja ukitumia kihariri cha vipengee vingi.

  1. Ingia katika akaunti ya Studio ya YouTube.
  2. Kwenye menyu ya kushoto, chagua Maudhui.
  3. Bofya kijipicha cha video.
  4. Nenda kishabofya ONYESHA ZAIDI.
  5. Chini ya “Maoni na ukadiriaji," chagua mipangilio yako ya maoni.
  6. Bofya Hifadhi.

Pia unaweza:

  1. Kuingia katika akaunti kwenye programu ya YouTube kwenye kifaa chako cha mkononi.
  2. Nenda kwenye mojawapo ya video zako.
  3. Gusa Maoni chini ya video au upande wa kulia wa Video yako Fupi ya YouTube.
  4. Gusa Mipangilio .
  5. Gusa Maoni chini ya Kwenye video hii ili ubadilishe mipangilio.
Pata maelezo zaidi kuhusujinsi ya kubadilisha mipangilio ya maoni kwenye Machapisho yako ya jumuiya.

Kubadilisha mwonekano chaguomsingi wa maoni

Unaweza kubadilisha jinsi maoni yanavyopangwa kwenye ukurasa wako wa kutazama video. Unaweza kupanga maoni kulingana na maoni maarufu au tarehe yalipowekwa.

  1. Ingia katika akaunti ya Studio ya YouTube.
  2. Kwenye menyu ya kushoto, chagua Maudhui.
  3. Bofya kijipicha cha video.
  4. Nenda kishabofya ONYESHA ZAIDI.
  5. Chini ya “Maoni na ukadiriaji," chagua Panga kulingana na.
  6. Chagua kati ya Maarufu na Mapya zaidi.
  7. Bofya Hifadhi.

Je, maelezo haya yamekufaa?

Tunawezaje kuboresha?
Tafuta
Futa utafutaji
Funga kisanduku cha kutafutia
Menyu kuu
14757325734226746543
true
Tafuta kwenye Kituo cha Usaidizi
true
true
true
true
true
59
false
false