Kutafuta video kwa kutamka

Tafuta video ukitumia kipengele cha kutafuta kwa kutamka.

Pata maelezo kuhusu kudhibiti rekodi zako za sauti ukitumia kipengele cha kutafuta kwa kutamka kwenye YouTube.

Anza kutafuta kwa kutamka

  1. Ingia katika akaunti kwenye YouTube.
  2. Gusa Tafuta .
  3. Gusa Maikrofoni .
  4. Ruhusu ufikiaji wa maikrofoni.
  5. Itaanza kurekodi mara moja.
  6. Gusa  ili umalize kurekodi.
  7. Gusa X ili urudi nyuma au ughairi kurekodi.

Badilisha ruhusa za maikrofoni

  1. Ikiwa ulikataa kutoa ruhusa za maikrofoni awali, unaweza kuona ombi la kutoa ruhusa za maikrofoni kupitia mipangilio ya simu yako.
  2. Bofya kidokezo ili uende kwenye mipangilio ya simu, au fikia Mipangilio ya Android kwenye menyu ya jumla ya simu yako ya Android.
  3. Kutoka mipangilio ya Android, bofya Programu na Arifa.
  4. Tafuta programu ya YouTube na ubofye mipangilio ya YouTube.
  5. Bofya Ruhusa.
  6. Geuza ruhusa ya maikrofoni iwe Imewashwa.
  7. Rudi kwenye programu ya YouTube, na unapaswa sasa kuweza kutafuta ukitumia sauti yako.

Njia zaidi unazoweza kutumia sauti yako

Amri hizi kwa sasa zinapatikana kwenye Android pekee na baadhi huenda zisipatikane katika kila lugha.

Kutafuta wimbo

Unaweza kutafuta kwenye YouTube kwa kutumia sauti. Kwa kuimba au kurekodi wimbo unaochezwa sasa, unaweza kutafuta video za YouTube, Video Fupi na maudhui rasmi ya muziki yanayohusiana. 
Ili kuanza kutafuta wimbo: 
  1. Ingia katika akaunti kwenye YouTube.
  2. Gusa Tafuta .
  3. Gusa Maikrofoni .
  4. Ruhusu ufikiaji wa maikrofoni.
  5. Gusa Wimbo .
  6. Kurekodi kutaanza mara moja na kumalizika mara tu wimbo utakapotambuliwa. 
  7. Gusa X ili urudi nyuma au ughairi kurekodi.
Kumbuka: Ikiwa wimbo hauwezi kutambuliwa, utapata ujumbe wa hitilafu kukujulisha kuwa wimbo unaolingana haukupatikana.

Kutazama au kusikiliza maudhui mahususi

  • Nenda moja kwa moja kwenye video au wimbo wowote: “Cheza muziki.”
  • Cheza video au muziki kutoka kwa msanii mahususi: “Cheza nyimbo za Ariana Grande.”
  • Cheza video au muziki wa aina mahususi: “Cheza muziki wa heavy metal.”
  • Cheza video au muziki kulingana na jinsi unavyojisikia: “Cheza muziki tulivu.”
  • Cheza video kutoka kwenye orodha yako ya unazopendekezewa: “Cheza video zinazopendekezwa.”

Nenda kwenye ukurasa mahususi kwenye YouTube

  • Nenda kwenye vituo unavyofuatilia: “Nionyeshe vituo ninavyofuatilia”, pia “Ni nini kipya kutoka kwenye vituo ninavyofuatilia?”
  • Nenda kwenye historia ya video ulizotazama: “Nionyeshe historia yangu ya video nilizotazama.”
  • Nenda kwenye maktaba yako: ”Nionyeshe maktaba yangu.”
  • Nenda kwenye vipakiwa vya hivi karibuni vya mtayarishi: ”Nionyeshe video za hivi karibuni kutoka TeamYouTube.”
  • Nenda kwenye video zinazohusiana kulingana na video unayotazama sasa: ”Onyesha video zinazohusiana.”
  • Pata bahati ya video mpya: ”Nini kipya kwenye YouTube?”

Je, maelezo haya yamekufaa?

Tunawezaje kuboresha?
Tafuta
Futa utafutaji
Funga kisanduku cha kutafutia
Menyu kuu
13086520975175632977
true
Tafuta kwenye Kituo cha Usaidizi
true
true
true
true
true
59
false
false