Desturi bora za kutayarisha maudhui yanayofaa watangazaji

Ikiwa umejiunga kwenye Mpango wa Washirika wa YouTube na ungependa kuchuma mapato kupitia matangazo, hakikisha kuwa maudhui yako yanafuata mwongozo wetu wa maudhui yanayofaa watangazaji

Maudhui yote lazima yafuate mwongozo

Tunazingatia vipengele vyote vya maudhui yako. Tunapozungumzia maudhui, tunamaanisha:

  • Video, Video fupi au maudhui ya mtiririko mubashara
  • Mada
  • Kijipicha
  • Maelezo
  • Lebo

Ili kufaa kwa matangazo, maudhui yako yote lazima yafuate mwongozo wetu wa maudhui yanayofaa watangazaji.

Kuweka muktadha kwenye video zako

Muktadha ni muhimu. Ikiwa kuna thamani ya elimu, hali halisi, sayansi au sanaa, inaweza kubadilisha ufaafu wa video kwa watangazaji. Kwa mfano, ikiwa unaonyesha jinsi ya kutumia dawa ya kokeini ili “kulewa,” hiyo haifai kwa matangazo, kwa hivyo hupaswi kuwasha matangazo kwenye video hiyo. Lakini, ikiwa video yako inaonyesha dawa ya kokeini ikitumiwa kama sehemu ya utaratibu wa matibabu, inaweza kukubaliwa kwa baadhi ya watangazaji. 

Kuongeza muktadha pia hutusaidia kufanya uamuzi sahihi wa uchumaji wa mapato. Mifumo yetu si sahihi kila wakati. Ikiwa mifumo yetu itabainisha video yako kama isiyofaa kwa watangazaji wote, unaweza kuomba ikaguliwe na binadamu. Wakaguzi wetu binadamu watatathmini maudhui na muktadha wako ili kufanya uamuzi wa mwisho wa uchumaji wa mapato. 

Pata maelezo zaidi kuhusu jinsi wakaguzi hutathmini maudhui kwa kutumia mwongozo wetu wa maudhui yanayofaa watangazaji. 

Zima matangazo kwa maudhui yasiyofaa watangazaji

Ikiwa ungependa kupakia maudhui yasiyofuata mwongozo wetu wa maudhui yanayofaa watangazaji, unapaswa kuzima matangazo kwenye video mahususi. Chaguo hili linakuruhusu kujiondoa kwenye mpango wa uchumaji wa mapato katika video zozote ambazo hazifai watangazaji unapoendelea kutumia Mpango wa Washirika wa YouTube.

Je, maelezo haya yamekufaa?

Tunawezaje kuboresha?
Tafuta
Futa utafutaji
Funga kisanduku cha kutafutia
Menyu kuu
17931160392713770512
true
Tafuta kwenye Kituo cha Usaidizi
true
true
true
true
true
59
false
false