Kichupo cha Hadhira katika Takwimu za YouTube kinakupa muhtasari wa wanaotazama video zako za YouTube na maarifa kuhusu demografia zao. Kinatoa muhtasari wa haraka wa vipimo muhimu kama vilewatazamaji wanaorudi tena, watazamaji wa kipekee na wanaofuatilia.
Angalia ripoti za Hadhira yako
- Ingia katika Studio ya YouTube.
- Katika Menyu ya kushoto, chagua Takwimu .
- Kwenye menyu ya juu, chagua Hadhira.
Ripoti za hadira
Video zinazokuza hadhira yako
Ripoti hii inaonyesha idadi ya watazamaji wapya na wanaorudi kwenye chaneli yako. Unaweza kuitumia kuelewa ni maudhui gani yanayowavutiwa watazamaji wengi wapya.
Watazamaji wako wanapotumia YouTube
Ripoti hii hukuonyesha wakati ambao watazamaji wako wanakuwa mtandaoni kwenye YouTube katika siku 28 zilizopita. Unaweza kuitumia ili ikusaidie kukuza jumuiya yako, kufahamu wakati wa kuratibu Onyesho la kwanza au kupanga kuhusiana na mtiririko wako mubashara unaofuata.
Arifa za kengele kwa wanaofuatilia kituo
Ripoti hii hukufahamisha asilimia ngapi ya wanaofuatilia chaneli yako wanapata arifa za kengele kutoka kwenye chaneli yako. Pata maelezo zaidi kuhusu arifa kwa wanaofuatilia chaneli.
Muda wa kutazama wa wanaofuatilia chaneli
Ripoti hii inakufahamisha ni asilimia ngapi ya muda wa kutazama inatokana na wanaofuatilia na watazamaji wasiofuatilia chaneli yako.
Umri na jinsia
Ripoti hii inakuonyesha upeo wa umri unaotazama chaneli yako kwa muda mrefu zaidi na usambaaji wa hadhira yako kwa misingi ya jinsia.
Chaneli ambazo hadhira yako hutazama
Ripoti hii hukuonyesha chaneli nyingine ambazo watazamaji wako wametazama mara kwa mara nje ya chaneli yako katika siku 28 zilizopita. Unaweza kuitumia kufahamu chaneli zinazowavutia watazamaji wako na kupata fursa za kushirikiana.
Maudhui ambayo hadhira yako inatazama
Ripoti hii inakuonyesha ni video, Video Fupi, mitiririko mubashara na podikasti zipi nyingine ambazo watazamaji wako walitazama nje ya chaneli yako katika siku saba zilizopita. Unaweza kuitumia kupata mada za video mpya na majina. Unaweza pia kutumia maelezo haya kupata mitindo ya vijipicha na fursa za kushirikiana. Iwapo una Chaneli Rasmi ya Msanii, hutaona video ambazo wewe ni msanii mkuu, hata video ikiwa nje ya Chaneli yako Rasmi ya Msanii.
Miundo ya maudhui ambayo watazamaji wako wanatazama kwenye YouTube
Ripoti hii inakuonyesha aina ya miundo ambayo watu wametazama katika siku 28 zilizopita. Miundo hiyo inaweza kuwa ya video, Video Fupi au mitiririko mubashara. Unaweza kutumia ripoti hii ili uangalie miundo ya maudhui ambayo watu wanatazama sana ili ubadilishe muundo wako uwe kama hiyo.
Maeneo ya kijiografia ambako wametazama zaidi
Ripoti hii inakuonyesha maeneo ya kijiografia ambako chaneli yako imetazamwa kwa muda mrefu zaidi.
Lugha maarufu za manukuu
Ripoti hii inaonyesha hadhira ya chaneli yako kulingana na lugha yenye manukuu.
Vipimo unavyopaswa kujua
Watazamaji wanaorudi tena | Idadi ya watazamaji ambao tayari wametazama kituo chako, na wamerudi kukitazama katika kipindi kilichochaguliwa. |
Watazamaji wapya | Idadi ya watazamaji waliotazama kituo chako kwa mara ya kwanza katika kipindi kilichochaguliwa. Watazamaji ambao hutazama kwenye kivinjari cha faragha, waliofuta historia ya video walizotazama, au ambao hawajatazama kituo chako kwa zaidi ya mwaka mmoja huchukuliwa kuwa watazamaji wapya. |
Watazamaji wa kipekee | Kadirio la idadi ya watazamaji ambao wametazama maudhui yako ndani ya kipindi kilichochaguliwa. |
Wanaofuatilia | Idadi ya watazamaji ambao wanafuatilia kituo chako. |
Muda wa kutazama (saa) | Muda ambao watazamaji wametazama video yako. |
Utazamaji | Idadi halali ya mara ambazo chaneli na video zako zilitazamwa. |