Kuelewa ufikiaji wa video yako ya YouTube

Kichupo cha Ufikiaji katika Takwimu za YouTube ni muhimu katika kukusaidia kuelewa jinsi watazamaji wanavyopata maudhui yako. Kinatoa muhtasari wa haraka wa vipimo muhimu kama vile asilimia ya mibofyo, muda wa kutazama, utazamaji na vipimo vingine.

Kumbuka: Huenda baadhi ya ripoti zisipatikane kwenye vifaa vya mkononi.

Tazama ripoti zako za Ufikiaji

  1. Ingia katika Studio ya YouTube.
  2. Kwenye menyu ya kushoto, chagua Maudhui .
  3. Kwenye video uliyochagua, teua Takwimu .
  4. Kwenye Menyu ya juu, chagua Ufikiaji.

Ripoti za ufikiaji

Jinsi watazamaji wanavyopata video hii

Ripoti ya aina za vyanzo vya watazamaji inakuonyesha jinsi watazamaji walivyopata maudhui yako kwenye YouTube na vyanzo vya nje.

Programu au tovuti za nje

Ripoti ya nje inakuonyesha tovuti na programu mahususi za nje ambako watazamaji walipata maudhui yako.

Maudhui yanayopendekeza video hii

Ripoti ya video zinazopendekezwa inakuonyesha video ambazo watazamaji walitazama kutoka kwenye mapendekezo.

Orodha zinazoangazia video hii

Ripoti ya orodha inakuonyesha ni orodha zipi ziliwaelekeza watazamaji kwenye maudhui yako.

Maonyesho na jinsi yalivyoathiri muda wa kutazama

Maonyesho na jinsi yalivyochangia katika ripoti ya muda wa kutazama hukupa taswira ya jinsi maonyesho ya kijipicha chako yalivyochangia katika mara za kutazama na muda wa kutazama. Pata maelezo zaidi kuhusu vidokezo vya kutumia maonyesho na data ya asilimia ya mibofyo (CTR).

Arifa za kengele zilizotumwa

Ripoti hii hukufahamisha asilimia ngapi ya wanaofuatilia chaneli yako wanapata arifa za kengele kutoka kwenye chaneli yako. Pata maelezo zaidi kuhusu arifa kwa wanaofuatilia chaneli.

Hoja za utafutaji kwenye YouTube

Ripoti ya utafutaji kwenye YouTube inakuonyesha maneno ambayo watazamaji walitafuta walipopata maudhui yako.

Fahamu aina za vyanzo vya watazamaji

Chanzo cha watazamaji kwenye video zako kinaweza kuwa ndani ya YouTube au kutoka vyanzo vya nje. Utaona vyanzo vyote viwili kwenye kadi ya “Jinsi watazamaji wanavyopata video hii”.

Wanaotazama kwenye YouTube
Vipengele vya kuvinjari Wanaotazama kutokana na ukurasa wa Kwanza, wanaokufuatilia, Tazama Baadaye, Zinazovuma au Gundua na vipengele vingine vya kuvinjari.
Kurasa za chaneli Watazamaji kutokana na chaneli yako ya YouTube au chaneli nyingine za YouTube.
Kadi za kampeni Watazamaji kutokana na kadi za kampeni ya mmiliki wa maudhui.
Skrini za mwisho Watazamaji kutokana na skrini za mwisho za mtayarishi.
Video Fupi Watazamaji kutoka hali ya mtazamo wa wima wa Video Fupi.
Arifa Watazamaji kutokana na arifa na barua pepe zilizotumwa kwa wanaokufuatilia.
  Arifa kwa wafuatiliaji waliowasha kengele Watazamaji kutokana na arifa zinazotumwa kwa wanaokufuatilia waliowasha "Arifa zote" kwenye chaneli yako na arifa za YouTube kwenye vifaa vyao.
  Arifa zingine za programu Wanaotazama kutokana na arifa zilizowekewa mapendeleo, arifa za barua pepe, kikasha na muhtasari.
Vipengele vingine vya YouTube Watazamaji kutoka ndani ya YouTube ambao hawajabainishwa katika aina nyingine yoyote.
Orodha

Watazamaji kutokana na orodha yoyote iliyojumuisha mojawapo ya video zako. Orodha hizi zinaweza kuwa zako au za mtayarishi mwingine. Pia hujumuisha takwimu kutoka kwenye "Video Ulizopenda" na "Video Pendwa" za orodha za kucheza za watumiaji.

Unaweza kuona orodha mahususi za kucheza zilizovutia watazamaji katika video zako kwenye kadi ya “Chanzo cha watazamaji: Orodha za kucheza" katika kichupo cha Ufikiaji.

Video ya mseto Watazamaji kutoka miseto inayoonekana ya maudhui yako.
Kurasa za sauti Watazamaji kutokana na ukurasa ulioshirikiwa wa matokeo ya sauti unaopatikana katika hali ya mtazamo wa wima wa Video Fupi.
Video zilizopendekezwa Watazamaji kutokana na mapendekezo yanayoonekana karibu na au baada ya video zingine na kutokana na viungo vilivyo katika maelezo ya video. Unaweza kuona video mahususi kwenye kadi ya “Chanzo cha watazamaji: Video zilizopendekezwa” katika kichupo cha Ufikiaji.
Kadi za video Watazamaji wanaotokana na kadi katika video nyingine.
Utangazaji kwenye YouTube

Iwapo video yako imetumika kama tangazo kwenye YouTube, utaona “Utangazaji kwenye YouTube” kama chanzo cha watazamaji.

Mara za kutazama kutokana na matangazo yanayoweza kurukwa yenye urefu wa zaidi ya sekunde 10 inahesabiwa iwapo yametazamwa kwa sekunde 30 au hadi yanapoisha. Matangazo yasiyoweza kurukwa hayatimizi vigezo vya kujumuishwa kwenye Takwimu za YouTube za mara za kutazamwa.

Utafutaji kwenye YouTube Watazamaji kutokana na matokeo ya utafutaji kwenye YouTube. Unaweza kuona hoja mahususi za utafutaji kwenye kadi ya “Chanzo cha watazamaji: Utafutaji kwenye YouTube” wa kichupo cha Ufikiaji.
Kurasa za bidhaa Watazamaji kutokana na kurasa za bidhaa za YouTube.
Watazamaji kutokana na vyanzo vya nje
Vyanzo vya nje Wanaotazama kutoka kwenye tovuti na programu ambako video yako ya YouTube imepachikwa au kuunganishwa kwayo. Unaweza kuona tovuti na vyanzo mahususi vya nje kwenye kadi ya “Tovuti au programu za nje” katika kichupo cha Ufikiaji.
Vyanzo vya moja kwa moja au visivyojulikana Watazamaji kutokana na URL inayowekwa moja kwa moja, alamisho, watazamaji walioondoka kwenye akaunti na programu zisizobainishwa.

Vipimo unavyopaswa kujua

Maonyesho

Mara ambazo vijipicha vyako vilionyeshwa kwa watazamaji kwenye YouTube kupitia maonyesho yaliyohesabiwa.

Asilimia ya mibofyo kwenye maonyesho

Mara ambazo watazamaji walitazama video baada ya kuona kijipicha.

Inaonyeshwa kwenye mipasho Mara ambazo Video yako fupi inaonyeshwa kwenye Mipasho ya Video Fupi.
Waliotazama (ikilinganishwa na ambao hawakutazama) Asilimia ya mara ambazo watazamaji walitazama Video zako Fupi ikilinganishwa na mara ambazo hawakutazama.

Utazamaji

Idadi halali ya mara ambazo vituo na video zako zilitazamwa.

Watazamaji wa kipekee

Kadirio la idadi ya watazamaji waliotazama maudhui yako katika kipindi ulichochagua.

Wastani wa kipindi cha kutazama

Makadirio ya wastani wa dakika zilizotazamwa kwa kila tukio la kutazama katika kipindi na video uliyochagua.

Muda wa kutazama (saa) Muda waliotumia watazamaji kutazama video yako.

Je, maelezo haya yamekufaa?

Tunawezaje kuboresha?

Je, unahitaji usaidizi mwingine?

Jaribu hatua zifuatazo:

Tafuta
Futa utafutaji
Funga kisanduku cha kutafutia
Menyu kuu
8109372560554293567
true
Tafuta kwenye Kituo cha Usaidizi
true
true
true
true
true
59
false
false