Ufafanuzi wa “matangazo machache au kutoonyeshwa kwa matangazo yoyote”

Utaona aikoni za “matangazo machache au kutoonyeshwa kwa matangazo yoyote” ( au ) ikiwa tu uko kwenye Mpango wa Washirika wa YouTube.

Aikoni hii inamaanisha kuwa umewasha kipengele cha uchumaji wa mapato kwenye video, lakini mifumo yetu ya kiotomatiki au wataalamu wa sera wanaamini kuwa video hiyo haifuati mwongozo wetu wa maudhui yanayofaa watangazaji. Unaweza kuchuma mapato madogo kwenye maudhui haya (kwa sababu matangazo machache yanaweza kuonyeshwa) ikilinganishwa na maudhui yanayofaa watangazaji wote.

Katika hali fulani, unaweza kukata rufaa dhidi ya uamuzi huu. Ikiwa huna uhakika, kagua maudhui yako ukizingatia makala yetu ya mifano ya maudhui yanayofaa watangazaji. Ikiwa bado unafikiri kuwa hayapaswi kuwekwa katika hali ya “matangazo machache au kutoonyeshwa kwa matangazo yoyote”, unaweza kuomba tufanye uhakiki wa binadamu.

Pata maelezo zaidi kuhusu jinsi aikoni zetu za uchumaji wa mapato zinavyokuathiri.

Je, maelezo haya yamekufaa?

Tunawezaje kuboresha?
Tafuta
Futa utafutaji
Funga kisanduku cha kutafutia
Menyu kuu
8480862579109263661
true
Tafuta kwenye Kituo cha Usaidizi
true
true
true
true
true
59
false
false