Maswali Yanayoulizwa Sana kuhusu kukataliwa kwa chaneli yangu kwenye mpango wa uchumaji wa mapato

Kwa nini nilikataliwa kwenye mpango wa uchumaji wa mapato?

Ikiwa ombi lako la Mpango wa Washirika wa YouTube (YPP) lilikataliwa, ina maana kwamba wakaguzi wetu wanaamini kuwa sehemu kubwa ya chaneli yako haikidhi sera na mwongozo wetu. Ili upate maelezo kuhusu hatua zinazofuata, angalia maswali mengine katika makala haya.

Ninaweza kutuma ombi tena?

Ndiyo. Ikiwa ni mara yako ya kwanza kukataliwa, unaweza kutuma ombi tena kwenye Mpango wa Washirika wa YouTube siku 30 baada ya kupokea barua pepe yako ya kukataliwa. Ikiwa si mara yako ya kwanza kukataliwa au ulituma tena ombi hapo awali, unaweza kutuma ombi baada ya siku 90 tangu ulipopokea barua pepe ya kukataliwa. Utatakiwa kukagua chaneli yako ili ufahamu ikiwa inakiuka sera kabla ya kutuma ombi tena.

Ikiwa unaamini kuwa chaneli yako ilikataliwa kimakosa kwenye Mpango wa Washirika wa YouTube (YPP), una chaguo la kukata rufaa ndani ya siku 21, bila kujali idadi ya majaribio ya kutuma maombi. 

Nifanye nini ili ombi langu liwe thabiti?

Hatuwezi kukuahidi kuwa utaweza kuchuma mapato baada ya kurekebisha chaneli yako. Lakini tuna mwongozo wa jumla wa kukusaidia ufanye chaneli yako itimize masharti ya mpango huu.

  1. Soma barua pepe ya kukataliwa. Itakufahamisha sera mahususi ambazo chaneli yako ilikiuka.
  2. Kisha, kagua maudhui yako (video, majina, maelezo, vijipicha na lebo) ukilinganisha na Sera zetu za uchumaji mapato kwenye chaneli za YouTube na Mwongozo wetu wa Jumuiya.
  3. Hatua itakayofuata ni kuhariri au kufuta video zozote zinazokiuka sera zetu.

Iwapo utatuma ombi tena, timu yetu ya ukaguzi itakagua tena kwa umakini maudhui yako. Tutakutumia barua pepe ili kukufahamisha mchakato huu utakapokamilika (huchukua takribani mwezi mmoja). Unaweza pia kuangalia hali ya ombi lako kwenye Sehemu ya kuchuma mapato ya Studio ya YouTube.

Je, maelezo haya yamekufaa?

Tunawezaje kuboresha?
Tafuta
Futa utafutaji
Funga kisanduku cha kutafutia
Menyu kuu
14663086184531534544
true
Tafuta kwenye Kituo cha Usaidizi
true
true
true
true
true
59
false
false