Kutafuta makala yanayohakikisha ukweli katika matokeo ya utafutaji kwenye YouTube

Vidirisha vya maelezo hutoa muktadha zaidi kuhusu video kwenye YouTube. Utagundua aina tofauti za maelezo kutoka kwenye vyanzo vingine, kama vile viungo vya makala yanayohakikisha ukweli katika matokeo ya utafutaji. Tunakupa muktadha huu ili ukusaidie kufanya uamuzi wako mzuri kuhusu video unazotazama kwenye YouTube.

Unapotafuta jambo linalohusiana na dai mahususi kwenye YouTube, wakati mwingine utagundua kidirisha cha maelezo. Vidirisha hivi hujumuisha makala yanayohakikisha ukweli kutoka kwa mchapishaji huru mwingine. Maelezo haya hukuelezea ikiwa madai yako yanayohusiana ni ya kweli, uongo au jambo jingine kama vile "ukweli kwa kiasi fulani," kulingana na makala yanayohakikisha ukweli wa mchapishaji.

Vidirisha vya maelezo hupatikana tu katika idadi ndogo ya nchi au maeneo na lugha. Tunajitahidi kuweka vidirisha vya maelezo katika nchi au maeneo zaidi.

Jinsi makala yanayohakikisha ukweli yanaonekana kwenye YouTube

Iwapo mchapishaji amehakikisha ukweli wa jambo mahususi kwa utafutaji wako, utagundua kidirisha cha maelezo chenye alama ya "ukweli umehakikishwa" na:

  • Jina la mchapishaji anayehakikisha ukweli
  • Dai kuwa ukweli umehakikishwa
  • Muhtasari wa matokeo ya shughuli ya kuhakikisha ukweli iliyofanywa na mchapishaji
  • Kiungo cha makala ya mchapishaji ili upate maelezo zaidi
  • Maelezo kuhusu tarehe ya kuchapishwa kwa makala ya kuhakikisha ukweli

Wakati kuna makala yanayohusiana yanayohakikisha ukweli kutoka kwa wachapishaji kadhaa, utagundua matokeo machache.

Iwapo huoni makala ya kuhakikisha ukweli

Makala ya kuhakikisha ukweli hayaonekani kwa kila utafutaji. Kuna vigezo kadhaa vinavyoathiri ikiwa makala yanayohakikisha ukweli yataonekana. Kimsingi, ikiwa hoja za utafutaji zinatafuta maelezo dhahiri kuhusu usahihi wa dai. Pia, tunazingatia ufaafu na upya wa makala yanayohakikisha ukweli kulingana na hoja za utafutaji.

Iwapo makala yanayohakikishwa ukweli hayaonekani, inaweza kuwa ni kwa sababu mchapishaji anayetimiza masharti hajachapisha makala yanayohakikisha ukweli yanayohusu utafutaji wako. YouTube haitoi maelekezo ya uhariri kuhusu makala yanayohakikisha ukweli au mifumo ya ukadiriaji inayoonekana katika vidirisha vya maelezo.

Maoni kuhusu makala yanayohakikisha ukweli

YouTube haiidhinishi au kutunga makala yoyote yanayohakikisha ukweli yanayoonyeshwa katika vidirisha vya maelezo kwenye YouTube. Ikiwa hukubaliani na maelezo katika makala mahususi yanayohakikisha ukweli, wasiliana na mmiliki wa tovuti aliyechapisha makala hayo. Ikiwa utapata makala ya kuhakikisha ukweli yanayokiuka Mwongozo wetu wa Jumuiya, unaweza kututumia maoni.

Nani huchapisha makala yanayohakikisha ukweli

Makala ya kuhakikisha ukweli yanayoonyeshwa kwenye YouTube hutumia lebo ya Schema.org ClaimReview inayopatikana hadharani na wachapishaji wanastahiki kushiriki ikiwa:

  • Mchapishaji ni mtu aliyethibitishwa kutia sahihi kwenye Kanuni za Maadili za Mtandao wa Kimataifa wa Kuhakikisha Ukweli au mchapishaji wa kuaminika.

NA

Wachapishaji na makala yao yanayohakikisha ukweli hukaguliwa mara kwa mara ili kuhakikisha:

  • Makala yanayohakikisha ukweli yanafuata Mwongozo wa Jumuiya ya YouTube.
  • Makala yanayohakikisha ukweli yanadhibitiwa na mwongozo wa data iliyopangwa ya ClaimReview.
  • Makala yanayohakikisha ukweli yana madai ya kipekee na ukadiriaji wazi unaopatikana kwa urahisi kwenye sehemu kuu ya makala. 
  • Mbinu na vyanzo vya makala yanayohakikisha ukweli:
    • vinaweza kufuatiliwa
    • viko wazi
    • vina manukuu na marejeleo ya vyanzo msingi

Huenda makala yasistahiki kufanyiwa uhakiki wa ukweli ikiwa makala hayo au mchapishaji hafuati mwongozo huu. Pia, inawezekana kwamba mchapishaji anaweza kukosa uwezo wa kuonyesha makala ya kuhakikisha ukweli kwenye YouTube.

Kumbuka: Nchini Marekani, tunaonyesha tu makala yanayohakikisha ukweli kutoka kwa wachapishaji walio Marekani.

Jinsi tunavyobainisha kuaminika

Tunatumia ishara kadhaa kupima hali ya kuaminika ili kuhakikisha kuwa maudhui yanayotoka kwenye vyanzo thabiti na vinavyofaa ndiyo tu yanayoonekana kwenye vidirisha vyetu vya maelezo. Pia, tunatumia wakadiriaji wa nje kutathmini utaalamu na uaminifu wa maudhui. Tunajitahidi zaidi kuimarisha bidhaa zetu na kutekeleza sera zetu. Vitendo hivi hutusaidia kuhakikisha kwamba mielekeo ya kiitikadi au kisiasa haijumuishwi katika tathmini ya vyanzo vya kuaminika.

Je, maelezo haya yamekufaa?

Tunawezaje kuboresha?
Tafuta
Futa utafutaji
Funga kisanduku cha kutafutia
Menyu kuu
1681576640991992791
true
Tafuta kwenye Kituo cha Usaidizi
true
true
true
true
true
59
false
false