Kuanzisha mtiririko mubashara kupitia kamera ya wavuti

Kamera ya wavuti ni njia rahisi ya kutiririsha mubashara ukitumia kompyuta yako, bila kuhitaji programu ya usimbaji ya kutiririsha mubashara.

Jinsi ya Kuanzisha Mtiririko Mubashara wa Kamera ya Wavuti kwenye YouTube

 

  1. Hakikisha umeruhusu akaunti yako iweze kutiririsha mubashara. Kutiririsha kupitia kamera ya wavuti kunawezekana kwenye Chrome 60+ na Firefox 53+.
  2. Ingia kwenye YouTube.
  3. Upande wa juu kulia, bofya Buni  kisha Mubashara.
  4. Katika upande wa kushoto, chagua Kamera ya wavuti .
  5. Weka jina na maelezo kisha uchague mipangilio ya faragha. Unaweza pia kuratibu mtiririko wako mubashara ili ufanyike tarehe ya baadaye.
    • For users aged 13–17 on YouTube, your default privacy setting is set to private. If you’re 18 or over, your default privacy setting is set to public. All streamers can change this setting to make their live stream public, private, or unlisted.
  6. Bofya Chaguo zaidi kisha Mipangilio ya Kina kwa mipangilio zaidi.
  7. Bofya Inayofuata. Kamera yako itapiga kijipicha.
  8. Hakikisha umechagua kamera ya wavuti na maikrofoni sahihi.
  9. Bofya Tiririsha Mubashara.
  10. Ili udhibiti mtiririko wako, kama vile kuongeza lebo, kubadilisha mipangilio ya uchumaji wa mapato, gumzo na zaidi, bofya Badilisha. Unaweza kubadilisha mipangilio hii wakati wowote, iwe unatiririsha mubashara au la.
  11. Unapomaliza kutiririsha, bofya Maliza Kutiririsha iliyo katika sehemu ya chini. Mitiririko yote iliyo na urefu wa chini ya saa 12 itawekwa kiotomatiki kwenye kumbukumbu. Unaweza kufikia mitiririko iliyopita, ya sasa na ijayo kwenye Kichupo cha Moja kwa Moja.
Kumbuka: Ili ufikie au uanzishe mtiririko mubashara ulioratibiwa, nenda kwenye Ukurasa wa Kudhibiti Utiririshaji wa Moja kwa Moja na uchague Dhibiti.

Kutumia Paneli Dhibiti ya Mubashara

Unapotiririsha mubashara, unaweza kutumia toleo dogo la Ukurasa wa kudhibiti utiririshaji wa moja kwa moja (Paneli Dhibiti ya Mubashara) ili upunguze eneo la skrini unalohitaji katika mtiririko wako. Paneli Dhibiti ya Mubashara hukuonyesha taarifa muhimu kutoka kwenye Ukurasa wa kudhibiti utiririshaji wa moja kwa moja, kama vile mapato ya Gumzo na Utazamaji, katika eneo dogo zaidi la skrini

Ili ufungue Paneli Dhibiti ya Mubashara:

  1. Katika Ukurasa wa Kudhibiti Utiririshaji wa Moja kwa Moja, nenda kwenye dashibodi ya mtiririko.
  2. Katika kona ya chini kushoto, bofya dashibodi Ibukizi Pop out .

Ili ufunge Paneli Dhibiti ya Mubashara, ondoka kwenye dirisha.

Kumbuka: Unaweza kutumia kipengele cha Paneli Dhibiti ya Mubashara unapotiririsha mubashara ukitumia programu ya kusimba au kamera ya wavuti pekee.
 

Kuruhusu Skrini yako ifikiwe kwenye Ukurasa wa kudhibiti utiririshaji wa moja kwa moja ukitumia kamera ya wavuti

Unapotiririsha mubashara ukitumia Ukurasa wa kudhibiti utiririshaji wa moja kwa moja kupitia kamera ya wavuti, sasa unaweza kuruhusu skrini yako ifikiwe. Baada ya kutiririsha mubashara ukitumia kamera ya wavuti:

  1. Bofya RUHUSU SKRINI IFIKIWE , katika sehemu ya chini katikati, karibu na kitufe cha maikrofoni.
  2. Chagua skrini yako nzima, dirisha au kichupo.
    • Ukiwasilisha kichupo cha kivinjari kinachotumia kamera ya wavuti, hatua hiyo huruhusu ufikiaji wa sauti ya kivinjari kwa chaguomsingi.
    • Ili uwasilishe kichupo tofauti, chagua kichupo ambacho ungependa kuwasilisha, bofya Ruhusu ufikiaji wa kichupo hiki.
  3. Bofya Ruhusu ufikiaji.

Ili ukatishe ufikiaji wa skrini yako kwenye Ukurasa wa kudhibiti utiririshaji wa moja kwa moja:

  • Kwenye Ukurasa wa kudhibiti utiririshaji wa moja kwa moja, bofya Katisha Ufikiaji wa Skrini au
  • Katika kichupo cha dirisha la kivinjari, bofya Katisha ufikiaji wa skrini
Kumbuka: Unaweza tu kuruhusu ufikiaji wa skrini kwenye Ukurasa wa kudhibiti utiririshaji wa moja kwa moja ikiwa kamera ya wavuti na maikrofoni zimeunganishwa. 

Kuweka kionjo kwenye mtiririko wako mubashara

Changamsha hadhira yako kuhusu mtiririko wako mubashara ulioratibiwa kwa kuonyesha kionjo. Kionjo chako kitachezwa kwa watazamaji kwenye ukurasa wa kutazama kabla mtiririko mubashara haujaanza. 

Vionjo vinaweza kuchezwa tu kwenye mitiririko iliyoratibiwa katika kichupo cha “Dhibiti” kwenye Ukurasa wa kudhibiti utiririshaji wa moja kwa moja.

  1. Kupakia kionjo chako kwenye kituo chako cha YouTube sawa na unavyopakia video ya kawaida.
  2. Nenda kwenye Studio ya YouTube > Tiririsha Mubashara.
  3. Tayarisha mtiririko mubashara ulioratibiwa au chagua mtiririko ulioratibiwa kwenye kichupo cha “Dhibiti”.
  4. Kwenye upande wa juu kulia, bofya Badilisha.
  5. Bofya Weka mapendeleo.
  6. Chini ya “Kionjo,” bofya Weka.
  7. Chagua video yako ya kionjo.
  8. Bofya Hifadhi.

Masharti ya Kujiunga

Kipengele hiki kinapatikana kwa watayarishi walio na zaidi ya watu 1,000 wanaofuatilia, wasio na maonyo kwa kukiuka Mwongozo wa Jumuiya

 

Masharti

  • Aina ya video: Tumia aina yoyote ya video inayoruhusiwa kwenye YouTube.
  • Urefu wa video: sekunde 15 – dakika 3.
  • Uwiano na ubora: Tunapendekeza uwiano na ubora ule ule uliotumia kwenye video ya Onyesho la kwanza.
  • Haki za sauti na video: Hakikisha kuwa kionjo hakikiuki haki za maudhui mengine.
Hakikisha kuwa hamna maudhui yatakayokiuka Mwongozo wetu wa Jumuiya.

Kudhibiti mitiririko mubashara

Kwenye dashibodi ya Studio ya YouTube, unaweza kufikia mitiririko mubashara ya sasa, ijayo na iliyopita. Hivi ndivyo utakavyofanya:
  1. Nenda kwenye Studio ya YouTube au studio.youtube.com.
  2. Kwenye menyu ya kushoto, chagua Maudhui.
  3. Bofya Kichupo cha mubashara .
    • Zinazotiririsha Mubashara Sasa: video zinazotiririshwa mubashara sasa.
    • Zijazo: video ambazo bado hazijatiririshwa, lakini zimesharatibiwa kutiririshwa wakati fulani.
    • Kucheza Tena Mubashara: video ambazo zilishatiririshwa mubashara.

Unaweza pia kufikia na kuanzisha mitiririko mubashara iliyoratibiwa katika Ukurasa wa kudhibiti utiririshaji wa moja kwa moja.

  1. Katika upande wa kushoto, chagua Dhibiti.
  2. Bofya mtiririko mubashara ulioratibiwa ambao ungependa kuanzisha.
  3. Bofya Tiririsha Mubashara.

Je, maelezo haya yamekufaa?

Tunawezaje kuboresha?
Tafuta
Futa utafutaji
Funga kisanduku cha kutafutia
Menyu kuu
12352590175848525070
true
Tafuta kwenye Kituo cha Usaidizi
true
true
true
true
true
59
false
false