Majaribio ya vipengele kwenye Youtube.com/new

Maelezo zaidi kuhusu majaribio ya vipengele vipya vya YouTube na jinsi ya kushiriki yanapatikana kwenye youtube.com/new.

Si vipengele vyote vinavyofanyiwa majaribio huishia kutumika. Unapojaribu kipengele kipya, toa maoni ya kina ili utusaidie kuboresha YouTube.

Ili ushiriki:

  1. Tembelea youtube.com/new kisha uingie katika Akaunti yako ya Google. Baadhi ya majaribio hufanywa kwa muda mfupi pekee. Majaribio haya yatapatikana kwa wanachama wa Premium pekee, kwa hivyo unahitaji kuwa mwanachama wa YouTube Premium ili uweze kushiriki katika majaribio.
  2. Ukiona jaribio ambalo ungependa kujaribu, chagua Ijaribu.
  3. Tumia kipengele ambacho umechagua na utoe maoni. 

Ili upate fursa ya kutoa maoni zaidi, unaweza kujisajili wakati wowote ili ushiriki katika mojawapo ya tafiti zetu.

Kutoa maoni: ​

  1. Tembelea youtube.com/new.
  2. Chagua Toa maoni.

Huenda pia ukaona ujumbe kwenye YouTube kukukumbusha uwasilishe maoni, hasa majaribio yanapokaribia kuisha.

Ili uondoke kwenye jaribio:

  1. Tembelea youtube.com/new.
  2. Bofya kitufe cha Zima karibu na jaribio.
Kumbuka: Unaweza tu kuzima majaribio ikiwa wewe ni mwanachama wa Premium. Usipojiondoa mapema, kipengele kinachofanyiwa majaribio kitatoweka kiotomatiki jaribio likikwisha, na hali yako ya utumiaji wa YouTube itarejea kawaida.

Je, maelezo haya yamekufaa?

Tunawezaje kuboresha?
Tafuta
Futa utafutaji
Funga kisanduku cha kutafutia
Menyu kuu
690830988870775714
true
Tafuta kwenye Kituo cha Usaidizi
true
true
true
true
true
59
false
false