Kadi Rasmi katika Utafutaji

Kadi Rasmi hurahishia watazamaji kugundua maudhui kwa kuangazia nyenzo rasmi katika Utafutaji kwenye YouTube. Kadi hizi ni pamoja na video rasmi kutoka chaneli maarufu, kama vile za watayarishi maarufu wa YouTube, watu mashuhuri na wasanii maarufu wa muziki, na vile vile maudhui yanayohusiana na timu za spoti, filamu na vipindi vya TV, muziki na matukio maalum. Kadi hizi hutolewa kiotomatiki na haziwezi kuwekewa mapendeleo.

Kadi za muziki

Kadi za Muziki zinaweza kuangazia msanii wa muziki, wimbo, aina au video za muziki na albamu za hivi majuzi. Unaweza pia kutazama maonyesho ya kwanza na mitiririko mubashara ya hivi majuzi kutoka kwa wasanii unaowapenda kwenye Kadi Rasmi za Wasanii. Kadi za Chati Maarufu huonyesha video za muziki na nyimbo bora kutoka YouTube Music katika Utafutaji. Pata maelezo zaidi kuhusu Chati za Muziki na Maarifa.

Kadi za Spoti

Kadi za Spoti huonyesha timu za spoti, michezo ijayo au mubashara, mashindano au maudhui ya aina tofauti za spoti. Kadi hizi zinaweza pia kuangazia alama za hivi majuzi, vivutio na timu zinazohusiana.

Kadi za TV

Kadi za TV zinaangazia mitandao au vipindi mahususi. Kwa kawaida zinajumuisha vipindi na misimu ya hivi karibuni, na zinaweza kuoneysha kitufe cha kujisajili ikiwa kuna chaneli iliyothibitishwa. Maonyesho fulani yanaweza kupatikana bila gharama yoyote ya kifedha, kuhitaji malipo ya mara moja au kupatikana kwa waliojisajili kwenye Premium pekee.

Kadi za michezo ya video

Kadi za Michezo ya Video hujumuisha maudhui rasmi yanayohusiana na mchezo husika wa video. Kuchagua Kadi ya Mchezo wa Video huonyesha maudhui zaidi kuhusu mchezo kama vile mitiririko mubashara na vipakiwa vya hivi karibuni na video maarufu.

Kadi za matukio maalum

Kadi za Matukio Maalum zinajumuisha maudhui kuhusu matukio kama vile matamasha ya muziki na mashidano makubwa ya spoti, kama vile Kombe la Dunia.

Kadi Rasmi za Taarifa Binafsi

Kadi Rasmi za Taarifa Binafsi huonekana kwa watu mbalimbali wanaotafutwa sana kwenye YouTube, ambao wanajulikana pia kwenye YouTube na nje ya YouTube, kama vile waigizaji, wanamuziki, wanariadha na Watayarishi maarufu wa YouTube. Kadi hizi zina kitufe cha Jisajili na zinaangazia video iliyopakiwa hivi karibuni kabisa.

Kumbuka: Kadi Rasmi za Taarifa Binafsi zinapatikana kwa idadi ndogo ya watu kwa sasa. Huwezi kuomba kadi hizi, lakini tuna mpango wa kufikia chaneli zaidi katika siku zijazo.

Kadi za Mshika Ofisi

Kadi za Mshika Ofisi zitaonyeshwa katika hoja za utafutaji kuhusu:

  • Majina ya viongozi wa tawi la serikali wenye mamlaka ya serikali. Kulingana na nchi, hii inajumuisha Waziri MKuu, Rais na jukumu lingine lolote, ambalo lina mamlaka ya utawala wa taifa.
  • Ofisi ya tawi la serikali yenye mamlaka ya serikali.
Kumbuka: Kadi ya Mshika Ofisi inapatikana tu katika baadhi ya nchi. Haitaonyeshwa katika kipindi cha kuelekea kwenye uchaguzi wa jukumu hili.

Kadi za Rasmi za Vyama vya Siasa

Katika nchi ambapo kipengele kinapatikana, Kadi Rasmi za Vyama vya Siasa zinaweza kuonyeshwa katika hoja faafu za utafutaji. Ustahiki unatokana na uwakilishi na uchaguzi wa chama cha siasa kwenye aina ya serikali ya uwakilishi na kitaifa kama chama cha siasa kilichochaguliwa na wengi.

Kumbuka: Kwa sasa, kadi rasmi za Vyama vya Siasa zinatumika Marekani pekee.

Kadi rasmi za Podikasti

Kadi rasmi za podikasti huangazia maonyesho mahususi ya podikasti na vipindi vya hivi karibuni kabisa vya onyesho hilo.

Kumbuka: Kadi rasmi za podikasti zinatumiwa na watayarishi wachache wa podikasti. Tunapanga kufikia chaneli zaidi katika siku zijazo.

 

Je, maelezo haya yamekufaa?

Tunawezaje kuboresha?
Tafuta
Futa utafutaji
Funga kisanduku cha kutafutia
Menyu kuu
8292662955180914547
true
Tafuta kwenye Kituo cha Usaidizi
true
true
true
true
true
59
false
false